RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE 24
ENDELEA..................... ................. ...24......... Salha alitulia kisha akaniuliza tena, "Mnali, unajua sijakuelewa japo umenieleza kila kitu kinachokuhusu, sasa inawezekana vipi usile chakula cha kawaida alafu badala yake ukapenda nyama mbichi?". Swali lake lilikuwa lina maana kubwa sana kwangu lakini sikuwa na namna zaidi ya kuwa muwazi mbele yake. "Salha! Nisikilize kwa makini tena kwa umakini mkubwa sana" "Ndio nakusikiliza". Niliinuka kisha nikauelekea mlango nikautikisa ili kujua kama umefungwa na kweli ulikuwa umefungwa. "Vipi! Hakuna mtu tofauti na mimi na yule mlinzi" "Kwa nini uishi peke yako" "Basi tu haya tuendeleee" "Sawa Salha! Kama nilivyokuelekeza natafutwa na makundi mawili mpaka sasa tena matatu..hapa ninapokuambia polisi nao wananitafuta, maisha yangu ni ya ajabu sana na yameibuka kutoka hivyo na tatizo ni Uvuvi wangu". "Uvuvi wako? Kivipi tena". Aliuliza "M...