RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE 28.







ENDELEA............ 
.................Ndipo pale nilipoamua kuwaambia ukweli ili yasije kutokea mapema kabla hata niliyokwenda nayo pale hayajitimia. "Jamani naombeni mnisikilize, huku tunakoelekea si kuzuri kabisa, kwa maana kuwa kuna viumbe vya ajabu sana". Walinishangaa wakati yule mwingine alishafika tayari nchi kavu na mimi nikiwa na yule mwingine tupo ndani ya maji bado. "Kwa nini unasema hivyo na viumbe gani hao wa ajabu ambao wanaweza kututishia sisi maisha". Niliona vyema kuwaeleza kwa kutumia busara kubwa ambayo ingeweza kunifanikishia mimi yale malengo yangu muhimu. "Huku kuna viumbe vya hatari sana, viumbe ambavyo vinapenda kukaa nchi kavu pekee, lakini ndani ya maji hawawezi kabisa kukanyaga". "Kwa hiyo?". Aliuliza mmoja wao. "Inachobidi tulale ndani ya maji mpaka asubuhi au laa tukae ndani ya maji hadi asubuhi ndipo tutaanza kutoka na kuwapeleka huko ambako mnataka." Walishtuka lakini ndipo wakaanza kuongea wao wenyewe. 'Sasa, moris umesikia hayo mambo?" Ndio nimesikia, lakini mimi sijawahi kutishika kabisa acha mimi nikae hapa nchi kavu siwezi kulala kwenye maji kama vipi laleni huko. Yule ambae alikuwa anajulikana kwa jina la Moris alijifanya ubishi basi akalala kwenye mchanga na sisi tukakaa kwenye maji. Usingizi haukuja kabisa kutokana na yale maji kuwa ya chumvi pia ni ya baridi. Mpaka majira ya usiku sana maji yalizidi kujaa mpaka tukashindwa kuvumilia ndipo tukakaa kwenye mchanga karibu kidogo na yale maji lengo likitokea la kutokea basi tunakimbilia kwenye maji kiurahisi. Mpaamajira ya asubuhi yanatimia kila mmoja alikuwa salama kwa kumuangalia tu kwa mbalimbali japp hatukuwa na uhakika na kila mwenzake. Niliwaingiza kwenye kijimsitu kile lengo nitokeze kwenye lile pango. Aisee kabla hata hatujazama mbali sana tayari harufu ya wale viumbe ilianza kupatikana. Moris na mwenzake walianza kushangaa sana ndipo wakaanza kujihami kwa kuchukua bastola zao pamoja na visu. Hii ni baada ya kuona mafuvu ya watu mule msituni. Oyaa ina maana huku kuna watu ambao walifika na wakashindwa kurudi?, waliniuliza. Ndio wapo wengi sana na hawakuweza kurudi kwa sababu ya ubishi wao kama wenu nyinyi. Walishangaa lakini haikuwafanya waache zile silaha. Tulitembea kwa uangalifu mkubwa sana. Mamaaaaaa!. Sauti iliyosikika nyuma yetu ilitushtua na kutufanya tugeuke wale tulioweza kugeuka laaaah! Moris hayupo kwenye upeo wa macho yetu. Hofu ilianza kutanda na mimi nilifahamu kuwa tayari wale viumbe wameanza kazi zao. Lakini wale viumbe hawana nguvu kubwa ya kuwanasa na kiwabeba watu wakubwa kama sisi. Inakuwaje hili au ni kiumbe gani huyo?. Yule jamaa alianza kuweuka pale. Moriss, moriiiiiis. Niliamua kujikokota hadi pale alipo. Ndugu moris yupo ila usitie kelele utaleta matatizo makubwa sana tofauti hata na hilo la kwanza. Ndipo tulitoka lakini akili ya yule jamaa haikuwa pale kabisa. Safari yangu iliishia kwenye lile pango ambalo ninatakiwa kuingia ndani yake. Mnali!, umetuleta huku kuwa kuna masanduku ya mali sasa yako wapi?, mbona nazidi kuona maajabu tu mwanzo mwisho?, aliniuliza yule jamaa. Nilivuta pumzi kisha nikamuangalia, nilijua kabisa ni uongo na hakuna hizo mali wanazotaka bali tamaa zao tu. Kaka mali ziko kwenye hili pango., sasa si tuingie mara moja?....hapana kaka hapa panatakiwa mimi niingie kwanza, nitengeneze mazingira ya humu ndani kisha utaweza kuingia. Una maanisha nibaki nje?, haswaaaaa. Weeeee nani kasema nimemuona moris anachukuliwa hivihivi alafu mimi uniache huku nje acha wewe. Wakati tunalumbana ndipo wale viumbe wakaingia pale tulipo, tukiwashuhudia jinsi walivyo na hawakuweza kuchelewa kabisa walimfuata yule jamaa kwa hasira kali. Jambo lililomfanya ashtuke na kuanza kukimbia ovyo mule msituni. Ajabu mimi walikuwa wananipita kama hawanijui. Hapohapo mlango wa lile pango ukafunguka. Nikaingia na lile sanduku langu hadi karibia lile eneo ambalo linapatikana kuwepo mahali pa kutolea mwanga maalumu. Kwa kuwa nilikuwa na haraka sana nikajikuta nafungua boksi kwa urahisi hali liliwashinda watu wengi sana. Nikakutana na kipande cha almasi kinachong'aa sana. Kabla sijachukua ndipo mawazo ya upande wa pili yananijia yaliyo kama ndoto hivi. "Fanya haraka sana, kuweka hilo jiwe mahali husika kabla hujazalisha milki yenye roho chafu." nilishangaa kusikia ile kauli kuwa niwahi kuweka lile jiwe mahali husika yani kabla hata sijazalisha milki yenye roho chafu.  roho chafu ipi hiyo ambayo ilikuwa inaongelewa. nilifananisha yale maongezi na yale ya kwanza kabisa ambayo siku nafika humu nilipata kuyasikia.  nilichukua lile jiwe kazi sasa ikawa natafuta lile eneo mahali pake. lakini hofu kubwa ilikuwa kutofahamu wapi ambapo wale wengine wamekwenda. nilitembea taratibutaratibu sana kwa hofu ya hali ya juu. mpaka pale ambapo niliona kuwa kuna dalili ya mwanga kutoa kama ile awamu ya kwanza kufika hapa. nilifurahi sana kwa kuhisi kuwa tayari maisha yangu yatarudi kama mwanzo na kuachana na mitihani hii ya kila siku. lakini chini nilipokuwa nakanyaga kulikuwa na miili ya viumbe vingi ambavyo vilikuwa vinatoa harufu nzito yenye kunuka sana kiasi kwamba nikawa nashindwa hata kupumua vyema kama awali nilipoingia.  kadri muda ulivyozidi kusonga ndipo harufu kali ilizidi kuenea mule ndani.  lakini nashukuru sana kutokana na ujasiri nilionao na maisha magumu niliyonayo nilijitahidi kuvumilia sana hadi kuifikia na kuanza kulinganisha lile jiwe hadi yale maeneo.  nilipofanikiwa kuliweka nilisikia kama kitu kinagonga masikioni mwangu yani ukelele mkubwa sana. ukelele huo sikufahamu ulikuwa na maana gani ndipo niliporudi kinyumenyume hadi pale ambapo palikuwa na lile sanduku langu lakini kila nikipapasa nashindwa kulifikia kutokana na mitetemo niliyonayo kwenye mwili wangu.  ghafla bin vuuup! lile eneo lilitoa mwanga wa kila aina kisha kama kitu kinajifunga hivi alafu makelele ya makofi na vifijo vikirindima.  hapo ndipo nikasikia kama watu wanaongea huko nje ya pango.  nikaanza kutoka taratibu taratibu hadi nje lakino sikupata kusikia zile kelele.  jambo lingine la ajavu ni pale nguvu nilipozikosa hata za kusimama maana nilianza kulegea kama mlenda,  viungo vyangu havifanyi kazi kabisa na nikawa mbele sioni vizuri mpaka pale nilipopatwa na usingizi mzito. nakumbuka nilikuja kuzinduka toka usingizi baada ya kutoka kwenye ndoto kali ambayo ilikuwa inahusiana na kuonana na yule jamaa ambae mwanzo alinichukuaga na kunitibia. aliniambia kuwa hongera sana kwani umefanikisha lengo letu ndani ya kisiwa hiki kufukuza hawa viumbe ambao walikishikilia kwa muda mrefu sana.  lakini tatizo ni moja ambalo umezalisha. tatizo lenyewe kuwa bado ndugu zako watapata tabu sana kwa.... " hapo ndipo nikaamka toka kwenye njozi hiyo.  nikasimama niko kamili kabisa alafu nipo ufukweni nani kanileta sifahamu.  niliamua kuita mmoja mmoja kati ya wale wawili ambao walipotea mbele yangu kila mmoja.  japo nia yangu ni kuwaonyesha lakini huruma kama mwanadamu ilinijia. nilianza kuwatafuta. kwa bahati nzuri kwa mbali namuona morisi ambae alikuwa kasimama ananiangalia akiwa kwa mbali. kila nilipojitahidi kumfuata alizidi kuingia msituni.  nilikaribia pale ghafla nilipigwa kofi takatifu la nyuma ya kichwa mpaka nikazunguka kama mara mbili hivi na kudondoka chini.  nilishindwa kujifahamu vyema maana netweki ilikata kabiasa. mala ghafla niliona kitu kinanipita nyuma yangu kwa kasi sana hata sikupata hata nafasi ya kujua ni kitu gani. ndipo niliona mambo si mambo baada ya kona mauzauza yanazidi nilikimbia hadi kwenye maji lakini hapakuwa na hata mtumbwi wala mtu ambae yupo karibu anaweza kunisaidia.  kelele za kutisha zilianza kwenye kile kisiwa mpaka miti ikaanza kutikisika kama mtu anaitikisa.  sauti zenye kupishana zilizoambatana na mwangwi mzito sana.  hofu yangu ilitanda baada ya kuhisi kuwa kuna mnyama au mtu anakuja karibu yangu lakini haonekani ila hatua zake kwenye mchanga naziona kama anatembea anakuja mbele yangu.  sikujua ni nini kwa kweli... hahaaaaa haaaaah! ziliendelea kusikia huku zikizunguka karibu yangu alafu mngurumo mkubwa sana.  jasho lilinitoka huku nikiomba mungu anisaidie kuushinda mtihani huu.  nikiwa kwenye maji pale kwenye mchanga naona kabisa nyayo zinazunguka ila wenyewe hawaonekani. nilijiangalia kwenye sehemu yangu ambayo nilipata tatizo halikuwepo kabisa. ilipita dakika kadhaa ukimya ulitawala kumbe kuna mtumbwi kwa mbali unakuja.  nilipiga kelele ili aje kunisaidia nilishukuru kuwa alinisikia ndipo nikafanikiwa kupanda na kumuomba afanye haraka sana kutoka yale maeneo.  lakini ajabu zaidi ni pale tupo mbali na ufukwe wa kile kisiwa tukiwa ndani ya mtumbwi ule sauti ilijitokeza ya mngurumo mkubwa kama ule wa awali.  nikajiuliza nausikia mimi tu au wote.  nilimuuliza na yeye alikuwa hafahamu wala hata kusikia hakusikia.  moyo wangu uliishiwa nguvu baada ya kuhisi lile jambo.  mpaka tunashuka kwenye ufukwe ule ambao nilikuwa nautumia zamani na akina manyota.  sauti ilikuwa karibu na mimi. watu walionifahamu walikuja karibu na kunishangaa lakini ajabu pale mmoja wao alipotaka kunishika kwa mshangao alio nao lakini alisukumwa na kitu asichokijua na hata mimi nilikuwa sikifahamu. 

JE?  BASHIRI NI NINI HIKO.  KUJUA HILO TUKUTANE TOLEO LIJALO 

Comments

Popular posts from this blog

SMS 47 ZA MAPENZI ZITAKAZO MNYEGEZA** MPENZI WAKO

KWANINI WADADA WENGI WAREMBO NA WANAOJIONA WAREMBO HUCHELEWA KUOLEWA,HUKOSEA KUOLEWA AU KUTOOLEWA KABISA?SOMA HAPA

HATUA ZA KUCHEZEA KIHARAGE NA KISIMI