Posts

Showing posts from June, 2020

Bangi ilikuwa ikichomwa wakati wa ibada' na Waisraeli wa zamani

Image
waisraeli wa jadi walichoma bangi ikiwa miongoni mwa tamaduni za kufanya ibada za kidini , utafiti wa matukio ya zamani umebaini. Mabaki yaliohifadhiwa katika hekalu hilo lenye umri wa miaka 2,700 mjini Tel Arad yametambuliwa kuwa bangi. Watafiti walibaini kwamba bangi huenda iichomwa ili kuwashawishi waumini. Huu ni ushahidi wa kwanza wa dawa za kisaikolojia zilizotumiwa katika ibada za zamani za Kiyahudi, kulingana na ripoti ya vyombo vya habari vya Israeli. Hekalu hilo liligunduliwa mara ya kwanza katika jangwa la Negev yapata kilomita 95 kusini mwa mji wa Tel-Aviv miaka ya 60. Katika utafiti huo mpya, uliochapishwa katika chuo kikuu jarida la matukio ya zamani katika chuo kikuu cha Tel aviv , watafiti hao wa mambo ya zamani wanasema kwamba madhabahu mawilili yaliojengwa na mawe ya chokaa yalikuwa yamezikwa katika eneo hilo takatifu. Hali kavu ya hewa na kuzikwa kwa mabaki hayo yalisababisha kuhifadhika juu ya madhabahu hayo. Ubani ulipatikana katika dhabahu moja , kitu ambacho sio

Maana ya Kuning'iniza Viatu Juu ya Nyaya za Umeme

Image
Ushwahi kuona viatu vimening'inizwa juu ya nyaya za umeme hapo mahali unapoishi au mahali popote ulipowahi kutembelea? Je,unajua ina maana gani? Usijali tupo hapa kukujuza yote haya. Kitendo hiki kimetapakaa sana siku hizi za karibuni lakini wengi wetu hatujui maana halisi ya kitendo hiki,hakika kina maana nyinghi tofauti tofauti hivyo huwezi kutafsiri kwa jumla ya vitendo vyote kila mahali,ifuatayo ni oropdha ya maana hizo 01# HUWAKILISHA MAHALI PAUZWAPO DAWA ZA KULEVYA  Mara nyingi uonapo viatu vimening'inizwa juu ya nyaya za umeme maana yake eneo la karibu na hapo panauzwa dawa za kulevya.kwa mfano kuna gazeti moja la huko LOS ANGELES,CALIFORNIA lilieleza kuwa hofu ya wakazi wengi wa LOS ANGELES ni kuwa viatu hivyo huwakilisha maeneo yauzwapo dawa za kulevya. 02# HUFANYIKA KUTOKANA NA UKOROFI Baadhi ya wahalifu walieleza ni kwanini kitendo hiki kinafanyika ,baadhi yao walieleza kuwa ni kutokana na ukorofi,yaani mtu mkorofi huweza kuiba viatu na kuvining'iniza juu ya nyay