SEX MACHINE - SEHEMU YA 05
SEHEMU YA 05
Baada ya muda kidogo alinyanyuka na kuwasha gari yake hiyo, ila kabla ya kuliondoa, aliwasha redio na kuutafuta wimbo wa mwanamama Celine Dion. wimbo unaokwenda kwa jina la 'That the way It is'. ambao aliamini kidogo unaweza kuyapeperusha mawazo yake kwa muda huo.
"When you want it the most,
there's no easy way out,
when your heart's left in doubt" ndivyo alivyokuwa akiufuatisha wimbo huo huku akitingisha kichwa kidogo kidogo. Wimbo huo ulimfanya ayasahau mawazo lukuki yaliyokuwa kichwani mwake.
"When you question me for a simple answer,
i don't know what to say,
no but it's plain to see,
if we stick together. Your gonna find the way yeah." Kwakweli wimbo huo ulimpeleka mbali kihisia, ulimfariji kwa kiasi fulani hadi nyumbani kwake akapaona karibu sana. alifika nyumbani kwake bila matarajio. Alikibonyeza kitufe fulani kwenye rimoti na lango kubwa la jengo hilo likafunguka. lilikuwa ni jengo kubwa na la thamani kweli ambalo limejengwa kisasa kabisa.
___________
Joesan ndiye aliyekuwa mjomba wa Chriss na alikuwa ni mtu mwenye utajiri mkubwa sana mjini hapo. Alikuwa akimiliki majumba kadhaa mjini na biashara kubwa mno. Hakuna asiyemjua Joesan, alifahamika kila kona na alikuwa ni mtu mwenye kumsadia kila anayehitaji msaada. Hilo likapelekea jina lake kukuwa siku hadi siku. Alimiliki mwili mkubwa uliobeba kitambi cha wastani na kifua kipana. Huyu ndiye hasa aliyeyafikisha maisha ya Chriss hadi kufikia hapo alipo na alikuwa akimpenda kijana huyo kupita kiasi. Yeye ndiye aliyebeba historia nzima ya maisha ya kijana huyo. Aliufunga mlango wa gari vizuri na kupiga hatua ndogo ndogo kuelekea ndani ya jumba hilo na lenye thamani ya juu mno waswahili wenyewe huita Villa. Aliingia ndani na kumkuta mkewe akiwa sebuleni na Mery wakiwa wako katika harakati ya kuangalia runinga wakifuatilia filamu ya kibongo. Mery aliruka kutoka mahali alipokaa na kumrukia Joesan.
"Ankoo huyoo! Shikamoo Anko?" Alisalimia Mery akiwa yupo mikononi mwa anko wake akining'inia baada ya anko wake huyo kumnyakuwa na kumbeba.
"Marahaba anko hujambo?"
"Sijambo anko,"
"Ok, vizuri, haya endelea kuangalia muvi sawa anko?" Joesan alimwambia mtoto huyo huku akimshusha binti huyo mdogo. Akamgeukia mkewe.
"Vipi mmeshinda salama?"
"Ndiyo ni salama tu mume wangu sijui wewe huko kazini?" Akarudisha salamu anti martha.
"Kazini si kubaya sana ila bado hakujatulia, vipi mbona mko wenyewe wengine wako wapi namaanisha Chriss maana hao mabinti si sana kukaa hapa muda huu?" Akauliza Joesan baada ya kujuzana hali na mkewe.
"Tokea alivyotoka bustanini kufanya usafi wa bustani yake, ameishia kujifungia tu huko chumbani kwake sasa sijajua ni kipi kilichomsibu au labda atakuwa amelala kutokana na uchovu tu wa kawaida."
"Siyo Chriss!" Alidakia Joesan.
"Sasa anafanyaje maana ni muda sana eti, tangu kuondoka hapa." Alisema tena anti Martha.
"Hebu ngoja nikamuangalie chumbani kwake," akaongea Joesan na kuelekea kilipo chumba cha Chriss lakini kabla hajakigusa kitasa cha mlango, akasikia kelele za majibizano kutokea upande wa jikoni. Zilikuwa ni kelele haswa ambazo hakika kwa mtu mzima kama yeye zilimshangaza sana hata hivyo hakutaka zimpite ilibidi kujipa utulivu kuweza kuyasikiliza malumbano hayo.
"Mh! Kuna nini tena mbona kelele hivi?" Alijiuliza Joesan akiwa anajisogeza kwenye ukuta karibu na mlango wa jukoni ili kusikiliza vizuri hata hivyo aliona si sawa kufutilia majibizano hayo ya watoto wa kile ila kuna kitu kilimvutia sana katika majibizano hayo.
"Hebu ngoja," akajishauri na kuelekeza nguvu zake za kusikiliza zinapotokea sauti hizo.
"Nimekwambiaje, kuanzia sasa basi kama hujui ndiyo ujue upo hapo bibi wewe. Chriss yuko hapa tenaa...! Nilikuwa sijajua raha unazozipata kutoka kwa mwanaume yule. Sasa kwa taarifa yako ameshaukubali mziki wangu. Halafu sijakuambia eenh! Anasema hivi, hawezi kuendelea na wewe aliyekukuta umesha haribiwa njia, mtoto kanikuta na mkanda wangu ndoo ikiwa bado haijafunguliwa upo hapo?" Yalikuwa ni maneno ya Maida akimtambia Salome. Yalikuwa ni maneno yenye kuudhi sana, kama ni vijembe basi hivyo vilikuwa ni vijembe haswa. Salome alikuwa kafura kwa hasira vibaya sana hapo sasa aliamini kweli hana chake kwa Chriss.
"Sijui hata nikufanye nini wewe malaya nakuchukia sana Maida, sikutegemea kama ungekuja kunigeuka namna hii Hivi...!"
"Hee!" Maida alimkatisha Salome akisema;
"Mimi na wewe malaya nani? Nakuuliza hivi, mimi na wewe malaya ni nani? Malaya ni wewe uliyeliwa mtaani. mimi Chriss amenikuta mzima na bikira yangu, wewe je? Na kwa taarifa yako bibi wewe, Chriss akiwa na hamu tu hapa," Maida akakipigapiga kifua chake kuashiria kuwa Chriss ndipo anapolala pale anapokuwa na hamu ya kufanya mapenzi. Akaendelea kutema shombo mtoto huyo.
"...na simuachi mwanaume yule hata ukaroge. Mwanaume dakika arobaini na zaidi hatoki kifuani utadhani katokea milimani au kala miti shamba!" Alikuwa akitamba kweli kwa maneno mtoto huyo. Salome hakutia neno hata moja na si kama hakupenda kusema bali hakujua ni neno gani linafaa kumwambia Maida hadi limuingie. kwa hapo ni wazi Salome alikiri kuwa amepatikana. Ni kweli Maida ana haki ya kujitapa maana tayari Chriss alishauonja utamu wake. Tangu siku hiyo ya kwanza tangu alipomruhusu mwanaume huyo auchungulie mwili wake na kula vile vilivyofichwa, ambapo ilikuwa ni kama wiki mbili zilizopita. Salome hakuonekana tena kumfuata Maida nyakati za usiku na kwenda kumtambia hali hiyo ikajenga maswali mengi sana kichwani mwa msichana huyo.
"Salome amekuwa kimya sana siku hizi, simuoni tena akija kunipa sifa za Chriss sijui ni kwa sababu gani?" Ndivyo alivyokuwa akijiuliza siku moja Maida.
"Au hakuna mitindo mipya siku hizi au amekuwa na nini kiasi cha kumfanya akose sifa ya kuja kunisifia?" Alijiuliza tena namna hiyo na kuachia tabasamu pana. Si kwamba alisema hivyo kwa kujua la hasha! Ila kuna jambo alihisi. Huwenda labda mwenzake hapati nafasi kwa sababu muda wote yeye ndiyo yuko na mwanaume huyo. Salome aliuvunja kabisa utaratibu wake wa kwenda chumbani kwa Maida kila anapotoka kushuhulika na mwanaume huyo. Hali hii ndiyo iliyompa Maida nafasi kubwa ya kujiona yeye ni bora kuliko mwenzake. Kile kitendo cha kuja chumbani kwa Maida na kujitupa kitandani kujifanya amechoka kwa kusulubishwa na mwanaume huyo, ziliyeyuka kama Ubuge kwenye upepo wa kisulisuli. Maida hakutaka kujiaminisha moja kwa moja kisa tu kutomuona Salome chumbani kwake bali aliamua kwenda kumuuliza Chriss kabisa juu ya jambo hilo. Ndipo Chriss alipomwambia kwamba havutiwi na Salome hata kidogo kwanza alimkuta mweupe hana bikira hivyo mara nyingi amekuwa akimtolea mbavuni kila anapohitaji kukutana nae kimwili. Maida kwa kiburi akamfuata Salome usiku huo huo na kwenda kumuuliza sababu za kutomtambia usiku kila akitoka kufanya mapenzi na ni nini ilikuwa ni sababu ya hayo au alikuwa tayari ameshakua na kujitambua kuwa ayafanyayo ni mambo ya kitoto? Salome naye bila kufikiria akamueleza kila kitu akidhani anatengeneza au Maida angekwenda kumpigia kifua kumbe ndiyo alikuwa akizidi kumpa kichwa mwanadada huyo. Hapo kibao kikamgeukia. Maida akamwambia Salome waziwazi kuwa asijisumbue kwani kwa muda huo hakuwa na jipya tena mbele ya Chriss. Ameshamkamata na asitegemee kupata penzi la mwanaume huyo mwenye utamu wa aina yake, kisha akatoka chumbani humo na kumuacha mwenzake akiwa na maswali mengi ya kujiuliza. Na jambo hilo ndilo lililompa Salome msukumo mkubwa wa kumfuata Chriss kule bustanini alikokuwa akifanya usafi na kumuuliza. Malumbano yote hayo yaliyokuwa yakiendelea, yalikuwa yakisikiwa na kuonwa moja kwa moja na Joesan aliyekuwa bado amejibanza kwenye pembe ya mlango wa kuingia jikoni. Hakutia neno lolote alikaa mahali hapo akifuatilia majibizano hayo mwanzo mwisho hadi pale alipoona mabinti hao wanataka kupigana ndipo akajikohoza na kuwafanya washtuke na kila mmoja kujifanya kama siyo yeye aliyekuwa akijibizana na mwenzake mahali hapo. Joesan alikunja sura na kuwatazama mabinti wale kwa muda na kuwasontea kidole.
"Hili siyo danguro, sitaki hizo kelele zenu na nikizisikia tena mtanieleza vizuri. Sitaki kusikia huo ujinga wenu tena sawa?" Joesan aliwagombeza sana mabinti wale hadi wakaogopa na kuwa wadogo. Haikuwahi kutokea hata siku moja kwa bosi wao kuwa mkali kiasi hicho. Joesan aliondoka hapo akiwa ameghadhibika sana alielekea chumbani kwake akiwa na lengo la kwenda kujipumzisha. Alijitupa kitandani na kujilaza chali, alitulia kitandani hapo kwa muda kidogo akitafakari hili na lile, lile na hili hata lile wazo la kwenda chumbani kwa Chriss likiyeyuka kabisa akilini mwake.
"Hawa mabinti siwaelewi kabisa, kwanini hawaiheshimu nyumba hii, kwanini wanaifanya nyumba hii ni sehemu ya majibizano ya kijinga jinga, wangejua nilivyo vurugwa wala wasingeleta uwenda wazimu wao. Hii hali ni mpya sana na haijawahi kutokea." Aliwaza Joesan akiwa kitandani hapo amejilaza kiwiliwili lakini upande wa miguu wote ukiwa nje ya kitanda.
"Chriss amefikia hatua hii ya kugombaniwa (akacheka kidogo). Ameitoa wapi hii tabia ya kutembea na wanawake wawili kwa wakati mmoja tena wakiwa ndani ya nyumba moja. Hayajui mapenzi huyu kijana, hajui mapenzi yanauwa, yameuwa, yalishauwa na yanaendelea kuuwa hapa duniani? Hajui kuwa mapenzi ni hatari sana? Hapana lazima nimuweke chini niseme nae hii ni hatari sana na inaweza kuleta balaa." Joesan alizidi kumfikiria kijana wake na kwa muda huo alisahau kabisa kwenda kumgongea kijana huyo chumbani kwake ili kuweza kujua nini sababu za kujifungia hadi majira hayo ya jioni ilhali si kawaida yake.
"Amekuwa hodari sana huyu kijana, dakika arobaini na tano mtu bado yuko maungoni mwa mtu," aliongea Joesan baada ya kukumbuka maneno ya Maida kuwa hawezi kumuacha Chriss kwasababu anajua kumfikisha safari zake ipasavyo na huwa anatumia muda mrefu sana awapo kifuani kwake.
"Chriss!" aliita Joesan kwa sauti ya chini na kukumbuka kauli ya mkuu wake.
"Mmejifungia wenyewe, 'that is bracket"
"Huwenda Chriss... Ooh! no, siwezi kufanya hivi. Kwanini sasa nawaza ujinga namna hii, hapana, hapana, hapanaaaa!" Alipiga kelele kubwa sana, hakutaka wazo la kumfanya Chriss kuwa Sex Machine limkae kichwani mwake. Lilikuwa ni wazo baya sana, kwnini wazo hilo lilimjia Joesan, huwenda labda ni sababu ya kuchanganyikiwa na hakujua ni wapi atampata huyo Sex Machine. Lakini pamoja na hayo, wazo hilo alipingana nalo kwa kiasi kikubwa sana. Alipinga na hakutaka limzoee kabisa. Chumba hicho akakiona kama kinamshangaa kwa wazo la kipumbavu lililotaka kumjia. Hakupenda kuwepo hapo tena. Kila alichokitazama chumbani mule alikionea haya. Alinyanyuka Joesan na kutoka mule ndani ikiwa sasa imetimu saa 05:30 za jioni. Alikwenda hadi bustanini na kujituliza pembezoni kabisa mwa bwawa la kuogelea. Nina muda mrefu sana sijafika mahala hapa, kazi hizi zinanifanya kuwa ubize mkubwa kila wakati. Akawaza Joesan akiwa hapo bustanini akiyashangaa mandhari yake. Leo imenilazimu kufika hapa bila kutarajia mawazo yamenizidi sana sielewi nifanye nini mimi. Aliwaza tena bwana huyo akiwa sasa amesimama ndani ya ile bustani ya maua.
Comments
Post a Comment