RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA 27







ENDELEA....... 

.. 
... 
.... 
..... 
......Baada ya kuhakikisha kuwa nimeitupa ile simu hapo ndipo shughuli mpya ilipoanza. Mguu wangu uliniuma sana mpaka kiuno kikawa kinanibana kisawasawa. Ilifikia hali kuwa hata natamani yale maeneo yakatwe nibaki na kidonda kipya ambacho kinaweza kutibika kuliko hii hali. 
Nilikaa takribani masaa kadhaa ambayo yalinifanya niwaze kuwa wale watu hawawezi kurudi tena. Kutokana na hilo nilijikokota na kusimama taratibu ili niangaze kule ambako waliingilia. Nilihisi kuwa ndio wamenitelekeza pale au vijana wa mjini wanasema wameniacha mataa. jambo kubwa zaidi ni wao kutowamini hali ya kutowafahamu. Muda ulivyozidi kusonga ndipo hali yangu na mimi ilizidi kuniwia ngumu sana. Lakini nilijikaza ili nifikie lengo langu. Maisha yangu yamekuwa magumu pia yenye kupitia misukosuko ya kila siku tangu nimeanza hadi sasa, na sijui lini nitapata faraja ambayo itanifanya nijihisi huru kama pale awali. 
Kwa mbali ndipo nililiona gari likija yale maeneo nilijikokota hadi pembezoni kabisa na kujificha ili nipate uhakika wa kusema wale ni akina nani. Gari lile lilisogea hadi maeneo yaleyale ambayo mwanzo lilikuwepo la mwanzo. 
Alishuka yule jamaa wa kwanza akiwa na yule mwingine. Hapo ndipo niliponyanyuka na kuwasogelea. 
"Wee jamaa vipi?". 
Waliniuliza. 
"Safi tu nilikuwa pale kuwasubiri". 
Mmoja wao akarudi ndani ya gari kisha yule mwingine akanifuata. 
"Sikia tumefanikisha jambo moja kati ya yale mawili ambayo umetuomba kufanya." 
Hadi pale kusikia ile kauli nikashukuru sana japo si kwa ishara ila moyo wangu ulijawa na amani kubwa tena ya kipekee sana. 
"Jambo gani ambalo mmefanikisha?" 
Niliwauliza. 
"Tumepata lile sanduku tayari", kuhusu hiyo familia yako tutaendelea kuifuatilia japo nasikia iko mikononi mwa Salha yule mwanamke ambae nilikuambia uwe nae makini". 
Nilishtuka sana. 
"Ina maana Salha alifanya kweli kuiteka familia yangu?". 
"Sas sikia lengo hapa sisi kufika huko ambako umesema kuna mali nyingi....pia mbona hili sanduku lako halifunguki ebu fungua tuone". 
Walinikabidhi ili nipate kulifungua. 
"Mh! Jamani siwafichi tangu hili niwe nalo sijawahi kulifungua ila huko papo mahali sahihi pa kuweza kufungua hili dude". 
Waliniangalia kana kwamba hawaniamini, ila ukweli sikuwahi kulifungua kabisa. Ilipita kama dakika saba tukiwa tunazungumza. Waliniahidi kuwa watanihakikishia familia yangu itarudi salama lakini pindi tu nikiwapeleka kule kisiwani. 
"Tunachohitaji hapa wewe kutupeleka huko kisiwani na maswala ya familia yako tutahakikisha inakua salama kwani huko pia tumemuacha mtu ambae anashughulikia upatikanaji wa mtoto wako". 
Waliniambia. 
"Lakini mimi hali yangu sio nzuri maana nashindwa hata kutembea". 
"Kwa nn unashindwa kutembea?" 
Nilisimama kisha nikafungua suruali yangu ili niwaonyeshe. 
"Unataka kufanya nini?" 
"Ngojeni niwaonyeshe". 
Nilifungua kisha niwaonyesha jinsi gani upande wa tako langu lilivyoharibika. 
"Oooh! Pole ilikuwaje nini tatizo.?" 
Nilijifikiria sana nikiwaambia ukweli kuhusu kule tunakotaka kwenda hawatoniamini au laa wataghaili na leengo langu niwaonyeshe adabu hawa wapuuzi. 
"Mambo ya maisha haya kuhangaika nikajikuta nimekali kitu hatari sana ambacho kimenidhuru". 
Niliamua kuwaongopea. 
"Sasa tunachukua chakula kwenye gari kisha tunakula baada ya kumaliza tunakodisha mtumbwi sisi na wewe hadi huko kisiwani sawa?". 
"Sawa..." 
Kweli chakula kililetwa pale mboga ilikuwa nyama ya ng'ombe ambayo wamenunua tokea mjini huko.
Kile chakula kilinishinda kabisa kula yani kwangu kilikuwa kama shubiri. Ile nyama ilinifanya nijihisi vibaya kisha niamshe hisia za mwili zilizolala. 
Niliacha kula kabisa japo walinishangaa. Si kwamba njaa sikuwa nayo hapana ila kutokana ile hali ilinifanya nihisi kuwa kama nakula shubiri ambayo hata nikibugia kilo ya sukari hakuna kinachofaa. 
"Nimeshashiba tayari". 
Baada ya kumaliza ndipo nikalala mule ndani ya gari lao nikisubiri nini kinaendelea. Sasa inabidi tutafute mvuvi yeyote kule mbali ambae atatusaidia kutuvusha hadi huko tunakokwenda. Hapo ndipo akatafutwa mvuvi. Kwangu ilikuwa rahisi sana kuwajua vijana wa pale ambao wanajihusisha na masuala ya uvuvi kwa kuwa nimeishi nao kwa muda mrefu sana kipindi ambacho mimi mwenyewe nilikuwa bingwa wa kuvua samaki. 
Aliletwa kijana mmoja hivi wa makamo. Wakaelewana nae kisha tukapanda katika chombo chake kwa ajili ya kuanza safari. Niliwekwa nyuma kabisa kule ambako nahodha wa chombo kile alikuwa anakiongoza, pembeni walijipanga wale jamaa wakiwa wamevaa makoti yao meusi. 
Moyoni mwangu nilijua kuwa mambo yanayokwenda kutokea huku ni mazito japo hawa jamaa hawajui lakini lengo niwakomeshe tu. Lengo langu lingine ni kutimiza kwenda kupeleka hili sanduku hadi kule ambako panatakiwa. 
Ninachokumbuka siku ile naanza kuingia ndani ya kisiwa kile nilikutana na jamaa ambae alinipatia hili sanduku na akaniambia kuwa ipo siku maisha yangu yatakuwa magumu na hili likawa msaada wangu mkubwa sana. Pia nilipata kuota ndoto nyingine inayofanana na hii kuwa nijitahidi kufanikisha lile ambalo wale vibwengo au viumbe wa ajabu wanaamini kuwa naweza kuwasaidia na hatimae leo nimepata lile sanduku nilupeleke sehemu husika na mimi maisha yangu yarudi kama awali. 
Mwendo huo ulizidi kuyoyoma na kiza kilianza kuingia. Ndani ya chombo wote tulikuwa kimya kabisa kila mooja akifikiria kule aendako kutakuwa salama au laa. Peke yangu ndio nilikuwa najua ugumu, urahisi wa kufika huko na changamoto zote ambazo tunaweza kukutananazo. Taa iliwashwa ili mwanga upatikane kutokana na kiza ndani ya bahari hiyo. 
Yule kijana aliniuliza. 
"Kaka nimepiga kasia mpaka mikono inaniuma hiko kisiwa kiko wapi?..maana tangu nianze kazi ya uvuvi sijawahi kusikia kama kuna kisiwa huku". 
Aliniuliza swali gumu sana amblo hata mimi nilishindwa kumjibu kwa wakati. Ndipo wale wengine wakaingilia. 
"Ina maana kijana huku hakuna kisiwa kabisa?" 
"Ndio...hakuna huku". 
"Oyaa Mnali unatuuza si ndio?" 
Waliniangalia huku wakinitwanga maswali. 
"Nyie sikieni huyu kijana ni mgeni kwenye hii bahari mimi ndio nafahamu nimekutana....eheee tena kileeeee mbele". 
Nilifurahi baada ya kuona kisiwa kinaonekana. Kile kisiwa ni cha maajabu sana muda kinaonekana ila muda mwingine hakionekani. Basi wakaniamini na muda si mrefu sana tulikaribia. 
Upepo uliovuma sana ulifanya taa kuzima kabisa na tukawa hatuoni. Tulipokaribia tulikanyaga maji ambayo yalitufikia kwenye vifua vyetu ila yule kijana akarudi hakutaka kubaki. 
"Jamani mimi nawaacha huku siwezi kubaki maana hakuna hata kisiwa nilichowahi kusikia kipo". 
Ndipo akatuacha sisi tukimaliza yale maji hadi ufukwe wa kile kisiwa. 
Nilikumbuka kuwa wale viumbe wapo kila mahali na dawa yao ni kuwa ndani ya maji kwani hawajawahi gusa maji ndio kinga pekee. Sasa tukilala kwenye mchanga lazima watulambe cha umuhimu kulala ndani ya maji. 
Nilijiuliza nikiwaambia watakubali au wataniamini?....... 

JE? WATAKUBALI KULALA NDANI YA MAJI. 

TUKUTANE TOLEO LIJALO 

Comments

Popular posts from this blog

SMS 47 ZA MAPENZI ZITAKAZO MNYEGEZA** MPENZI WAKO

KWANINI WADADA WENGI WAREMBO NA WANAOJIONA WAREMBO HUCHELEWA KUOLEWA,HUKOSEA KUOLEWA AU KUTOOLEWA KABISA?SOMA HAPA

HATUA ZA KUCHEZEA KIHARAGE NA KISIMI