SEX MACHINE - SEHEMU YA 06

SEHEMU YA 06 

Alinyanyuka Joesan na kutoka mule ndani ikiwa sasa imetimu saa 05:30 za jioni. Alikwenda hadi bustanini na kujituliza pembezoni kabisa mwa bwawa la kuogelea. Nina muda mrefu sana sijafika mahala hapa, kazi hizi zinanifanya kuwa ubize mkubwa kila wakati. Akawaza Joesan akiwa hapo bustanini akiyashangaa mandhari yake. Leo imenilazimu kufika hapa bila kutarajia mawazo yamenizidi sana sielewi nifanye nini mimi. Aliwaza tena bwana huyo akiwa sasa amesimama ndani ya ile bustani ya maua. Baada ya muda akahisi mikono laini ikimkumbatia kutokea nyuma na kukipapasa kifua chake kilichochanika kutokana na mazoezi mazito. 

"Mume wangu leo ni maajabu sana kufika mahali hapa, si kawaida yako maana hata chakula umegoma kula leo, nini kimekupata my dear?" Sauti mwororo ya Martha ikasikika kutokea nyuma ikimuuliza kwa utaratibu mkubwa. 

"Hapana mke wangu ni u-bize tu wa kazi hakuna kitu kingine," akazungumza Joesan. Martha alizunguuka kwa mbele na kumtazama vizuri mumewe huyo na kumuuliza 

"Mbona kama kuna kitu unanificha honey, hata kukataa kula chakula changu leo ni ubize wa kazi?"

"Mmh! Hapana mke wangu, unajua nilipata ofa leo. Rafiki yangu kutoka Marekani alinipigia simu leo wakati nipo kazini, akaniomba tukutane maeneo fulani hivi kwa ajili ya mazungumzo, hivyo nimekula vizuri tu na nimeshiba sana, usijali mke wangu pika chakula kizuri cha usiku na tutakula wote leo." Akasema kwa utulivu Joesan huku akizichezea nywele za mke wake na kuyashikashika mashavu yake laini. Martha alilipuka kwa furaha baada ya mume wake kumwambia jambo hilo. Alikumbuka sana kula pamoja na mumewe ni muda kidogo umepita tangu kuacha kujumuika na mumewe kwenye meza moja ya chakula, mambo yake mengi ya kikazi yalikuwa yakimfanya kula mwenyewe kwa kuchelewa kurudi kwani huwakuta wao walishakula tayari hivyo alikuwa na haki ya kufurahi kwa kuwa chakula cha jioni kinakwenda kuwa cha pekee sana. 

"Waaooh! Nitafurahi sana kula pamoja leo mume wangu, nimekumbuka sana chakula cha pamoja, punguza ubize sweetie jamani unakuwaje hivyo hadi naumiss uwepo wako?" Alizidi kulalama Martha. 

"Ni kazi mke wangu ndiyo inaniweka hivyo lakini hata mimi ninakumbuka sana uwepo wako karibu yangu, kiukweli nakosa tu jinsi lakini sina amani kabisa." Akasema Joesan. 

"Nakupenda sana honey wangu," 

"Nakupenda zaidi ya unavyonipenda marth...!" 

"Wapenda nao hao, naona mpo kwenye ubora wenu?" Sauti hiyo ikawashtua na kuwatoa kwenye maongezi yao wote wakageukia kule sauti hiyo ilipotokea. 

"Ooh! karibu sana Suzane?" Akakaribisha Joesan baada ya kumtambua mtu huyo. 

"Haa! Jamani Suzane, vibaya hivyo ukipotea ndiyo jiii! Unapotea kabisa jamani!" Alisema Martha huku akimgeukia Suzane, alimlaumu sana, akaendelea. 

"...inamaana bosi wako asipokuwepo nyumbani na wewe huonekani, leo yupo basi na wewe unaonekana vibaya hivyo ujue?" 

"Unanilaumu bure tu shosti ni kweli nastahili lawama hizo lakini kiukweli kazi zinabana sana muda wa kuwa huru ni mdogo sana kiasi kwamba tunashindwa kuonana." Alisema Suzane huku akimpa mkono Martha na Martha naye akaupokea katika hali ya kusabahiana. 

"Muulize mumeo, unafikiri ataniruhusu niondoke kazini ndani ya muda wa kazi?" 

"Mmh! Muda mwingine uwe unamtoroka tu huyu kwani atakufanya nini?" Alisema Martha huku akitabasamu. 

"Humjui Joesan akiwa kazini wewe, muone hukuhuku akicheka tu. Akiwa ofisini ni Simba huyu hataki utani hata kidogo." Alisema Suzane. wakazidi kuongea mengi sana na utani wa hapa na pale. Mwishowe Joesan akamuomba mkewe awapishe kidogo kwani kulikuwa na mambo muhimu walitaka kuyajadili. Anti Martha hakuwa na ajizi ikabidi awapishe ili waweze kujadili mambo yao ya kiofisi kwa uhuru zaidi na yeye akaenda kuwasadaia warembo wale wa jikoni kuandaa chakula cha usiku kwa ajili ya mumewe aliyekuwa akienda kujumuika nao siku hiyo. Joesan ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kuanzisha maongezi. 

"Twende kwenye kitovu cha makutano yetu Suzane muda umekwenda sana. Unajua kuwa nakusikiliza wewe mimi hata sielewi nifanye nini nimechanganyikiwa kabisa." Aliongea Joesan. Lakini muda wote huo wakati Joesan anaongea maneno hayo, Suzane alikuwa ameyaelekeza macho yake lilipo bwawa la kuogelea hali iliyomfanya Joesan naye kuyageuzia macho yake huko ambako mwanadada huyo alionekana kuduwaa. Joesan alichanua tabasamu baada ya kumuona kijana wake akiwa amesimama upande wa kaskazini mwa bustani ile. Palikuwa si mbali sana aliposimama Chriss na wao walipo ingawa kijana huyo hakujua kama mjomba wake yupo mahali hapo. 

"Ile ndiyo iliyokuwa target yangu." Alijisemea moyoni Suzane huku akitabasamu usoni. 

"Joesan!" Aliita Suzane baada ya kujiridhisha na kile alichokiona mahali hapo. Joesan akaitikia kwa kichwa na kumuonesha ishara kuwa anamsikiliza. Suzane akafungua kinywa chake tena na kusema. 

"Nadhani hakuna ugumu katika hili, lisikufanye ukose raha na kushindwa kufanya maamuzi yaliyo sahihi." Joesan akashtuka. Hakumuelewa huyo binti hata kidogo. Jambo hilo siyo zito? Kivipi? Anawaza kufanya nini Suzane mbona kama anashindwa kuelewa. Alijiuliza sana Joesan lakini hakupata majibu ya uhakika ikabidi amtazame kwa kumshangaa maana hata sauti hakuamini kama ingetoka kwa ufasaha kwa jinsi sintofahamu ilivyompata ghafla. Suzane alitabasamu na kuyageuza macho yake kule alikosimama Chriss kabla ya kuyarejesha kwa bosi wake na kunena. 

"Amekuwa kijana mzuri sana Chriss, hongera sana Joesan kwa kumpa malezi bora kijana wako." Joesan akajitahidi kulilazimisha tabasamu, akafanikiwa lakini bado hakumuelewa kabisa binti huyo. 

"Ooh! Yaa, ni jambo la kumshukuru Mungu sana, sasa ni kijana mkubwa!" Joesan alizungumza huku akimuangalia tena Chriss na kuyarejesha macho yake kwa Suzane ambaye bado alikuwa ameliachia tabasamu. alizidisha tabasamu kabisa na kuifanya sura yake ya urembo kuzidi kuwaka. 

"Chriss should be on our program Joesan, amenivutia sana," alisema Suzane huku akiwa ameyakaza macho yake kutazama kule alipo kijana huyo. mshtuko mkubwa ukamkumba Joesan, hakutegemea kupokea kauli hiyo kutoka katika kinywa cha katibu muktasi wake. Alimtazama Suzane kwa mshtuko mkubwa sana. 

"Sijakuelewa Suzane, Chriss anafaa vipi kuwa kwenye mpango wetu?" Alizungumza Joesan. Suzane alimtazama bosi wake usoni kwa muda kidogo na kumuambia. 

"Ondoa waswasi bosi, akatulia kidogo na kuendelea. 

"... maana yangu ni kwamba ni lazima Chriss awe SEX MACHINE!" 

"Eti, nini...?" Alishtuka tena kwa kiasi kikubwa sana Joesan, hilo jambo si kama hakulitegemea tu pekee bali pia lilikuwa haliwezekani kabisa. 

"Joesan nadhani umenisikia kwa dhati kabisa niliyoyasem...!" 

"Hapana Suzane, hilo haliwezekani. Kama hiyo ndiyo ilikuwa plani yako, haiwezekani hata mara moja Chriss is my boy tutafute mtu mwingine." Alilalamika Joesan tena alikuwa akiongea kwa sauti kubwa sana. Alidata kabisa bwana huyo. 

"Kwanini nimuingize Chriss kwenye huu mchezo mchafu, mchezo wa kifo, mchezo ambao sikupanga hata siku moja kuja kumhusisha huyu kijana. Ni kweli nili...!" Alitaka kuongea jambo fulani Joesan akasita. Kwanini alisita baada ya kutaka tu kulitamka jambo hilo? Na ni jambo gani basi? Yote hayo yalikuwa ni maswali ya kujiuliza. Majibizano yale yaliendelea kila mmoja akitaka lake, huyu alisema hivi na huyu alisema hapana na haiwezekani nani ni nani, hakukuwepo na aliyetaka kushidwa. Joesan alilipinga kabisa jambo hilo. Suzane akaona kuwa hakuna sababu ya kuendelea kulumbana kwa jambo ambalo amelibeba kama msaada tu hivyo akaamu kujishusha. 

"Ok, sina njia bosi na najitoa katika jambo hilo mimi sitahusika tena. Niliubeba mzigo wako na kutoa siku tatu tu kwa Mkuu kwa kujua unae Chriss ambaye ni msomi mkubwa na anauwezo wa kufiti vizuri kabisa kwenye hiyo nafasi ya Sex Machine, aliyekufa kwa kazi zenu binafsi. Naomba unisamehe bosi kwa kukushauri vitu vya kijinga." Aliongea Suzane na kuangalia pembeni kabisa. Joesan akapigwa na butwaa jingine la ghafla. Ni kweli alikuwa hapendi Chriss aingie kwenye huo mchezo lakini kwa hilo alilolizungumza Suzane hapo ni kwa namna gani atalikabili. Suzane ni mtu ninayemtegemea sana, sasa vipi kama akiacha kunisaidia. Aliwaza Joesan kisha akasema; 

"Hapana Suzane, huu mchezo hauhitaji hasira, kwanini unafanya maamuzi magumu hivyo nadhani unajua ni kwa jinsi gani ninavyo kutegemea?" Suzane akageuka na kumtazama bosi wake huyo usoni na kumwambia. 

"Hakuna njia ya kupita Joesan zaidi ya hiyo, unadhani tutafanya chaguo gani zaidi ya hilo?" Joesan alishusha pumzi nzito sana. Hapo najua hawezi kupindua, hana chaguo jingine Joesan zaidi ya kijana wake labda kama atafeli jaribio lakini kama atashinda, Chriss anafaa sana, rangi yake, kifua chake kipana na mwili wake kwa ujumla vimenivutia sana hata mimi namtamani. Aliwaza Suzane huku akiwa anamtazama bosi wake kwa tabasamu zito. Joesan hakuwa na la kufanya alijikuta mpole ghafla. Jibu alilo bakiza ni moja tu na hilo ndilo ambalo lilikuwa likisubiriwa na huyo msichana. 

"Unadhani tutaweza kumshawishi vipi hadi kuingia kwenye hii kazi?" Aliuliza Joesan. 

"Joesan! Usitake kuniambia hujui. Yule ni kijana wako na anakusikiliza sana acha huko kukuheshimu, sidhani kama ukimwambia kuwa unajambo la msingi unataka kumueleza, anaweza kukukatalia. Hakikisha unaongea naye mambo mazuri na kila ulichomuahidi sasa kinakwenda kutimia na wewe mwenyewe unajua Joesan kuwa anakwenda kuiingizia kampuni mamilioni ya mapesa lakini hata yeye ataingiza pesa nyingi zitakazo badilisha maisha yake kwa kazi hiyo." 

"Ndiyo najua," akadakia Joesan na kisha mwanadada huyo akaendelea. 

Comments

Popular posts from this blog

SMS 47 ZA MAPENZI ZITAKAZO MNYEGEZA** MPENZI WAKO

KWANINI WADADA WENGI WAREMBO NA WANAOJIONA WAREMBO HUCHELEWA KUOLEWA,HUKOSEA KUOLEWA AU KUTOOLEWA KABISA?SOMA HAPA

HATUA ZA KUCHEZEA KIHARAGE NA KISIMI