MPENZI/MKE BORA HUWA NA SIFA HIZI

Wapenzi wengi ambao wanapendana leo mapenzi yao hayadumu kiasi cha kubatizwa jina la utamu wa BIG BOM,, yote hii inatokana na ukweli kwamba elimu ya mapenzi ambayo ni kama chakula kwa binadamu haitolewi kwa ufasaha kuimarisha upendo na mapenzi baina ya Wapendanao….

Pia katika Jamii zetu imekuwepo dhana potofu kwamba kumfundisha mtoto mapenzi ni kumharibu,,,,,jambo ambalo si kweli ila inategemea mtoto huyo anafundishwa nini na ni kwa wakati gani??? Lakini cha kushangaza zaidi hata watu wazima ambao ni wadau wa mapenzi hawayajui, matokeo yake wanajiingiza kwenye uhusiano wakiwa bumbumbu na hivyo wanaambulia kuteswa na changamoto zinazowakabili.

Leo tutajifunza kwa undani sifa za mpenzi bora(wife material) ili tuweze kuwatambua wapenzi wetu kabla ya kuwapa mioyo(kujiingiza kwenye bahari ya malavidavi) na utu wetu.

Sifa hizo ni hizi zifuatazo;
1. Anajitoa kwa ajili yako

Mpenzi bora ni yule ambaye hatangoja kujua nini unahitaji yaani hana sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo atoe msaada.

2. Ni yule atakayejua wakati gani huna furaha au una furaha na atakuwa na wewe kwa hali zote mbili .

3. Ni yule atayekuwa tayari kukusikiliza kwa kile utakachosema, hatojali umeongea baya au zuri

4. Atakuwa na wewe wakati wa shida na raha. Hatakuwa mtu wa kuvizia vizia na kujisogeza wakati ukiwa na raha.

5. Mpenzi wa kweli atakuheshimu na hatopenda kuwa kikwazo cha maisha yako, atakulinda daima.

6. Atakupenda kwa moyo wake wote na wala si kwa ajili ya shinikizo fulani (pesa au mali)

7. Mpenzi wa kweli ni yule atakayeonyesha kuthamini nafasi yako kama rafiki au mpenzi mbele ya wengine, hafichi hisia zake mbele za watu, atakutetea na kukufanya wa kwanza.

8. Kwenye ukweli mpenzi mzuri atasema bila kukuficha na atapenda kukuonyesha mifano ya namna ya kuwa mkweli na mwaminifu.

9. Mpenzi wa kweli ni yule anayejiamini, asiyeyumba katika maamuzi hata kama atalazimika kufanya maamuzi magumu .

10. Atakuwa tayari kuvumilia, hatakuwa mwepesi wa hasira wala kutumia lugha chafu na ubabe.

Comments

Popular posts from this blog

SMS 47 ZA MAPENZI ZITAKAZO MNYEGEZA** MPENZI WAKO

KWANINI WADADA WENGI WAREMBO NA WANAOJIONA WAREMBO HUCHELEWA KUOLEWA,HUKOSEA KUOLEWA AU KUTOOLEWA KABISA?SOMA HAPA

HATUA ZA KUCHEZEA KIHARAGE NA KISIMI