MAMBO 10 YA KUFANYA BAADA YA KUBAINI UMESALITIWA NA MPENZI WAKO!
Karibu mpenzi msomaji kwa kunitembelea katika blog yangu hii, Leo napenda kushea nawe kitu muhimu katika maisha ambacho kinajitokeza mara kwa mara katika uhusiano na mahusiano kwa ujumla . Katika maisha ya kimapenzi hakuna kitu kinachouma kama kusalitiwa, tena kusalitiwa kunakouma zaidi ni pale ambapo unapobaini mpenzi wako amempa penzi mtu unayemjua halafu ukijilinganisha wewe na huyo aliyepewa unashindwa kuelewa kilichomshawishi mpenzi wako huyo kufanya hivyo. Lakini licha ya kwamba usaliti si kitu kizuri, watu wamekuwa wakisalitiana, tena sana tu. Inafika wakati unashindwa kuamini kama yupo mtu ambaye hajawahi kumsaliti mpenzi wake. Niseme tu kwamba wapo wachache waliotulia ila asilimia kubwa ya walio kwenye uhusiano na mahusiano ni wasaliti hata tafiti zimethibitisha hilo. Kama hali yenyewe iko hivyo, cha kujiuliza ni kwamba unapobaini mpenzi wako kakusaliti ni kipi unachotakiwa kufanya? Je, ni kuamua kunywa sumu kama ambavyo wamekuwa wakifanya wengine? Sidhani kama huo...