RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA THELATHINI 30







ENDELEA....... 
................Nakumbuka ilikuwa siku ambayo nilipanga niende kuanza rasmi kazi ya uvuvi tena ili niweze kupata kiasi ambacho kitanisaidia kutafuta familia yangu. Lakini asubuhi hiyo wakati naelekea pwani niliwaona watu wakikimbilia maeneo hayo. Nilishikwa na mshangao ikabidi na mimi niwahi kujua kuna jambo gani. Nilipata kumuuliza mmoja wa wale wanaoelekea huko. Ndugu habari yako..Salama vipi?, eti huko kuna jambo gani mbona watu wengi wanakimbilia huko?. Haah! Ndugu kuna watu watatu wamekufa wamekutwa nchi kavi wamekufa ila kilichowauwa hakifahamiki. Mh nilishtuka sana. Tulifuatana njianibkuelekea huko. Ghafla ile sauti ya mngurumo karibu yangu ikanijia naisikia sana inanguruma, ilinichukiza sana na hadi ikanifanya safari yangu iwe nzito. Nilimuambia yule jamaa basi atangulie tu. "Ndugu basi wewe tangulia tu nitakukuta, vipi kuna shida, hapana ila nenda tu basi. Nilimuacha aende ili yasije kutokea mengine tena. Tulipofika kule kweli tuliwakuta polisi wakiwa wamezunguka na kulinda mazingira yale. Nilichoshukuru baadhi ya watu wengi walielewa mustakabari wa maisha yangu hivyo wengi wao hawakuwa wabishi sana kunielewa. Alitokea askari mmoja na kutangaza kuwa kuanzia muda ule hakuna shughuli yeyote ya uvuvi inayotakiwa kufanyika mpaka pale watakapohakikisha usalama upo. Baadhi ya watu kama sisi tunaotegemea maisha yetu baharini tuliona kazi nzito kwani vipato vyetu vinapatikana humo. Nikiwa naanda nyavu zangu na mtumbwi wa kuazima kwa ajili ya kazi yangu ya jioni. Nikiwa kwenye hatua ya kumalizia nashtushwa na kicheko cha mtu akiwa mbele yangu. Hakuwa mwingine bali ni bwana Manyota. ..haaahaa!.. aaaaaah! Aisee maisha kweli yanabadilika...wewe hujafa mpaka sasa". Nilimuangalia na kujua kuwa huyu alihitaji mimi nife. Kwa nini ulihitaji nife?....kwa sababu kuwepo kwako kuna madhara sana kwetu na hili nitalishughulikia mpaka unazama chini ya ardhi kama nduguyo kibona...". Nilimuangalia kwa jazba sana. Jamani nimewaacha muishi mtakavyo ili nipate muda na nafasi ya kuja kuishi na amani kama ya mwanzo, maisha magumu niliyopitia leo hii sitaki niyakumbuke kupitia wewe. Alicheka sana. Sawa mnali ila kumbuka kuwa huna uwezo tena wa kuchukua samaki wengi kama mwanzo na wakakusifia huna huo uwezo kabisa. Nilimuitikia kwa kumuambia kuwa ndio sina ila pale nafanya ili nipate hata ya mboga ingawa polisi wamekataza kuvua samaki. Manyota alionyesha kunipinga sana kwa kuwa maisha yake ni mazuri sana tofauti na mimi. Niliona kubishana na huyu ni tatizo niliondoka na kuhifadhi zile nyavu kwenye ule mtumbwi na kuelekea mbali kidogo mala ghafla askari wakauona ule mtumbwi na kuuvamia kutaka kuuchima moto. Nilikimbilia hadi pale. Jambo ambalo nilianza kupewa kipigo kwa kosa la kutaka kuvua. Sisi tumekataza kuvua samaki kutokana na haya matatizo wewe unajiandaa kwenda kuvua pumbavu, nilimuambia askari kuwa kunipiga si ndio kutanipatia shida yangu mimi niliyejia pale hapana ila shida yangu ni kufanikisha kile ambacho nakihitaji. Mpaka maijra fulani hivi waliniacha nifanye kile ambacho nakitaka basi na mimi sikuwa na ajizi 
Baada ya kupata nafasi ile sikutaka kuchelewa kabisa ndipo nilielekea kule ambako upo mtumbwi wangu kisha nikauweka tayari kwa kazi husika. Kwa kuwa ilikuwa ni jioni basi nilielekea sehemu zile wanazouza samaki wa kuchomwa na mafuta nilwakuta akina mama wengi ambao wananifaha kuwa mimi ni mtabe kwenye mambo yale ya uvuvi. Baadhi waliniuliza lini naanza kazi ya uvuvi. Niliona ndio nafasi pekee ya mimi kukamata ela. Nilichukua oda pamoja na kukusanya ela za kotosha nikiwa na imani kuwa narudi na mzigo wa kutosha. Hapo nilikamata kama laki na kitu nilielekea kwa Mshana ambae nilimkabidhi kama kuhifadhi wakati mimi naelekea ndani ya maji. majira ya usiku tayari nilielekea na kuanza safari ya kuingia ndani ya maji. Nilifurahi kuona napata kile ambacho nakitafuta kwani mpaka narudi samaki walikuwa wengi ila nikiwa ndani ya maji kufika ufukweni nahisi kama kitu cha harufu ya samaki yani damu yake. Alafu kama kuna kitu kinakula nyuma yangu. Nakuja kutahamaki ile sauti iliyozidi kunguruma ikiwa na mimi inatafuna samaki wangu wote. Nilishindwa kuamini kama kweli naona damu zinatapakaa tu hakuna hata samaki wale wakubwa niliowaamini napata fedha za kutosha, hakika nilichukizwa sana. Sikuwa na jinsi alfajiri wale wahusika niliwapa japo hawakufurahia na kile ambacho walikiona ila waliniheshimu tu. Na mimi nikaondoka hadi kwa mshana nikamueleza kila kitu. "Mnali, inabidi tuende kwa mganga ili ukatibiwe siku hilo dude likikosa chakula litakukula wewe". Hakika maelezo yake yalinijaza imani ya kuwa kweli inawezekana ikawa vile asemavyo Mshana. Mchana huohuo taarifa kuwa baharini wameonekana viumbe viwili vya ajabu na wamesababisha mauaji kwa watu wawili kisha wakatokomea. Sasa baharini kumechafuka hakuna siku ambayo hakuna taarifa kama hizi. Tukiwa tumepumzika sauti ya gari ilisikika ikipiga breki tulichungulia mlangoni hatukuwafahamu watu ambao walishuka na kuhitaji kuingia ndani. Tulitoka nilishangaa kuwaona Salha na bwana paul wakiwa na Manyota na musa. Nilimnong'oneza Mshana kuwa aingie ndani haraka, alifanya hivyo. Walihitaji wanibebe ila nilikataa jambo hilo liliwafanya Manyota na musa kupata vipigo wasivyovitegemea kutoka kwa mtu asiejulikana na kuwafanya wawe hoi na kukimbizana na kuondoka. Mr Paul alibaki na mshangao maana  vipigo walivyopigwa si vya kitoto. Damu ziliwadondoka, mimi pekee ndio nilikuwa nafahamu nini kimewadhibu vile. Nilimuita Mshana huku nikimuambia kwa sauti kuwa tuelekee kule kwa mganga. Aise tulipigwa wote mimi na Mshana na nusura yetu tulipoingia ndani daa! Nifanye nini kuondokana na haya?. 

TUKUTANE TOLEO LIJALO 

Comments

Popular posts from this blog

SMS 47 ZA MAPENZI ZITAKAZO MNYEGEZA** MPENZI WAKO

KWANINI WADADA WENGI WAREMBO NA WANAOJIONA WAREMBO HUCHELEWA KUOLEWA,HUKOSEA KUOLEWA AU KUTOOLEWA KABISA?SOMA HAPA

HATUA ZA KUCHEZEA KIHARAGE NA KISIMI