SEX MACHINE - SEHEMU YA 03
SEHEMU YA 03
"Ni kweli Chriss nina makosa lakini siyo kwa hukumu hiyo, inamaana umeshindwa hata kujizuia my love...? No, i don't belive that Chriss umenikosea sana." Alilalamika sana Salome hakutegemea kutokea kwa jambo hilo kiwepesi namna hiyo. Chriss alimuangalia msichana huyo kwa kina na kisha akakifungua kinywa chake tena.
"Naomba unisikilize kwa umakini mkubwa we binti, ulishindwa kulifanya hili liwe siri baina yangu mimi na wewe ukaamua kumwambia kila kitu Maida. Ukitegemea kwa mtoto wa kike kama yeye angekwenda wapi kumalizia haja zake na ilhali mnajua mazingira mnayoishi? eenh...!"
"hata kama siyo kwa namna hiyo Chriss, mimi siyo wa kuchangia penzi na Maida." Salome alimkatisha Chriss na kusema maneno hayo kwa sauti ya juu sana tena alikuwa akiongea huku machozi yakianza kujichora machoni mwake.
"Hujui ulisemalo na laiti ungejua, ungekwisha kuufunga mdomo wako!" Alisema namna hiyo Chriss na kumfanya Salome kuganda kwa muda mithili ya mtu aliyepigwa na shoti ya umeme.
"Kivipi?" akahoji.
"Msinifanye mimi ni mashine yenu ya ngono. Na kuanzia sasa ninavyoongea, naomba usinikaribie na usahau kabisa kama ulikuwa na mimi kimapenzi...!"
"eenh...?" Salome aling'aka, macho yalimtoka kama kapatwa na taarifa mbaya, ulikuwa ni mshtuko mkubwa sana na wala hakuutarajia kabisa.
"Chriss please he...he...hebu acha utani!" Akasema sasa akiwa makini kabisa kumsikiliza kijana huyo kile ambacho atajibu.
"Nimesema hivi, nisikilize kwa makini tafadhali, sihitaji mahusiano na wewe tena na si wewe tu hata huyo Maida. naona mnanichezea share, nimefunga mahusiano na ninyi na naomba uondoke hapa mbele yangu."
"Chriss are you...!"
"I said i do not want, tokaa...! you are so stupid, you can not make me Your sex machine!" Alifoka Chriss akionesha dhahiri hakuhitaji tena majadiliano juu ya suala hilo. Salome aliangua kilio kizito sana, machozi yalimtiririka mashavuni mwake kama mifererji ya maji. Yalikuwa ni maamuzi magumu sana alitamani kumuomba msamaha mwanaume huyo lakini tayari alishachelewa, Chriss alikwisha kuondoka eneo hilo na kumuacha mwenyewe. Iswear Maida utalipa hili, sikuachi hata kidogo lazima uniambie ulichompa huyu mwanaume. Chriss hawezi kuwa hivi lazima atakuwa amefanya hivi ili aendelee na wewe. Aliwaza Salome na kujikuta akifika mbali zaidi. Hakujua nini sababu hasa ya mwanaume huyo kuwa hivyo bali fikra zake zote alizipeleka kwa Maida.
Chriss alipotoka pale bustanini, moja kwa moja alielekea ndani. alipofika sebuleni alimkuta shangazi yake akiwa anacheza na Mery. Chriss alimtazama sana shangazi huyo jinsi alivyo na upendo mkubwa kwa watoto japo yeye hakubahatika kuwa na mtoto hata hivyo hakuwa akiwachukia watoto. Hata Mery hakuwa mwanae wa kumzaa alikuwa ni mtoto wa mdogo wake wa kike ambaye pia alipoteza maisha yeye na mumewe kwa ajali kama walivyokufa wazazi wa Chriss na shangazi huyo kuamua kumlea mtoto huyo kama alivyofanyiwa Chriss. Itakuwaje kama nitamuuzi shangazi, kwanini nionekane mkosaji kisa mapenzi. Aliwaza Chriss akiwa hapo hapo kwenye kona iliyotenganisha chumba chake na sebule. Salome nakuchukia, umenikosea sana kwa hili. Alizidi kujisononesha kijana huyo. Donge zito likamkaa kooni na kufuatiwa na kilio cha kwikwi. Ni kweli alikuwa akimpenda sana binti huyo lakini kwa jambo hilo alikosa kabisa jinsi. alikimbilia chumbani kwake huku akiuzuia mdomo wake kwa kiganja cha mkono ili asiweze kutoa sauti. aliubamiza mlango kwa nguvu hadi anti huyo akasikia hali iliyopelekea kusitisha kidogo kwa muda mchezo aliokuwa akiucheza na Mery sebuleni hapo. alijitupa kitandani Chriss na kukiruhusu kilio hicho kilichoamsha hisia kubwa za maumivu.
____________
SEHEMU MOJA KATIKATI YA MJI WA MOROGORO.
"Bosi nafikiri ni muda muafaka wa kikao kama alivyoagiza Mkuu." Mwanamama mmoja mrembo, mrefu kwenda juu, asiye mwembamba wala mnene, mwenye miguu minene na pua ya kisomali; nyembamba ndefu kiasi na nywele nyeusi tii! Akaongezewa na weupe wa asili akiwa katika vazi ghali kabisa. Alikuwa amesimama mbele ya meza kubwa ya mninga iliyokaliwa na kompyuta mpakato akimfikishia ujumbe huo mtu huyo aliyemuita bosi huku akilitua faili fulani mezani hapo. Ilikuwa ni ofisi kubwa na nzuri iliyo ndani ya kampuni kubwa sana inayojihusisha na masuala ya utalii. ambayo ilikuwa imebeba jina la SAFARI COMPANY (S.C). Ni kampuni kubwa ambayo shughuli zake tambulishi ni upokeaji na usafirishaji watalii wa ndani na wa nje kutokea hapo Morogoro mjini hadi zilipo mbuga za wanyama na vivutio mbalimbali vinavyopatikana ndani ya mkoa huo uliozunguukwa na safu ya milima ya URUGURU.
"Suzane?" Aliita mtu huyo anayefahamika kwa jina la Bosi kisha akasema;
"Najua unajua cha kujibu, sitegemei uniangushe?"
"Najua Bosi toa shaka kabisa kuhusu hilo lakini hata wewe si unaweza kujibu baadhi ya mambo au ni mimi tu?" Alijibu Suzane mtu wa karibu na ni kama alikuwa ni katibu mukhutasi wa Bosi huyo na kuuliza swali.
"Tunategemeana." Akaongea Bosi, Suzane akajibu sawa na kutoka ofisini humo akimuacha Bosi akijiandaa.
Ulikuwa ni ukumbi mkubwa sana uliopo sakafu ya juu ya jengo hilo kubwa. Kulikuwa na meza kubwa ya thamani sana yenye umbo la mstatili iliyokuwa imezunguukwa na watu saba waliotakata. Fedha ilijitangaza yenyewe mbele ya watu hao hakukuonekana hata mmoja aliyechoka mahala hapo kila mmoja alikuwa na hadhi ya kuitwa Bosi. Kati ya viti hivyo saba vilivyopangwa kufuatana na meza hiyo ya mstatili yaani vitatu kushoto na vitatu kulia huku kimoja kikiwa kimekaa kichwani mwa meza hiyo, sita vilikuwa vimebeba watu walionyuka suti za rangi nyeusi safi hata hivyo huyu wa saba pekee ndiye aliyekuwa tofauti, yeye alikuwa ndani ya suti ya kijivu iliyomkaa vizuri mwilini mwake.
"Mhg, mhg!" Yule bwana aliyevaa suti ya rangi ya kijivu alijikohoza kidogo kuliweka koo lake sawa kabla ya kukifungua kikao hicho rasmi.
"Habari za muda huu ndugu zangu? Natumai wote mko hapa kujua nini kinachokwenda kuzungumzwa. Mimi sina mengi sana ya kuzungumza ila kila kitu atatueleza Mkuu." Alipokwisha kusema hayo mtu huyo ambaye alifahamika kwa jina la Bosi kama mimi na wewe tunavyomfahamu, sauti ya mkoromo ikasikika kutoka kwenye spika maalumu zilizofungwa kitaalamu sana ndani ya ukumbi huo. Mara zikaanza kusikika sauti za mhemo kisha sauti ya mtu anayezungumza ikarindima mahali hapo.
"Tuko katika hali mbaya sana kiuchumi na ninyi mnajua, kampuni inaangamia. Gharama zinazotumika ni kubwa kuliko faida inayoingia... Joesan...?" Sauti hiyo nzito iliunguruma kwa maelezo machache yasiyo na salamu mwisho ikalitaja jina la Joesan.
"Naam Mkuu...!" yule mtu anayefahamika kwa jina la Bosi akaitika kwa sauti ya chini kidogo lakini iliyoweza kupenya vema kwenye masikio ya Mkuu huyo.
"Kampuni ikifa jua umemruhusu Iziraili andoke na uhai wako, utakufa kweli Joesan uzembe ni wako. Tunashindwa kupokea oda kubwa na za pesa nyingi za kunawirisha utajiri wetu sababu yako. SEX MACHINE alikufa kwa uzembe wako." Ilisema kwa nguvu sana sauti hiyo, mtu huyo alionekana kuwa na ghadhabu kubwa huko aliko. Joesan alikuwa kimya akiisikiliza sauti hiyo kwa umakini mkubwa. Hofu ikauvaa moyo wake, afanye nini hapo. alihema kwa nguvu nyingi baada ya sauti hiyo kuweka tuo.
"Najua Mkuu...!" Akaificha hofu mbele ya watu wanaomtazama na walio chini yake kiutendaji na kujikakamua kusema.
"nini utetezi wako sasa, unaliambia nini jopo la watu wanaokutegemea hapo ulipo?" Iliuliza sauti hiyo. Joesan alitulia kwa muda bila kutoa utetezi wowote. Ukumbi ule ulikuwa kimya sana. Wote walikuwa wakimtazama yeye. Joesan aliona kama jumba bovu linamuangukia na hakuna kizuizi chochote cha kuweza kulizuia. Afanye nini sasa? Hilo likabaki kuwa swali gumu ubongoni mwake. Alichokifanya kwa wakati huo ni kuyainua macho yake na kumtazama Suzane yeye alishachanganyikiwa tayari. Hakujua nini cha kulieleza jopo hilo, alitaitika haswa. Suzane aliiona hali hiyo akajua kuwa bosi wake yupo katika hali mbaya mno, akawatazama wote waliopo mbele yake kisha kushotoni kwake, akashusha pumzi ndefu iliyowafanya watu wote pale kugeuka na kumtazama. Mtoto wa kike huyo akabeba ujasiri na kusema.
"Tupe siku tatu mkuu naa...!" Akakwama na kumgeukia bosi wake aliyepatwa na mshtuko wa waziwazi kabisa baada ya yeye kuomba siku tatu tu kama ahadi ya utekelezaji wa jambo hilo au upatikanaji wa majibu kuhusiana na jambo hilo kisha akamalizia kwa kusema;
"...nadhani tutalishughulikia hilo na kabla ya siku ya nne Sex machine atakuwa mbele yako." Akaweka tuo. Miguno ikasikika mule ndani kisha ukimya tena. Sauti ya Mkuu ikarindima tena kutokea kwenye zile spika zilizofungwa kila kona ya ukumbi ule.
"Mmejifunga wenyewe 'that is bracket,' mkienda kinyume mnajua nini kitawakuta. Nimefunga mjadala na ninyi sasa nageukia kwako Mahmood...! Vipi Mahmood, hujaniambia chochote kuhusu mamilioni ya pesa yaliyopotea mikononi mwako kwa uzembe tu?" Watu wote sita pale mezani wakageuka na kumtazama mtu huyo mwenye asili ya kiarabu. Mahmood hakujibu kitu alibaki kimya tu.
"Una chochote cha kuniambia sasa?" Ilikazia hiyo sauti ya mkuu, Mahmood alishtuka baada ya sauti hiyo kumgutusha.
"Mkuu nimejitahidi sana lakini sijafanikiwa kuwapata wale wavamizi walioondoka na ile pesa...!"
"kwa hiyo?" Akapokea swali jingine.
"Nisamehe mkuu ni makosa yangu." Akajitetea Mahmood.
"Ha ha ha haaa!" Cheko zito la fedha likatikisa ukumbi huo, Mahmood akashtuka na wote mule ndani wakajua nini kitakachokwenda kumkuta Mahmood muda mchache ujao. Kicheko cha mtu huyo wanaemuita mkuu, siku zote walikitafsiri ni kama hasira zake na ndivyo hivyo. Mara nyingi linapoibuka jambo la kumchukiza yeye hucheka tu lakini madhara yake huwa ni makubwa. Hivyo walijua dhahiri nini kinachokwenda kujiri mahali hapo.
"Mahmood, kirahisi rahisi tu kama unamuomba mkeo unyumba. Blood foolish!" Ikasema sauti hiyo na mara hiyohiyo ghafla, sauti ndogo ya maumivu ikasikika. watu hao walipogeuka na kumuangalia Mahmood, walimuona akiwa ameegamia kiti chake akiwa na alama ya nyota kwenye paji la uso. Halikuwa jambo la kushangaza na hali hiyo walishaizoea.
"Milioni mia moja na hamsini halafu unasema nikusamehe. Nani kasema kuwa ninasamehe kipumbavu kwenye pesa. Amenitia hasara sana huyo shoga, mzigo amekosa na pesa zimekwenda mbaya zaidi amesababisha vifo vya vijana wangu wawili. Hivi mnajua hii kazi ni ya kuchambua mchicha eenh! Inabidi muwe ngangari kwenye kampuni hii na sitawavumilia watu wazembe tena. Mtakufa." Ikamaliza sauti hiyo kwa kutoa kalipio baya sana kwa washirika wote wa humo ndani kisha mkoromo wa spika ukafuatia na kufuatiwa na ukimya kuashiria kuwa mkuu huyo alishakata mawasiliano. Minong'ono midogo midogo ikaibuka mahali hapo huku vijana maalumu wakihangaika na kuutoa mwili wa Mahmood eneo hilo.
Comments
Post a Comment