Posts

JE Corona Imetengenezwa Maabara?

Image
Daktari wa Ufaransa aliyeshinda tuzo ya Noble Medicine award mwaka 2008 Luc Montagnier amesema kuwa virusi vya Corona(Covid-19) vilitengenezwa katika maabara huko Wuhan, Uchina. Luc Montagnier ameandika kwenye tovuti ya "daktari wa Pourquoi" kuwa haamini kwamba Covid-19 ilitoka katika soko la wanyama huko Wuhan. "Covid-19 ilitengenezwa kutoka maabara huko Wuhan. Maabara hii imekuwa ya kitaalamu katika kutengeneza virusi vya corona tangu miaka ya 2000." Montagnier amesisitiza kwamba amekuwa akichunguza suala hili vizuri. Montagnier amesema katika taarifa yake kwenye kituo cha CNEWS kuwa, "Virusi hivi havikuanza kwa njia ya kawaida, ni kazi ya kitaalam. Sijui vimetengenezwa kwa nia gani.". Daktari huyo mtaalamu ameendelea kufafanua na kusema kuwa kuna uwezekano ya kwamba virusi vya Corona vina chembechembe ya virusi vya UKIMWI ndani yake. "Hii inaweza kuwa ni njia ya kupata chanjo dhidi ya virusi vya UKIMWI" alisema.

Eminem: Kiumbe Ambacho Wana Hiphop Wanaogopa Kuwa na Bifu Nae, Rap God

Image
Ndiye king of freestyles zinazomake sense na hajuna anaepinga, unashauriwa kuwa na dictionary pembeni maana nahisi anajua maneno yote, Ole wako!!Ole wako ujitie wenda wazimu uanzishe bifu na hiki kiumbe Kumdisi eminem ni kama kumuua mbwa wa john wick, eminem na huyu bwana nahisi wana undugu maana wote wanateketeza kwa kalamu. Yanni eminem kitendo cha kukujibu ukimdisi ni kama anakuchimia kaburi la career yako ujizike mwenyewe. Huwezi kumdisi mtu ambaye tayari anajidiss, waliocheki 8 mile ya eminem nadhani mshanipata Kina jarule wallijaribu wakateketea mazima, kina machine gun kelly nao wakunga tela, nick canon nahisi kaanza kutumia madawa maana sijui hata kapata hii confidence wapi. Japo kina tupaccama notorious big walikuwepo vizuri, ila sidhani kama wamefika hata nusu ya eminem ila tatizo tu labda ni mzungu ndio mana wengi hawamp heshima anayostahili

22 Wapona Ugonjwa wa Corona Uganda

Image
Wizara ya Afya Uganda imesema wagonjwa wengine wawili wa corona wamepona na kufanya idadi ya waliopona kufikia 22 nchini humo, Uganda ina visa 55 ambapo kwa sasa wagonjwa 33 wanaendelea na matibabu, 22 wamepona na hakuna kifo kilichotokana na corona.

Dereva Boda Boda Mwenye Virusi vya Corona Akamatwa Akisafirisha Jeneza Feki

Image
Polisi nchini Kenya imemkamata dereva aliyekuwa na virusi vya corona pamoja na abiria watatu waliojidai kuwa waombolezaji wanaoelekea kwa mazishi. Watatu hao waliokuwa wamesafiri zaidi ya kilomita 370 kutoka kutoka Nairobi wakiwa na jeneza bila maiti walikamatwa katika jimbo la Homa Bay magharibi mwa Kenya. Tukio hilo la kushangaza liliangaziwa na Waziri wa Afya wa Kenya Bw. Mutahi Kagwe ambaye pia alithibitisha kuwa kundi hilo lilifanikiwa kuhadaa polisi kwa kutumia jeneza tupu na kupita vizuizi kadhaa njiani. Aliongeza kuwa dereva huyo ametengwa na abiria wake kuwekwa karantini. Karibu wiki mbili zilizopita serikali ya Kenya ilitangaza hatua kali za kudhibiti watu kuingia na kutoka katika mji mkuu wa Nairobi pamoja na majimbo menginine matatu ambayo yanasadikiwa kuwa na viwango vya juu vya maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19. Waziri wa Afya alisema serikali inachunguza madai kwamba baadhi ya watu wanatoa hongo kwa polisi wanaolsimamia vizuizi vya barabarani. Malori yanayoenda safari za...

Maelfu Wapona Corona kwa Siku Moja Italia

Image
Na habari njema kutoka Italia zinaarifu kuwa nchi hiyo kwa mara ya kwanza imerekodi idadi kubwa ya watu waliopona virusi vya corona katika kipindi cha masaa ishirini na mane.  Kulingana na mkuu wa idara ya kukabiliana na majanga Angelo Borelli, watu 2,563 wamethibitishwa kupona virusi vya corona katika kipindi cha siku moja. Idadi ya walioambukizwa virusi hivyo pia imepungua pakubwa. Kati ya Alhamis na Ijumaa ni visa 3,786 vya maambukizi vilivyoripotiwa.  Kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Afya mjini Roma, karibu wahudumu wa afya 17,000 wameambukizwa virusi hivyo sasa huku idadi kubwa wakiambukizwa wanapokuwa kazini.

Fahamu Tabia za Wanawake Wanaopenda Sana Pesa

Image
1. Huwa na tamaa ya mambo yasiyo ya lazima. Wanawake wengi wapendao pesa huwa na tamaa ya mambo yasiyo ya lazima, mambo ambayo hayagusi maisha moja kwa moja. Hata nilipokuwa chuo wanawake wengi waliokuwa wanapenda pesa Sana walikuwa na tamaa za kusikitisha ambazo zilipofusha fahamu zao. Unakuta mwanamke anaomba laki tano kwaajili tuu ya kununua Simu nyingine kubwa wakati akiwa bado na simu mpya. Katika maisha ni bora uingie jehanam kuliko kukutana na mwanamke mpenda pesa kwani utateseka Sana kwa ajili yake na bado hata ona msaada wako. Sio rahisi kujenga familia bora na mwanamke mpenda pesa. 2. Wengi hutoka familia masikini. Wanawake wengi Kama sio wote ambao hupenda pesa kuliko utu wao hutoka familia kame Sana. Ukame wa kiuchumi mpaka kiakili. Wengi wao huweza kutoa hata rushwa ya ngono ili tuu wapate pesa wasijue miili yao inathamani zaidi ya zile karatasi. Mtu ni masikini unandoto za kuwa na mwanaume mwenye pesa nani alikuambia wenye pesa wanataka masikini. Umasikini wako usikufanye...

Marekani yatangaza vifo 4,491 vya Covid 19 ndani ya saa 24

Image
Idadi ya vifo nchini Marekani yongezeka na kufikia 4,491 ndani ya saa 24 kwa mujibu wa takwimu za chuo kikuu cha John Hopkins. Hata hivyo, vifo hivyo vinaweza kuwa vinajumuisha watu waliofariki wakihusishwa kuwa na COVID19 na Madaktari kujiridhisha hivyo lakini bila mgonjwa kupimwa maabara. Aidha Marekani ilikuwa ikitangaza idadi ya vifo vya wagonjwa waliopimwa maabara na kuthibitika kuwa na Ugonjwa huu. Mpaka kufikia jana Chuo hicho kimetoa takwimu za kidunia kuhusiana na mwenendo wa ugonjwa wa COVID 19 vifo vikiwa ni 137,078 huku jumla ya visa vilivyothibitishwa kufikia takribani milioni mbili.