Posts

Bangi ilikuwa ikichomwa wakati wa ibada' na Waisraeli wa zamani

Image
waisraeli wa jadi walichoma bangi ikiwa miongoni mwa tamaduni za kufanya ibada za kidini , utafiti wa matukio ya zamani umebaini. Mabaki yaliohifadhiwa katika hekalu hilo lenye umri wa miaka 2,700 mjini Tel Arad yametambuliwa kuwa bangi. Watafiti walibaini kwamba bangi huenda iichomwa ili kuwashawishi waumini. Huu ni ushahidi wa kwanza wa dawa za kisaikolojia zilizotumiwa katika ibada za zamani za Kiyahudi, kulingana na ripoti ya vyombo vya habari vya Israeli. Hekalu hilo liligunduliwa mara ya kwanza katika jangwa la Negev yapata kilomita 95 kusini mwa mji wa Tel-Aviv miaka ya 60. Katika utafiti huo mpya, uliochapishwa katika chuo kikuu jarida la matukio ya zamani katika chuo kikuu cha Tel aviv , watafiti hao wa mambo ya zamani wanasema kwamba madhabahu mawilili yaliojengwa na mawe ya chokaa yalikuwa yamezikwa katika eneo hilo takatifu. Hali kavu ya hewa na kuzikwa kwa mabaki hayo yalisababisha kuhifadhika juu ya madhabahu hayo. Ubani ulipatikana katika dhabahu moja , kitu ambacho sio

Maana ya Kuning'iniza Viatu Juu ya Nyaya za Umeme

Image
Ushwahi kuona viatu vimening'inizwa juu ya nyaya za umeme hapo mahali unapoishi au mahali popote ulipowahi kutembelea? Je,unajua ina maana gani? Usijali tupo hapa kukujuza yote haya. Kitendo hiki kimetapakaa sana siku hizi za karibuni lakini wengi wetu hatujui maana halisi ya kitendo hiki,hakika kina maana nyinghi tofauti tofauti hivyo huwezi kutafsiri kwa jumla ya vitendo vyote kila mahali,ifuatayo ni oropdha ya maana hizo 01# HUWAKILISHA MAHALI PAUZWAPO DAWA ZA KULEVYA  Mara nyingi uonapo viatu vimening'inizwa juu ya nyaya za umeme maana yake eneo la karibu na hapo panauzwa dawa za kulevya.kwa mfano kuna gazeti moja la huko LOS ANGELES,CALIFORNIA lilieleza kuwa hofu ya wakazi wengi wa LOS ANGELES ni kuwa viatu hivyo huwakilisha maeneo yauzwapo dawa za kulevya. 02# HUFANYIKA KUTOKANA NA UKOROFI Baadhi ya wahalifu walieleza ni kwanini kitendo hiki kinafanyika ,baadhi yao walieleza kuwa ni kutokana na ukorofi,yaani mtu mkorofi huweza kuiba viatu na kuvining'iniza juu ya nyay

Shemeji hiyo mitego yako dawa Yako iko Jikoni

Image
sana amani ndio maana huwa najisikia vibaya sana ikitokea nimemkwaza mtu wangu yoyote wa karibu kwani najiuliza atanisamehe kweli kwa hili kosa nililomfanyia? Historia ya maisha yangu imenifanya niwe na moyo huu wakutopenda kumkwaza mtu kwani nimefadhiliwa sana na kaka yangu,nimepewa kila kitu muhimu ambacho kijana anastahili awe nacho kama vile simu nzuri,pesa ya matumizi achilia mbali ada ya masomo ya shule za private nilizosoma kuanzia kindergarten mpaka nimefika chuo kikuu,Kwa kweli kaka yangu ni mtu wa pekee sana maishani mwangu na hakika siwezi kulipa fadhila zake. Ameniamini sana kiasi cha kuwaananiachia gari lake anaposafiri niwehuru kulitumia muda wowote nitakao lakini kwa bahati mbaya moyoni nimekuwa mwenye huzuni sana kwani mke wa kaka yangu yaani shemeji amekuwa tatizo kila kaka akisafiri maana vituko anavyonifanyia sio siri nahisi kutamani kuhama kwake pasipohata kujua nitaenda wapi.  Shemeji anathubutuje kunitolea chozi akinililia eti anataka niwe namimi kimapenzi wakati

Sad Story:Siwezi Wachukia Wanawake wote..Ila Wamenitenda Sana

Image
Mimi ni kijana wa kiume nina miaka 24, makazi yangu ni jijini mwanza,nimeamua kushea story yangu ili niweze kupata ushauri kwa watu mbali mbali juu ya nini nifanye baada ya kutendwa katika kila uhusiano ninao anzisha naweza nikasema nilichelewa kidogo kujihusisha na mapenzi kwa mujibu wa Dunia ya sasa,na hii ni kwa sababu nimelelewa na kukua katika familia yenye maadili.  Siwez nikasema nina mvuto mkubwa saana , niko simpo tu kama profile pictures zangu zinavyojieleza lakini siku zote nimejikuta nikiwa kipenzi cha kinadada wengi kulingana na mazingira husika ntakayokua nikiishi, na binafsi me ni mwanamume mtanashati naejpenda sana, mpole na zaid ni mcheshi haswa pengine hizo ndiyo sababu..na story yangu ya mahusiano inaanza nikiwa na miaka 20,kipindi nilipojiunga katika chuo kimoja hapa mwanza.  Baada ya kufika pale chuoni nilijijengea idadi kubwa tu ya marafi na kama unavyojua mtu mcheshi hua ana malafiki wengi ,pamoja na hayo, ckua na mawazo kabisa ya kuwa na msichana k

Nani ni Muhimu Katika Maisha yako? Soma Hichi Kistori Kifupi cha Kufundisha

Image
Siku moja katika darasa la jioni la watu wazima, mwalimu wa saikolojia aliingia darasani na kuwaambia wanafunzi;  "Nataka tucheze mchezo, mtu yeyote yule naomba ajitolee aje hapa mbele" Mwanamke aitwae Cathy akatoka mbele. Mwalimu akamwambia aandike majina 30 ubaoni ya watu ambao anadhani ni wa muhimu katika maisha yake.  Cathy akaandika majina ya wanafamilia yake yaani mumewe na mwanae, ndugu, majirani na marafiki zake.  Mwalimu akamwambia Cathy afute majina matatu ambayo anadhani kwake sio ya muhimu sana kuzidi mengine. Cathy akafuta majina ya marafiki zake watatu.  Mwalimu akamwambia Cathy afute tena majina matano zaidi, Cathy akafuta majina ya majirani zake watano.  Hii iliendelea mpaka alipobakiwa na idadi ya watu wanne tu katika ubao. Haya yalikuwa majina ya wazazi wake, mumewe na mtoto wake wa pekee.  Darasa zima wakabaki kimya, baada ya kugundua kuwa huu sio mchezo wa Cathy peke yake sasa.  Mwalimu akamwambia Cathy afute majina mengine m

Fahamu Historia ya Condom..Ilipoanzia na Jinsi Ilivyogundulika na Kuanza Kutumika kwa Mara ya Kwanza..!!!

Image
KONDOMU ni kifaa/ zana iliyotengenezwa mahususi kuvalisha uume au kuwekwa ukeni wakati wa kujamiiana.Nazo hubana kutokana na umbile la uume au uke.  Kondomu hizi zipo za aina tofauti kutokana na muda na vipindi zilipotengenezwa, nazo ni kama ifuatavyo:-  Awamu ya I – zilizotengenezwa kwa mimea.  Hizi zilitengenezwa mahususi kama kinga dhidi ya maambukizo ya vimelea vya ugonjwa wa kaswende [ugonjwa wa kifaransa]  Awamu ya II – kutokana na utumbo wa kondoo.  Dr. Condom alifahamika kama mgunduzi wa kondomu hizi, naye alikuwa ni dakatari wa Mfalme Charles II.  Alimshauri Mfalme kutumia kama kinga kutokana na magonjwa ya zinaa kutokana na tabia yake ya kuwa na wanawake wengi nje ya ndoa yake.  Awamu ya III – kutokana na mpira  Hizi zilitengenezwa kwa urahisi na kwa wingi na zikawa ndizo pekee zenye uwezo wa kudhibiti mimba hadi miaka ya 1960 vilipogunduliwa na vidonge vya majira.  JE KONDOMU NI SALAMA?  Tunaelezwa kuwa kondomu hutengenezwa kwa ustadi mkubwa ki

Je, Una Malengo gani Katika Maisha?

Image
Je, leo unapofikiria maisha yako yaliyopita, unafurahi na kuridhika kuwa uliyaendesha vizuri au hauridhiki? Watu wengi husikitika hadi wakasema kama wengebahatika kupata nafasi kurudia maisha, wasingeishi kama walivyo sasa. Wanasema wangekuwa makini zaidi katika kupanga maisha yao ili kuyafanya yawe bora zaidi. Huenda hata wewe unafikiria hivyo. Lakini duniani tunaishi mara moja tu wala hatutarudi tena baada ya kufariki. Hivyo nafasi tulitonaayo ndiyo hii ya kurekebisha maisha yetu. Na wala hatujachelewa. Je tunawezaje kufanya maisha yetu yaliyosalia kuwa bora? Hebu tushirikiane kutaafakari kisa hiki tuone kama kitatusaidia kuboresha maisha: Kijana aliyemaliza chuo kikuu alikwenda kwa mwanafalsafa kumuomba amsaidie kuamua kazi itakayomfaa zaidi. Yule mwanafalsafa akamuuliza “ Kwani wewe unataka kazi gani?” Kijana akajibu, “ Nimekuja kwako kwa sababu sijui cha kufanya” Mwanafalsafa akamwambia Mimi sitaweza kukusaidia kama wewe mwenyewe hujui nini unachotaka. Labda fikiri na uniambie baa