SEX MACHINE - SEHEMU YA 07


"Joesan! Usitake kuniambia hujui. Yule ni kijana wako na anakusikiliza sana acha huko kukuheshimu, sidhani kama ukimwambia kuwa unajambo la msingi unataka kumueleza, anaweza kukukatalia. Hakikisha unaongea naye mambo mazuri na kila ulichomuahidi sasa kinakwenda kutimia na wewe mwenyewe unajua Joesan kuwa anakwenda kuiingizia kampuni mamilioni ya mapesa lakini hata yeye ataingiza pesa nyingi zitakazo badilisha maisha yake kwa kazi hiyo." 


"Ndiyo najua," akadakia Joesan na kisha mwanadada huyo akaendelea. 

"Sasa, anakwenda kuwa milionea. Hakuna mtu anayekataa pesa lazima ukimueleza hili atakubali hawezi kukataa hata kidogo." 

"Hata hivyo sina hakika kama Chriss anaweza kukubali kirahisi, huyu ni kijana mbishi sana kuelewa," akasema Joesan. 

"Joesaan!" aliita binti huyo na kuendelea. 

"... si wewe wala mimi atakayembadilisha Chriss. Chriss atabadilishwa na Sex Machine Controller (SMC). Hii ndiyo itakayobadilisha maisha yake na akiwa mbishi tutajua njia nyingine ya kufanya hatujawahi kushindwa na binadamu wa kawaida hata siku moja we mwenyewe unajua." Aliongea kwa kiburi sana. 

"Ooh! Yeah, nilitaka kusahau jambo hilo. Hapo sawa sina kipingamizi tena." Akasema Joesan huku akionekana dhahiri kuushusha mzigo mzito sana wa mawazo kichwani mwake. 

"Nashukuru sana bosi kama tumeweza kufikia muafaka. Suala lilikuwa dogo sana ulitaka kulifanya kubwa bure tu." Aliongea binti huyo na kumalizia kabla ya kuondoka. 

"... jaribio la kwanza ni leo, naomba umtume nyumbani kwangu kwa njia yoyote ile ifikapo saa mbili usiku. Kifua chake kimenivutia sana sasa nataka kuiona shughuli yake awapo kitandani na mzigo alionao si unajua tunatafuta watu walio kamilika kila idara?" Kisha akaondoka mahali hapo mara baada ya kusema maneno hayo na kumuacha Joesan mdomo wazi. 

"Huyu mtoto si dhani kama atakuwa yuko sawa." Aliesema bwana huyo huku akicheka cheko la ndani kwa ndani. 

Aliondoka kwa mwendo wa Twiga binti huyo, umbo lake jembamba lililojigawa chini kuanzia kiunoni kwenda chini na kumfanya kuonekana mrembo zaidi. Alikuwa akilitingisha umbo hilo kutokana na mwendo wake wa ki-miss lakini macho yake hayakuacha kumtazama Chriss. Hata alivyokuwa amemkaribia bado alikuwa akimtazama kwa matamanio makubwa sana. Na kutokana na kijana huyo kuwa amezama ndani ya jinamizi la mawazo, basi ndiyo kabisa mrembo huyo aliiyona kuwa hiyo ndiyo nafasi ya pekee kabisa kwa majira hayo ya kuweza kumtazama awezavyo. Alikuja kuacha kumtazama mara baada ya kumpita kwa hatua tano ndipo akaacha kabisa zoezi hilo la kumtazama na kuondoka zake. Amenivutia sana huyu kijana, natamani ndiyo ungekuwa muda huu niko nae kitandani nakichezea kifua chake huku na yeye akiyatomasa maungo yangu aaaaaaah! 'I was a mad'. Lazima nilale nae ili nijue uwezo wake. Alijisemea moyoni dada huyo alipokuwa garini akirudi zake nyumbani kwake. 

Chriss alijawa na mawazo sana siku hiyo hakuwa na furaha hata kidogo. Moyo wake ulikuwa umebeba mzigo mzito wa majuto. alijuta kushiriki mapenzi na wasichana hao kwani kitendo hicho cha kufanya nao mapenzi wote wawili ndicho kinachomfanya kukosa raha, furaha ilimkimbia kabisa kijana huyo. Macho yake yalikuwa yakitazama mbele lakini lenzi ya jicho lake ilikuwa haioni picha yoyote ile na hata kama angetokea mtu mahali hapo na kumuuliza ni nini atazamacho, ni wazi asingekuwa na jibu la kuridhisha. Salome sitokaa nikupende tena wewe mwanamke, umekuwa sababu kubwa ya haya mawazo. moyo wa Chriss ndivyo ulivyokuwa ukizungumza pasi na kuushirikisha mdomo wake. Bila ya wewe ninaimani isingefikia mimi kutembea na Maida. Ona sasa nimetembea naye na si yeye tu bali pia nimetembea na ninyi nyote hata hivyo sikulaumu. Ndiyo, sikulaumu kwasababu umenifanya nisiione thamani yako tena mbele ya Maida. Sikuwahi kufikiria kama ipo siku ningekuja kukutana na mwanamke mtamu kama Maida, mwanamke niliyemfundisha mwenyewe mapenzi kwa kuuharibu usichana wake, nakiri kuwa 'i love this girl.' Utanisamehe Salome na naomba ukae mbali kabisa na mimi. Moyo wa kijana huyo ulizidi kutiririsha maneno kisha akatabasamu, tabasamu ambalo ni ishara tosha kuwa kile ambacho kimetoka kuzungumzwa na moyo wake amekiridhia na kukipitisha. 

____________ 

Wakati Chriss akiwa anazidi kuwaza na kuwazua hili na kulitoa lile, huku nyuma kulikuwa na mtu ambaye alikuwa akijivuta taratibu na kusogea mahali alipo. Si kama hakuhisi kitu la! Alihisi sana na hisia zake zilimwambia kabisa kuwa kipo kiumbe kinakuja mahali hapo lakini kwa kuwa ni mazingira ya nyumbani, hakushtuka wala kujisumbua kutaka kujua kiumbe huyo ni nani. Alijiaminisha kuwa kitakuwa ni kiumbe salama na hakitakuwa na madhara yoyote ile kwake. Kiumbe huyo alisogea hadi ubavuni mwa Chriss upande wa kushoto, akasimama sawa kabisa na Chriss. Akasema; 

"Uncle, unawaza nini uncle...?" Ndivyo alivyosema mtu huyo ambaye hakuwa mwingine bali Joesan. Chriss alichelewa kidogo kulijibu swali hilo hivyo Joesan akaendelea. 

"... nilikuwa nimesimama pale kwenye yale maua nikitazama mazingira kidogo, ndipo nikakuona hapa muda mrefu sana ukiwa umetulia tuli, nikajua si kawaida yako ni nini mjomba?" 

"Mmh!...ha...hapana uncle, nimeamua tu kutulia hapa kwasababu sijisikii kufanya kitu chochote kwa wakati huu!" Akasema Chriss kwa kitete kidogo. Joesan aliacha kumuangalia Chriss na kugeukia upande ambao kijana huyo alikuwa akiuangalia kwa muda mrefu sana, akashusha pumzi ya wastani kidogo na kusema; 

"Unajua Tikiti maji ni tunda hata likiwa changa lakini thamani yake ni kubwa zaidi linapokomaa!" Chriss akashtuka kwa kauli ile ya mjomba wake. Nini maana ya msemo huo. Akamgeukia mjomba wake na kumtazama kwa makini zaidi. Ni nini anachokimaanisha sasa? Ndilo swali lililokuwa limekitawala kichwa chake kwa majira hayo. Joesan akajifanya kutouona mshtuko wa kijana wake huyo na kuendelea na kile alicholenga kukisema huku akiwa bado anatazama mbele hivyo hivyo. 

"Huwezi kuyazuia matamanio ya watu juu ya kile wanachokitamani." Akaweka tuo na kendelea tena.

"... Chriss, umeshakuwa kijana mkubwa sasa. Kuna maamuzi ya lazima yaani haya huna budi kuyafanya hata hivyo kuna mambo mengine huja tu yenyewe, haya nayo pia huna budi kukabiliana nayo." Akaweka tuo tena kisha akamgeukia na kumtazama usoni, akatabasamu kidogo na kumalizia. 

"... huna budi kuyaacha yafanyike yaliyojitokeza kwenye maisha yako. Huna njia ya kuyakimbia na uzuri wa changamoto ni kuitafutia ufumbuzi na siyo kuikimbia." 

"Sijakuelewa mjomba ungeniambia unamaanisha nini labda?" Akauliza kwa mshangao mkubwa sana Chriss. 

"Najua kuwa hujanielewa," akasema na kutulia kidogo kabla kuendelea na alipokomea. 

"... lakini maana yangu si kwamba unielewe sasa Chriss. Ninachotaka kukwambia kwa sasa ni kwamba, usiibebeshe mzigo mzito akili yako kwa kumuwaza Salome na Maida." 

"Mungu wangu!" Moyo wa Chriss ulipiga sarakasi za nguvu na kubadili kabisa mfumo mzima wa mapigo yake. Amejuaje? swali hilo jingine likakivaa kichwa chake. Aliogopa sana. Inamaana na mjomba amejua? Mungu wangu, atanielewa vipi sasa tena amejua kuwa wote nimetembea nao. Ndiyo maana yake, kwanini sasa amewataja wote kwa pamoja? Si inamaana...mama weee! Hii ni mbaya kabisa hii. Alichanganyikiwa kijana huyo, hofu ya kuonekana mshenzi wa washenzi ndiyo iliyokuwa ikimtafuna. Hakutaka kuamini mara moja kuwa eti, mjomba wake amejua. 

"Chriss!" Aligutushwa kijana huyo kutoka mawazoni kwa wito huo. Chriss aliogopa hata kumtazama mjomba wake usoni na kuyaelekeza macho yake chini lakini hali hiyo haikumfanya Joesan kutokufikia amuzi lake au kuacha kusema alichopanga kukisema. 

"Giza limeingia sasa my boy acha mimi nielekee ndani ila ukitoka hapa unione kuna mahali nahitaji kukutuma usiku huu hivyo ni vema zaidi kama ungejiandaa mapema ili uwahi kurudi," kisha akaondoka mahali hapo akimuachia kijana wake sinto fahamu ya hali ya juu kabisa. Joesan alifika sebuleni na kujibwaga sofani, macho yake akiyaekekeza runingani. Naamini hakuna kitakacho haribika, acha nimtumie huyu kijana na ninaimani naye sana. Aliwaza Joesan akiwa anazirusha hatua zake kumtoa hapo bustanini. Chriss si lele mama hata kidogo, amepitia mafunzo makali ya kimapigano yale ya self face difence na ya silaha pia hivyo ninampeleka kijana ambaye hata mkuu mwenyewe hataamini. Sikuwa na lengo la kukufanyia hayo my boy lakini sipendi kuupoteza utajiri wangu. Nitaulinda utajiri wangu hata kama ni kwa kuyatoa maisha ya mtu. Alizidi kuwaza bwana huyo na mawazo yake hayo yalikuja kukoma mara baada ya Chriss kufika na kukaa kwenye kochi la pembeni yake. Akamgeukia na kumwambia. 

"Kula kwanza basi ili uwahi kwenda," 

"Hapana anko ni vizuri ningekwenda kwanza kula nitakula hata nikirudi," akajibu Chriss. 

"Ok, sawa kamata hii." Akamkabidhi bahasha ndogo ya khaki, Chriss akaipokea kisha Joesan akasema; 

"Utakwenda nyumbani kwa Suzane na kwenda kumkabidhi hiyo bahasha. ukifika wewe muachie tu mimi nitaongea nae." 

"Sawa mjomba basi acha niwahi." 

"Kuwa makini na barabara maana wewe na gari kama mlizaliwa pamoja." 

"Ondoa shaka anko," aliongea Chriss na kutoka mule ndani. alichagua gari ambayo anaipeda kuliko gari zote zillizopo hapo na kuingia garini humo. Suzane amekuwa ni mtu anayenisaidia sana ninamuamini na ninaamini hawezi kushindwa kumshawishi huyu kijana. Nimekuwa karibu nae kwa miaka mingi sana na ninamjua kinagaubaga. Aliwaza Joesan na kujinyanyua pale kochini na kwenda kuchukua mkanda mzuri wa muvi apendayo kuangalia na kuiweka. akajitupa tena sofani akiwa na rimoti mkononi. 

Safari haikuwa ndefu sana hivyo Chriss alifika nyumbani kwa Suzane kwa muda mfupi sana. Akapaki gari maegeshoni na kutembea mwendo wa haraka hadi ulipo mlango wa mwanadada huyo. Sauti ya kugongwa kwa mlango ndiyo iliyomshtua Suzane ambaye alikuwa mezani akijipati chakula cha usiku. Akaamka na kuelekea mlangoni kabla ya kufungua mlango kwanza alichungulia kwenye kijitundu kidogo kinachoruhusu kumuona mtu aliyeko nje kisha akaufungua mlango huo. Tabasamu pana likiwa usoni mwake. 

"Karibu sana Chriss, karibu ndani." Alikaribisha. 

"Asante madam habari za hapa?" Alijibu salamu Chriss na kusalimia. 

"Za hapa nzuri sijui za huko utokako?" 

"Za huko ni nzuri pia," alijibu na kuingia ndani, Suzane aliufunga mlango kwa komeo kabisa na kumpita kijana huyo akiwa amesimama. 


Comments

Popular posts from this blog

SMS 47 ZA MAPENZI ZITAKAZO MNYEGEZA** MPENZI WAKO

KWANINI WADADA WENGI WAREMBO NA WANAOJIONA WAREMBO HUCHELEWA KUOLEWA,HUKOSEA KUOLEWA AU KUTOOLEWA KABISA?SOMA HAPA

HATUA ZA KUCHEZEA KIHARAGE NA KISIMI