Posts

KWANINI KUOA?

Image
Usioe kwasababu ya mvuto alonao utafeli! Usioe kwasababu ya kumuonea huruma,,mbeleni utafeli! Usioe kwasababu alikusaidia,,ukija kuamka usingizini utagundua umefeli mahala Kuna sababu moja tu ambayo itakufanya wewe uoe bila kujalisha hali,,mazingira au wakati,,,OA KWASABABU UMEMPENDA,, Ukimpenda hata akija kubadilika maumbile,,afilisike,,asiwe kama awali,,ile roho ya pendo dhidi yake itakufanya uwe na ndoa yenye amani na furaha siku zote hata kama wengine wanajiuliza huyu amewezaje kuendelea nae.

EPUKA KUISHI NA MTU PASUA KICHWA ATAKUTESA

Image
Umempa muda wa kufanya mabadiliko,,umechukua muda wako na kuwa mshauri kwake,,,lakini bado hataki kubadilika,, nikuambie kitu ndugu yangu,,usitaka kugombana na mwanamke au mwanaume ambae hataki kuwa bora kwako,,pia hataki kuijua na kuitumia thamani unayompa,,ni heri umuache aende zake ili awe na Uhuru wa kufanya mambo yake anayoona yanamfaa,, Kuendelea kumng'ang'ania ni kujiumiza kichwa tu,,mwache aende uupe na moyo wako pumziko huenda pia Mwenyezi Mungu akakubariki na mchumba mwingine ambae atakuwa bora zaidi na hata kama adipokupatia ni bora ukaishi pekee yako kuliko kuishi na mtu pasua kichwa.

HAKUNA MTU PERFECT KWENYE MAHUSIANO

Image
Kwenye mahusiano hakuna mtu perfect,,,,,wote bado tunatumia learner driving license,,,,,,kwa maana ya kwamba wote bado tunaendelea kujifunza,,,,,,kukosea na kutoa mafunzo na kuhakikisha ndoa na mahusiano yetu yanakuwa na afya na kuendelea kudumu zaidi na zaidi.

MWIZI HAPENDI VYA KWAKE ANATAMANI VYA WENZAKE

Image
Kuna mtu anaonekana anakupenda sana kwasababu kila wakati anakumiss,,,,tena yupo tayari achomwe na miiba kuvizia ulipo,,,,,lakini ukweli ni kwamba siku utakayotoka kwa mumeo umfuate umwambie sasa nimekuja kuishi na wewe moja kwa moja ili asichomwe na miiba tena,,,atatoka mbio kama usain bolt,,,,kwasababu siku zote mwizi hapendi vya kwake,,,,,anatamani vya wengine,,,,,,huu ni ushauri chukua hatua.

UMUHIMU WA KUONGEA MAMBO YA UKWELI KATIKA MAHUSIANO INASAIDIA KUISHI KWA AMANI NA UAMINIFU

Image
Ukweli utakuweka huru sehemu yoyote ile katika mahusiano yako,,usiseme una hiki au kile halafu mwisho wa siku humiliki chochote kile,,kama utakuwa na tabia hii ni rahisi kupoteza uaminifu katika mahusiano yako,,kumbuka kama hamna neno kuaminiana katika mahusiano yenu basi hata maana mapenzi  itakuwa imepotea katika mahusiano yenu.

USIENDEKEZE HISIA KUKUPA UPOFU WA AKILI

Image
Hata kama unampenda mtu kiasi gani lakini matendo yake hayaendani na vile unavyotaka awe,basi ni bora umwache AENDE,,,,haitakiwi kuvumilia hata mambo yasiyofaa eti kwasababu unampenda sana na huwezi kumuacha,,kama anakushauri mambo yasiyofaa ni bora umwache aende kuliko kuingia katika matatizo ambayo hukutalajia,,,,,Usiendekeze hisia kukupa upofu wa akili yako,,kutofanya maamuzi sahihi ya kumpata mtu sahihi ambaye atasahihisha mapungufu yake,,,,kumbuka unaweza kuongozwa na hisia na ukashindwa kufanya maamuzi yaliyo sahihi  lakini endapo utaongozwa na maamuzi sahihi basi hisia sahihi zitakuwa katika mapenzi yenu.

MASIKILIZANO HULETA MAELEWANO THABITI KATIKA MAHUSIANO

Image
Masikilizano huleta maelewano thabiti yanayopelekea kudumishwa kwa penzi,,,,mapenzi hayahitaji ujuaji uliopitiliza bali yanahitaji upeo ambao utaruhusu mawazo yenu wote yawapeleke njia ambayo ni sahihi,,,usawa kwenye mapenzi ni sahihi ili isije mmoja akaelemewa na mzigo halafu akakinai mapenzi,,,,,hebu ishini kwa kuongozwa na upendo na kila mmoja aweke tamaa pembeni ili mfikie malengo yenu mapema.