RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO 25






ENDELEA............ 
................. 
................ 
Basi ndipo Salha akaingia ndani ya gari kisha akafunga mlango wa gari yake na kuondoka yale maeneo. Nikiwa nazidi kuwaza hali yangu ya maisha niliyonayo ndipo nikagundua kuwa hata matajiri hawana furaha kwa hali hii. Kama mimi mwenye maisha magumu naishi kwa raha lakini kwa hatua chache ya kushuhudia maish ya wale walioendelea naona kabisa wanapata tabu. 
Gari lilifika hadi kwenye nyumba yake na mlinzi akafungua geti haraka sana na sisi tukapata kuingia. Akili ya Salha ililala sana kwenye mapenzi tofauti na mimi mawazo yangu aliniangalia kwa jicho la mahaba lakini mimi nilimkata jicho tu. Sikutaka kumuonyeshea moja kwa moja kuwa nimemkubalia ndio maana nilikaza baadhi ya sehemu kama hizo ambazo yeye alizifanya. 
Alinishika mkono tukaelekea ndani baada ya kufungua mlango wake. Nilifika nikatulia kwenye kochi pale sebuleni kisha nikajishika kichwa changu huku nikitazama jinsi Mzungu alivyotengeneza taa na ikawa inatoa mwanga mzuri na ukatusaidia kuangaza vitu vingi kwa sehemu mbalimbali. 
Niliwaza maisha ya kule Kisiwani, nilijiuliza vipi nirudi au niachane nayo. Kwa sababu nilijihisi kama nimepona hivi. Ila nikaachana na hayo mawazo ambayo yangenifanya niruke wazimu mule ndani kwa kuumwa na kichwa. Ndipo namuona Salha anarejea na chupa kimoja hivi, alikuja nacho hadi pale mezani na kutoa glass mbili. 
"Ehee! Beby unatumia hiki kinywaji?" 
"Kinywaji gani?" 
Nilimuuliza 
"Heeee hujui kama hii ni pombee." 
Nilishtuka Pombe na mimi wapi na wapi. 
"Hapana situmii hiyo labda soda". 
"Acha Ushamba baby ebuu onja kwanza". 
Nilishindwa kumuelewa kwa mapema sana japo wasiwasi uliniingia pale tu nilipoambiwa Be care 
"Hapana Salha wee kunywa tu mimi sijawahi kutumia kabisa na sihitaji kutumia". 
Lakini alimimina ile pombe kwenye moja ya glass pale mezani, kisha akaanza kuniangalia. Nilimkazia uso ili kumuonyesha msisitizo kuwa situmii vitu kama vile. Mwanamke alitumia uwezo wake kama mwanamke akaanza kulegeza macho kama kameza kungu manga. Aliigiza kulewa macho hata kabla hajanywa bado aisee. 
Nilipata tabu sana kuepukana na shetani yule wa pombe lakini kwa bahati mbaya mfuasi wake alikuwa na vigezo vyote vya kushinda. Alisimama kisha ndipo akavua nguo zake zote na kubaki mtupu. Binafsi moyo ulidunda akanijia hadi pale nilipoketi, alizidi kuteka akili yangu na kumuacha afanye kila kitu anachokitaka. 
"Baby si nimekuambia kuwa nakupenda". 
"Ndio" 
"Shida yako nini?" 
"Hakuna" 
"Haya onja ili wote tuwe kwenye ulimwengu mmoja" 
"Ila..." 
"Nooo! Hakuna ila onja bhana". 
"Haya". 
Nilipiga glass moja mpaka macho nikahisi yanataka kuchomoka. 
"Hiyoo inaitwa Wisk honey" 
"Oooh! Shalha hata mimi naiona hii". 
.....Asubuhi na mapema nashtuka nikiwa kama nilivyozaliwa tena nipo kitandani. Kichwa changu kiliniuma sana. 
Nilikumbuka kuwa ni zile pombe za jana lakini hali yangu si nzuri siwezi hata kusimama. Mwili mchovu kama nimepigwapigwa, mikono yangu iliishiwa nguvu siwezi hata kuinua na kuipandisha. 
Mdomo wangu pia mzito kusema kwa sauti kali ambayo kama kuna mtu anaweza kunisikia. Nilijishangaa kuona ile hali kuwa ni mbaya sana. 
Nilijitahidi kuinua sauti na kumuita Salha lakini hakuwa karibu, nilijitutumua na kufanikiwa kukaa. Wakati natafakari lipi limetokea simu pale kitandani inanguruma, nilitafuta nilipoipata ilikuwa ni ya Salha aliiacha. Nilijiuliza Salha kaenda wapi basi atakuwa hayuko mbali kwa kuwa simu kaacha. 
Niliangalia ni meseji kutoka kwa bwana Pooo. 
"Mh! Hivi hii namba si jana niliiona kwenye ile simu kubwa leo ipo tena kwenye simu ndogo ngoja." 
Nilifungua kwa kuwa haikuwa na pini yoyote. Nakutana na ujumbe ulioandikwa kwa herufi kubwa kuonyesha msisitizo. (SALHA! HAKIKISHA UNAMALIZA KAZI ASUBUHI YA LEO.) 
"Eboooo! Hakikisha unamaliza kazi asubuhi ya leo?..ahaaa kazi gani ambayo kaambiwa amalize..labda wafanya biashara hawa. Lakini yuko wapi?". 
Niliikariri ile namba harakaharaka kisha nikaacha simu pale ilipokawepo mwanzo. Nililala tena huku nikiugulia maumivu yangu. Nilijiuliza sawa kama ndio mara yangu ya kwanza kunywa pombe lakini si kwa maumivu haya, na kama wote wanaokunywa pombe wanapitia haya maumivu wanakazi na ndio maana kumbe pombe haramu. 
Mengi niliongea lakini jambo la kizani niliekwenye mwanga nitazidi kubashiri lakini hakuna uhalisia kabisa. Muda unaenda lakini Salha haonekani ndipo nilipojiondoa japo kwa kibishi hivyohivyo hadi kusimama pale sakafuni. 
Nilitafuta Nguo zangu sikifanikiwa kuziona kabisa. Hapo ndipo nilizidi kuchanganyikiwa zaidi. "Huyu kaenda wapi?". 
Nilichukua taulo nikajifunga kisha nikataka kufungua mlango ili nitoke Mngurumo wa simu ile ndogo uliingia tena. Nikataka kudharau ila nikachukua simu na kuangalia ilikuwa ni meseji. "TUNAKUJA SASA HIVI HAPO KWAKO". 
"Mh" 
"Nilishtuka! Nikaona kumbee hili swala lawezekana linanihusu...je? Yule jamaa kule kwenye kampuni ya uzoaji taka aliniambia Be care yani niwe makini na huyu mwanamke". 
Pumbavu sina muda wa kupoteza nilienda hadi bafuni huku nikichechemea kwa kuwa mguu wangu sehemu za tako zinauma. 
Sikuwa naangalia nini kinanisibu nilipofika bafuni nikajisafisha vyema japo mwili unauma sana, niliporejea ndipo nikaona beseni ambalo limelowekwa Nguo zangu. 
"Aisee! Kweli niwe makini na huyu mdada". 
Nilikusanya zile nguo toka kwenye maji nikazivaa kama zilivyo japo zimelowa, nikaingia chumbani na kuchukua ile simu ya Salha. Nilikubali kufanya uhalifu mule ndani kwa ajili nijisaidie ili nisije patwa na madhara. Taratibu nikafungua baadhi ya vitu mule ndani na moja ya sanduku nikakutana na Kipande kimoja kidogo cha Almasi. 
"Mh! Huyu mwanamke ni tajiri sana kumbe anamiliki Almasi kama hii". 
Niliachana nayo mpaka pale nilipopata kiasi cha fedha ambazo zingenisaidia katika mihangaiko yangu. Nikiwa nachechemea nilijiangalia na kuona pale ambapo wale wanyama walinibana panatoa funza yani wadudu kabisa hivi. 
Nilizidi kuchanganyikiwa sijui lipi nifanye kutoka mule ndani. Lakini nilifanikiwa kutoka nje hadi kwa mlinzi ambae alisimama katikati ya geti na kunitazama. 
"Habari za asubuhi kiongozi". 
"Salama mheshimiwa sema". 
"Sawa naomba unifungulie geti mara moja kuna mahali naeleke". 
"Haaah! Hahaaaa! Hahaaaaa!" 
Mlinzi aliangua cheko. 
"Kwa nini unacheka" 
Nilimuuliza 
"Kwa sababu unanichekesha. Sijapewa ruksa ya wewe kutoka humo ndani, ila nimepewa ruksa ya kutokukuruhusu wewe kupita hapa getini". 
"Daaah! Sasa kaka kama hukupewa ruksa ya mimi kupita hapa getini limewekwa kwa ajili gani sasa tutawezaje kuruka ukuta". 
"Nisikie braza nipo kazini hutotoka nje nenda ndani haraka". 
Ndipo simu inaita. 
Niliiweka sikioni na kuwasikiliza. 
"Helloo! Salha hakikisha huyu kijana hatoki ndani, pia mpige sindano nyingine tunakuja sasa hivi". 
Sikujibu chochote. 
Mwili ulipandwa na hasira lakini ni zile hasira zangu za kawaida lakini maumivu yangu yalizidi maradufu na wadudu nikiendelea kuhisi wanatoka na kudondoka chini tako langu lilioza kabisa alafu mlinzi ananipa kiwingu pale. 
"Kaka! Mimi ni mwanaume mwenzako matatizo niliyonayo mimi nahisi ungeyajua usingefanya hivo". 
"Una matatizo gani wewe wakati unaishi na wanawake wenye vyao kama hao mimi ndio nina shida nalala nje kuwalinda nyinyi ndio nimekuambia kuwa hapa hutoki mpaka Salha arudi". 
"Poa Salha yuko wapi?" 
"Sijui". 
"Basi naomba dakika moja nikuonyeshe tatizo nililonalo". 
Nilivua ile suruali wakati inavuja maji nikageuka nyuma na kumuonyesha jinsi funza wanavyopikitapikita na wengine kudondoka. 
"Kaka unaponichelewesha, nazidi kuumia nataka niende hospitali haraka kaka". 
Ndipo nilipomuona kanywea kabisa pale. 
"Daah! Kaka pole ilikuaje". 
"Huu si muda wa kukuhadithia ila ni muda pekee wa wewe kunifungulia na kutoka nje niende hospitali nirudi kisha nakuhadithia kila kitu.". 
Jamaa anafungua geti na haraka nachechemea kwa kuruka mguu mmoja hadi nje nikashukuru sana. Ghafla gari linakuja kwa kasi ya ajabu kuja pale nilipo. Ndipo breki kali ikapigwa karibu na pale nilipo kitendo kilichonifanya nidondoke chini na kushikilia mikono yangu nyuma nikitafakari nani ambae kaja na analengo gani na mimi. 

TUKUTANE TOLEO LIJALO 

Comments

Popular posts from this blog

SMS 47 ZA MAPENZI ZITAKAZO MNYEGEZA** MPENZI WAKO

KWANINI WADADA WENGI WAREMBO NA WANAOJIONA WAREMBO HUCHELEWA KUOLEWA,HUKOSEA KUOLEWA AU KUTOOLEWA KABISA?SOMA HAPA

HATUA ZA KUCHEZEA KIHARAGE NA KISIMI