RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA 31
Endelea.......
.............Tulibaki kushangaana mule ndani hali kila mmoja ana maumivu yake. Kwa upande wa Mshana alichukia sana kuhusu kile kitendo kwa kuwa anafahamu nini kimefanyika.
Ghafla nje tunasikia watu wakikimbizana ovyo na wengine wakiwa wanalia moja kwa moja tulijua kuwa lile lijitu limeanza kuua watu. Kumbe haikuwa kama vile ambavyo tumefikilia ilikuwa ni tofauti kabisa.
Mimi na Mshana tulitoka taratiibu na kuelekea nje ili tukaangalie nini kimetokea.
"Mshana.."
"Eeeh!"
"Unajua tufanye nini hapa.."
"Nakusikiliza Mnali"
"Inabidi tufute kwanza mawazo ya kwenda kwa mganga kwanza tuwaze mengine kabisa alafu baadae inawezekama tukawaza hilo na tukaenda kabisa".
Alikubali wazo langu japo ni ngumu kuacha kuwaza jambo ambalo lipo kichwani mwa mtu alafu umuambie kuwa asijaribu kabisa kuwaza ni jambo la ajabu. Tulipotoka nje tukawaona watu kadhaa wanakimbia ndipo walipofika pale tulipo na kuanza kuhema kwa harakaharaka sana. "Nini tatizo niliwauliza".
"Jamanii baharini kuna matatizo"
"Matatizo gani tena".
"Mudaa huu huu watu watatu wamekufa kwenye maji...alafu kama kuna viumbe wameonekana wawili wakizama na kupotea kabisa".
Nilishika kichwa changu pale huku nikiwaza nini tena hiki kinakuja kukumba sehemu muhimu ya kuingiza kipato changu. "Sasa mmefanya nini huko?".
"Watu wamejaa sana na sisi tunakimbia maana polisi wanaingia sasa hivi".
Pale niliona kuwa kutokana na yale maisha nisije kumpa tabu yule rafiki yangu bora hata nitafute sehemu ya peke yangu nikae. Nikiwa nawaza hilo nilirudi ndani baada ya kuhakikisha kuwa hata ile sauti sijaisikia tena. Kipindi hiki nilikuwa nimepona kabisa sina hata tatizo lolote mwilini kwangu, zaidi ya hili janga jingine.
Usiku tukiwa tumelala. Niliota ndoto ya ajabu yenye kunitishia maisha yangu. Niliota kuwa kuna watu wawili wametoka kwenye kina kirefu cha bahari na kuingia nchi kavu wakinitafuta mimi ili waje kunimaliza na walikuwa na hasira sana pia wakasema kuwa muda si mrefu wanakuja baada ya kumaliza damu changa.
Ile ndoto ilinitisha kiukweli.
Ilikuwa majira ya usiku sikujua saa ngapi kwa kuwa sikuwa na saa. Kelele za gari nilizisikia hapo nje zikipitapita. Tulitulia kimya wote bila hata kujinyoosha hata kama mbu walikuwa wanagonga kwa kiasi gani. mpaka inafika asubuhi tulitoka huku nikiwa na shaka kwa kuwa nilijua labda wale ambao wananifuata sana. Nilimuambia Mshana kuwa hawa watu walikuwa wananijia mimi hapa. Ikiqa mawazo yangu ni kuondoka pale kwa bwana Mshana kwa kuhofia majanga ambayo yatakayotokea mbeleni.
nilianza kusikiliza kama ile sauti ya yule kiumbe kipp karibu nilihisi kuwa hayupo karibu yetu hapo ndipo nikamsogelea Mshana.
"Mshana ndugu yangu"
"Ndio niambie mnali"
"Unajua kuwa hizi tairi ni za gari na pia zilikuwa zinakuja kunifuatilia mimi hapa"
"Ni kweli naona si ndio lile lililokuwa linanguruma majira ya asubuhi"
"Ndio kabisa na nahisi Kuwa kiumbe kinachonifuata ndicho kinaua watu huko baharini.."
"Kwa nini unasema hivyo mnali? "
"Unakumbuka Kuwa ile siku nimeenda kuvua samaki wale samaki waliliwa na lile jitu sasa nahisi linapenda sana nyama mbichi ndio maana nasema hivyo".
"duu! Mnali sasa tunafanyaje kuhusu hili?"
"Mawazo yangu mimi niache niondoke nikatafute maisha yangu kule kijijini ambako Mke wa Kibona anaishi kabla ya kwenda kwetu kama mtoto najua ipo siku atanifuata tu".
Mshana alinishangaa sana kwa ile kauli ambayo nilikuwa naiongea pale kisha akanishika mkono na kunivuta.
"Unajua mnali tufanye jambo moja hivi kwamba... ngoja nifunge mlango". Alienda kufunga mlango huku nikimshangaa anataka kufanya nini. baada ya kumaliza alinijia hadi pale nilipo kisha akaniangalia.
"Mnali unafikiri kuwa ni rahisi kuzungumza tu. unamuachia nani familia yako badala ya kuifuatilia na ujue wapi imeelekea au imehifadhiwa wapi eti unataka kukimbia".
nilibaki kuduwaa tu pale kwa kuwa sikuwa na hata ujanja wa kusema kwani ni kweli kabisa kwa kile ambacho anakisema mshana. mimi kama baba wa familia sina budi kupambana na kuhakikisha kuwa familia yangu naiweka kwenye himaya yangu.
Alinishika mkono na kunivuta huku tukitoka pale ambapo tulisimama. Nilimuomba tukae kidogo ili tuweze kuongea kirefu kuhusiana na jinsi gank naweza kuipata familia yangu. tulikaa kwenye benchi lililopo karibu na pale tulipo.
"Mshana unajua kuwa kuna watu ndugu zangu na marafiki zangu wa karibu sana wananifuatilia sana mimi hadi hapa nilipo"
"Kwa nini na akina nani hao wanaokufuatilia wewe"
"Mshana wewe ni rafiki ambae unaonyesha moyo wa kunisaidia lakini usije kuwa kama hawa wawili.. Manyota na Musa ambao wameamua kunisaliti na kutaka kuniua kwa kuwa walitamani kuwa na mali nyingi kutoka kwa mzee Paul ambae alinihitaji kunitumia mimi kwa faida yake, pia nikajikuta kuwa naingia kwa watu wabaya kama Salha pamoja na kundi la wauzaji wa madawa ya kulevya wa bwana Paul. hadi sasa nahisi kuwa baharini nina majanga mengi nako ndiko natarajia kupata kipato changu, pia mke wangu kachukuliwa na watu wenye ela. na sijui mwanangu anaishi vipi, tena huko kisiwani nimeishi kwa shida mpaka sasa unavyoona nafuu yangu nilikuwa na ugonjwa mkubwa sana wa kuoza tako hili ila mpaka nimepona mungu mwenyewe anajua ndugu yangu. "
Machozi yalikuwa yananitoka na Mshana akawa ananionea huruma sana ndipo akasimama na akanishika mkono tena. Akawa ananivuta huku akinilazimisha kuondoka bila hata kusema wapi tunaelekea.
"Vipi unanipeleka wapi sasa"
"Mnali nifuate mimi najua familia yako iko utaipata vipi na haya matatizo yako yataisha haraka sana".
Nilishangaa sana kusikia kwamba anataka kuniambia anajua familia yangu naipata vipi. tulikimbia kwa kuwa yeye muongozaji alikuwa anakimbia na mimi nilimfuata.
tulifika mpaka maenwo fulani ya mapori kabisa kama tunaelekea njia ya kwenda vijijini. nilisimama na kumuaomba kitu. "Mshana tunaelekea wapi lakini? ". "weee twende Mnali huku ndiko msaada wako uliko fanya haraka kaza mguu". Akiwa anasema hivyo ghafla na mimi nasikia sauti ambayo peke yangu ndio naweza kuisikia na sauti hiyo ya yule kiumbe akiwa anakimbia. alikuwa kwa mbali sana akiwa anatukimbilia na kwa kujua akitukuta hapa lazima tusage meno. nilimgeukia Mshana "mshana yule kiumbe anakujaa anatukimbilia huku tuliko namsikia.. "
"Mnaliiiiii unashangaa nini sasa tumefika tukimbieeeew asitukute bwanaaaaa.... ". Daaaaa tulikimbia kwa kasi kubwa sana mimi nikiwa sijui wapi naelekea ila Mshana ndie anafahamu.
TUKUTANE TOLEO LIJALO........
Comments
Post a Comment