SEX MACHINE - SEHEMU YA 09

"Nimechanganyikiwa Maida na ndiyo maana nipo hapa kwa ajili moja tu ya kukuuwa." Alisema Salome na kumfanya Maida ashangae na kuangua kicheko kabisa. 

"Hee! Hivi umechanganyikiwa wewe yaani huoni hata haya eti, niko hapa kwa ajili ya kukuuwa (akabana pua yake kwa vidole viwili na kuifanya sauti itokekee nyembamba ya dhihaka), yaani wewe uniuwe mimi?" 

"Kwaiyo unashangaa kuwa mimi siwezi kukuuwa au kinachokushangaza ni nini, ngoja uone vile nitakufanyia sasa!" Alisema Salome wakati huo akiwa tayari ameshamsogelea Maida karibu. 

"Siwezi kukuacha Maida, mimi moyo wangu kwa sasa hauna amani sababu yako. Umeninyang'anya furaha yangu, siwezi kuishi kwa namna hiyo. Chriss hataki hata kuniona mimi sababu yako?" Aliongea kwa uchungu mkubwa sana Salome. Maida alimtazama binti huyo kwa dharau kubwa kisha akatazama pembeni akasema; 

"Nilidhani labda leo umewekwa style ya mbuzi kagoma kwenda ndiyo umekuja kunihadithia kama kawaida yako kumbe limekushuka pol...!" Hakufika mwisho wa kauli yake Maida, kofi zito la haja likatua kwenye shavu lake la kushoto. Maida alihisi kama shavu linataka kudondoka, nyama za shavu zilimchonyota. Binti aliyerusha kofi hilo akawa anatamba kwa maneno. 

"Unadhani nimekuja hapa kucheza ngonjera siyo, Maida hujui kuwa maneno yako ni kama kisu butu kwenye shingo yangu? Inamaana hujui kama naumia Maida, hujui?" 

"Salome unathubutu kunipiga?" Badala ya kujibu maswali aliyoulizwa Maida akainuka na swali huku akiwa kalishika shavu lake lililokuwa likimuwanga kwa kipigo. 

"Na siyo kukupiga tu mwanahizaya wewe, leo lazima ucheze ngoma ya asili ya kabila letu." Alibwata Salome. Hasira kali zikampanda Maida aliinuka kama Nyati na kumvaa Salome na kumtupa kweye meza iliyopo chumbani hapo. Salome akajipigiza kwenye mbao ngumu ya meza hiyo hadi paji lake la uso likapasuka. Damu nyingi zilimtoka. Maida hakujua alilolifanya ni kosa linalokwenda kuyagharimu maisha yake. hakujua kuwa mwenzake hakuwa na imani, tena roho yake ilibadilika kabisa na kuwa ya mnyama hatari. Aliinuka kutokea mezani hapo mithili ya mzimu akafunua gauni alilolivaa na kujipekuwa kwenye kufuli lake akatoka na kisu. Maida akabaki mdomo wazi kwa kile alichokiona hapo kikifanywa na mwanamke mwenzie tena pasipo matarajio yake. Kisu kile kikajaa kifuani. Maida akatokwa na ukelele mdogo, Salome akachomoa na kukirudisha tena tumboni mwa mtu ambaye walikuwa wakichangia jiko pamoja wakiwa katika harakati za kuwaandalia mabosi wao chakula. Kisu kile kikafanya kama kilivyoagizwa. Maumivu makali yakazidi kumtambaa binti huyo masikini. Salome hakuwa yeye tena akakitoa na kuchoma tena na tena ni kama alikuwa akiamrishwa hivi hadi pale Maida alipodondoka chini akiwa anapambana na hatua za mwisho za uhai wake ndipo jini baya la ukatili likavuka mwilini mwa binti huyo na kumuacha mwenyewe. Kitu cha kwanza kukiona kilikuwa ni kisu kilichojaa damu nyingi mkononi mwake, macho ya hofu yakamtoka pima. Alipokuja kutazama sakafuni kulikuwa na dimbwi dogo la damu, hapa aliogopa zaidi na mbaya zaidi ni pale alipomuona Maida akiwa chini akikunja na kunyoosha miguu ikiwa ni moja ya hatua za mwisho za kupambana na sakaratul mauti. 

"Mama weee! Nimeuwaaa!" Alikema vibaya sana sauti kubwa ikapaa. akajirusha mlangoni ili aweze kutoka mule ndani, akajipigiza mlangoni na kudondoka chini akakukuruka na kunyanyuka kwa spidi kali, sasa badala ya kuwa mlangoni akajikuta kwenye mwili wa Maida ambaye kwa wakati huo jina lake lilikwisha badilika tayari. Alikuwa ni marehemu. 

"Mayooo!" Aliita mama kikwao. 

"Nimeuwa kweli mimi Salome! Haa! Maida nilikuwa nakutania tu amka bwana usife kweli!" Ama kweli upumbavu huja mara moja tu pasipo matarajio. Unawezaje kumtania mtu kwa kumkita mara zaidi ya nyingi. Wimbo wake wa kuwa nimeuwa kweli ukachanganya, akachoropoka huku akipiga kelele akimuita bosi wake kwa hamaniko kubwa kabisa. 

____________ 

"Hapana Chriss leo nimechoka sana tufanye siku nyingine bwana," alikuwa ni Suzane ambaye alitoa malalamiko mbele ya kidume cha mbegu kilichokuwa kinataka mchezo urudiwe. Alimuweka kwenye himaya yake hadi mwanadada huyo akakosa kufurukuta, akabaki akitumia utetezi wa maneno. Chriss ikambidi kuwa mpole na kuamua kuchukua nguo zake na kuzirudisha mwilini kisha alimuaga mrembo huyo na kuondoka. Chriss alipotoka tu mazingira hayo, Suzane alichukua simu na kumpigia Joesan. simu iliita kwa muda mrefu sana pasipo kupokelewa, akarudia tena na tena hata hivyo bado iliita tu. 

"Mh! Atakuwa amelala huyu hebu niache asijekupokea mkewe ikawa shida maana namjua vema Martha kwa wivu." Alisema lakini wakati akiwa anawaza hayo, simu yake ikaita na mpigaji akiwa ni Joesan. 

"Vipi Chriss ametoka kwako tayari?" Lilikuwa ni swali la kwanza kutoka kwa Joe. 

"Ndiyo, mbona unawasiwasi sana Joe?" 

"Hapana ooh...! Ngoja kuhusu yaliyojiri huko utanieleza kesho kazini hapa nyumani kuna tatizo kidogo limejitokeza hivyo hatutaweza kuelewana." Alizungumza Joe. 

"Ok, bosi," akajibu Suzane. 

Chriss alifika nyumbani akajua amechelewa sana hivyo hawezi kueleweka kwa mjomba wake lazima ataonekana kuna sehemu amepitia. Hata hivyo hakujua kuwa ni yeye ndiye anayechezewa share. Hali ya tafarani ndani mule ikamtisha, akawa anaingia kwa kunyata kuhofia isije ikawa ni majibizano kuhusu yeye hata hivyo alivyozidi kuvuta hatua ndipo aliposikia kuwa Maida amekufa kabla hata ya kufika hospitali. Mwili ukaanza kuingiwa na baridi ni Maida yupi, aliyemuacha nyumbani au ni yupi? Yakawa ni maswali ya kujiuliza kichwani mwake. Akafika sebuleni pale ambapo ndipo mjadala ulipokuwa ukiendelea. 

"Maida yupi Uncle...?" akajikuta akipata msukumo mkubwa wa kuuliza swali. Wote pale ndani wakawa kimya hakuna aliyejua alijibu vipi swali hilo japo ilijulikana kuwa ni Maida wa humo ndani. Mjomba alishajua moyo wa Chriss ulipo lalia, ni vipi sasa akisema eti, Maida ameuwawa na Salome? Joesan alimjua vizuri kijana wake, Salome asingeachwa salama. Sasa ili kutomchanganya kijana huyo na mambo yaliyokusudiwa yasiharibike ni kumdanganya. 

"Ni Maida wa humu ndani Chriss na amedondoka ghafla tu chumbani kwake. Salome ndiye aliyetuletea taarifa hiyo. nimejaribu kumkimbiza hospitali lakini hali si hali tulichelewa!" Alisema Joe huku akionesha masikitiko makubwa sana. Chriss alijisikia vibaya sana kwa taarifa hiyo. Alisha muhusudu binti huyo na alishaweka nadhiri kuwa Maida ndilo chaguo lake, leo eti, anapokea taarifa ya kifo chake. Maida alikuwa anasumbuliwa na nini? Mbona ghafla namna hii? Kwanini Salome awe wa kwanza kupokea taarifa hiyo na kuja kumjuza Uncle? Si bure? Aliwaza Chriss na mwisho akajishauri na kuelekea mbio chumbani kwa Maida. Chumba kilikuwa kimefungwa. akanyong'onyea, alipogeuka nyuma akakutana uso kwa uso na mjomba wake. 

"Chriss hata sisi pia tumeumizwa sana na hili jambo, hutakiwi kuwa katika hali hiyo uliyokuwa nayo sasa." Alizungumza Joesan kwa sauti ya upole sana. 

"Lakini Unle kwa nini hiki chumba kimefungwa sasa?" Aliuliza Chriss. Joesan akajibu. 

"Ndiyo, tumekifunga ili kisitumike tena kwani huwezi jua baada ya mwili wa marehemu kufanyiwa uchunguzi, wakahitaji kujua mazingira ambayo marehemu alifia. Sasa kuingia kwako kunaweza kuwa siyo sahihi kiusalama." 

"Ok, nimekuelewa mjomba sasa Salome yuko wapi kwa sasa?" akauliza Chriss akiwa amechanganyikiwa wazi wazi. Joesan baada ya kuulizwa swali hilo ilibidi awe mpole kwanza hakutaka kukurupuka kulijibu kwani baada ya binti huyo kufanya hilo tukio, alikimbilia chumbani kwake na kujifungia hivyo haikujulikana huko aliko anafanya nini au amechukua amuzi gani. Alichokifanya kwa wakati huo Joesan ni kukimbilia chumbani kwa Salome ili kujua usalama wake. Chriss naye akakimbilia huko huko huku akiwa na alama ya kujiuliza kichwani mwake, nini hasa sababu ya mjomba wake kukimbia kwa haraka namna hiyo mara tu alipomuuliza hilo swali. Waligonga mlango lakini haukufunguliwa hata kidogo, Joesan akaenda chumbani kwake na kwenda kuchukua ufunguo wa hakiba ili kuweza kuufungua mlango huo. 

"Mjomba kunausalama kweli lakini?" akauliza Chriss akiwa ametoa macho. 

"Hata sielewi mjomba, hawa watoto wananichanganya kabisa," alijibu Joesan. Walipofanikiwa kuufungua mlango huo, jambo la kwanza kuliona ni sakafu ya chumba kile ambacho alikuwa akikitumia binti huyo, ilikuwa haitamaniki kwa damu. Joesan macho yakamtoka kama mjusi aliyebanwa na mlango. Hofu ikawatanda. Joesan akapagawa kabisa. Kitendo cha kumficha Salome kwa dakika chache ili tu kumsitiri na hasira za Chriss endapo angemkuta katika hali ile ya kuchanganyikiwa ilhali akiwa na damu mwili mzima, vipi sasa akute damu na asimkute muhusika. Chriss alishindwa kuelewa ni kwanini yale yote yanatokea. Nini sababu ya mambo yote yale, hakuelewa hata kidogo. Wakaingia mule ndani kwa mwendo wa taratibu huku wakiangaza macho yao kwenye kila kona ya chumba hicho. 

"Salome.......! Salomee......!" Aliita Joesan bila mafanikio. Wakaendelea kutafuta mule ndani. 

"Unauhakika mjomba kuwa Salome yuko humu ndani?" Akauliza Chriss. 
"asilimia zote na aliingia humu ndani akiwa amechanganyikiwa sasa sielewi ata...!" Akakatisha maneno yake Joesan baada ya kusikia sauti za manung'uniko kuashiria kuwa kulikuwa na mtu aliyekuwa akipambana na maumivu makali sana. Wakaelekea kwenye upande mmoja wa kitanda, huko wakamkuta Salome akiwa anapambana na maumivu si ya kawaida huku kisu kikiwa kifuani mwake. 

"Salome nini tatizo mbona umechukuwa maamuzi magumu hivi? Kwa nini unataka kujiuwa?" Aliuliza Chriss akiwa na sura ya huruma sana. Zile hasira zote juu ya msichana huyo ziliyeyuka huruma kwake kilikiwa ni kitu cha kwanza kumkaa moyoni mwake kijana huyo. 

"Niambie Salome nini tatizo?" Alizidi kuuliza. Salome akalilazimisha tabasamu lakini ilionekana dhahiri maumivu aliyokuwa akiyapata yalikuwa si lelemama hata kidogo. Sura yake haikukunjuliwa kabisa na tabasamu hilo. Akanyanyua mkono wake mmoja na kulishika paji la uso la Chriss na kulipapasa kisha akasema; 

"Ni...ni...sa...mmehe...sana...!" Akanyamaza kidogo na kuikunja sura yake hadi pale maumivu yalipopungua kiasi akaendelea. 

"... Chriss nimeamua kijiuwa ili kuukwepa mkono wa sheria, najua mjomba anao uwezo wa kunipeleka Hospitali na nikahudumiwa hadi kupona lakini sihitaji kupona Chriss, napenda nife tu." Mkono wa sheria...kuukwepa mkono wa sheria...? Kivipi yaani kuna nini amefanya hadi aogope mkono wa sheria...? Aliwaza Chriss hata hivyo akalipuuzia hilo kutokana na hali ya Solome kwa wakati huo ilivyo. 

"Hapana huwezi kufa hata kidogo Salome lakini kwanini umeamua kujikatishia maisha?" Akauliza Chriss akiwa kamshika mabegani. 

"Chriss nakupenda na nimeamua kufa kwasababu tu nakupenda. Sikuiona sababu ya kuendelea kubaki hai wakati sipo moyoni mwako, sikuona sababu hiyo hata kidogo," akaweka pumziko na kulazimisha cheko lililojaa maumivu. Damu zikamtoka kinywani kwa wingi sana lakini hakuacha kucheka hadi pale alipogoa akatulia zaidi halafu akaendelea kusema; 

"Unajua kwanini ninacheka? Unajua au hujui...?" Alivyosema hivyo akayageuza macho yake na kumtazama Joesan ambaye alikuwa kimya muda wote. Joesan akatikisa kichwa kukataa kuwa asiseme hicho alichotaka kukisema lakini Chriss aligeuza haraka shingo yake na kumtazama mjomba wake na kumkuta katika hatua za mwisho za kutingisha kichwa. Akashangaa na kunyanyuka kwa hasira sana na kumkabili mjomba wake kwa maneno. 

Comments

Popular posts from this blog

SMS 47 ZA MAPENZI ZITAKAZO MNYEGEZA** MPENZI WAKO

KWANINI WADADA WENGI WAREMBO NA WANAOJIONA WAREMBO HUCHELEWA KUOLEWA,HUKOSEA KUOLEWA AU KUTOOLEWA KABISA?SOMA HAPA

HATUA ZA KUCHEZEA KIHARAGE NA KISIMI