RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA 26





...... 
.................Ule uharaka wa lile gari ulinifanya niweweseke na bila hata kutambua kinachoendelea. Mlinzi ambae alikuwa kwenye nyumba ile ya salha alishtuka kwa haraka sana akataka kufungua mlango ajue nini kinaendelea. 
Lakini alitokea jamaa mmoja ambae sikuweza kumfahamu vyema kutoka kwenye lile gari lake na kuninyanyua fasta kwa haraka sana hadi kwenye gari na kufunga mlango na yeye kuingia upande wake. Nikiwa mule ndani nilifungwa pingu mikononi hadi miguuni pia jamaa yule maana walikuwa wawili wakanifunga mdomo, safari ya gari lilikwenda huku nikizidi kutapatapa maumivu ya mguu wangu, pia sikuwa nafahamu wale akina nani, safari iliiva hadi ufukweni kabisa wa bahari ndipo waliponishusha. 
Nilikuwa nachechemea kutokana na mguu wangu kuharibika sana. Yule dereva alifungua mask yake usoni na nikapata kumuona sura yake ila kadri nilivyojitahidi kuvuta taswira ilizidi kukataa kutokana sikuwa namfahamu kabisa. 
"Kijana samahani kwanza kwa hili tendo ambalo tumekufanyia muda mfupi.." 
Nilishangaa ananiomba msamaha. 
"Sasa mnahitaji nini kwa mimi masikini". Akili yangu ilizama kwenye ile simu ndogo ya salha yenye jumbe mbili nilizozishuhudia kwa macho yangu nikasoma hapo ndipo nikahisi kuwa hawa ndio wale watu ambao walikuwa wanawasiliana na Salha. 
"Sisi hatukuitaji wewe ila mimi ninahitaji roho yako iendelee kuhema kama wengine." 
"Mh! Nyinyi si wale watu mliokuwa mnawasiliana na Salha kuwa mnamuambia ahakikishe namalizwa mapema sana." 
Niliona wakishangaa ndipo yule dereva akanijia na kunishika bega. 
"Kijana acha hizo fikra kabisa, unakumbuka neno hili nikikuambia?.." 
"Neno gani..?" 
"Be care!" 
Nilivuta taswira nikakumbuka kuwa neno hili nilishaambiwaga na jamaa fulani. Wakati mimi na Salha tunaelekea kule kampuni ya uzoaji taka.nikaambiwa niwe makini na Salha. 
"Wewe ni nani?".......... 
"Hupaswi kuniuliza mimi nina?...bali ninachohitaji kukusaidia na mimi unisaidie sawa..!" 
Nia yao ilikuwa mimi kunisaidia japo sikufahamu ni msaada gani ambao wanataka japo mimi tayari wamenitoa kwenye kile kisanga cha hatari. 
"Sasa nimefuatilia kwa makini kuwa lile sanduku bado lipo tena kwenye ileile kampuni ambayo ile usiku mlinikuta kama mlinzi...lakini kwa utafiti ambao wameuchunguza kuwa lile sanfuku halifunguki hata kwa njia gani, pia ni sanduku la kale sana tunachohitaji mguu wako mguu wetu hadi kwenye ile kampuni, tumeshafanya mchakato kuwa wapi tunaifikia maana inaonekana wewe ndio muhusika wa lile huo ndio msaada tunaohitaji." 
Nilivuta pumzi ndefu yenye faraja la matumaini ila hapa nikahitaji niwachezee akili kidogo. 
"Jamani sikilizeni kwanza...nawashukuru sana kwa kunifikisha hapa maana nilishakuwa marehemu..pia nafurahi kupata ujumbe wa uwepo wa Sanduku langu.." 
"Wee Sanduku letu lako wapi yako maisha..." 
Mh nilishtuka. 
"Haya sanduku lenu.." 
Lakini nina ombi mambo mawili. Hapo nilitulia na nikawa nawaangalia kwanza muitikio wao. 
"Yapi hayo..?" 
"Jamani mimi siwafichi maisha yangu magumu hadi sasa" 
"Ongea muda unakwenda" 
"Nina muda mrefu sana sijafanikiwa kumuona mtoto wangu Asante pamoja na mke wangu pia mnisaidie kuwaona hao viumbe pia mnipatie hilo sanduku mimi ninawapeleka ambako hayo masanduku yanapatikana kuna kama matatu makubwa sana ambayo nilishindwa hata kusukuma na inasemeka kuna vito vya thamani humo". 
Waliangaliana wale wawili. 
"Mh! Inaweza kuwa kweli haya tuambie hiyo famulia iko wapi?" 
"Familia yangu inaongozwa na rafiki wa bwana Paul...." 
"Paul huyu mfanya biashara za haramu hapo mwanzo alikuwa ana hoteli nyingi sana" 
Aliongea yule jamaa mwingine. 
"Ndio yeye. Mke wangu aliniacha akaenda kwa mwanume mwingine, nikajiingiza kwenye kazi ya uvuvi ambayo nilikutana na huyu jamaa.......mpaka sasa mnaniona upande wa huu mguu unaoza kama hivi." 
Niliwahadithia kila kitu mpaka wakakubali kabisa. 
"Sasa tunakuletea familia yako hapa pamoja na sanduku hilo, lakini kwa sharti moja tu hatutokupa familia yako mpaka utupeleke huko Kisiwani." 
Nilikubali kwa yale yote kutokana nahitaji kuwa huru kabisa. 
"Sawa fanyeni hivyo na mimi nitawafanikishia kuwapeleka huko salama na mkachukua mtakacho". 
Waliniacha pale wkiniahidi jioni yake wananijia pale nilipo wakiwa na familia yangu pamoja na lile sanduku ili mimi niwapeleke huko kisiwani. 
Nikiwa nimebaki pale simu ilinguruma, hapo ndipo nikakumbuka kuwa nilikuwa na simu ya Salha. 
Niliipokea. 
"Mnali...baby mbona haupo umeelekea wapi?" 
Sauti yake ya kiunafiki Salha alidhani nitalegea na kuwa bwege mtozeni". 
"Sema shida yako katili mkubwa wewe mwanamke uliyepoteza sifa ya uanamke wako..." 
"Kwa nini unanituhumu hivyo mpenzi wangu..." 
"Mshenzi weweeee mpenzi wako nani hapa na ukome kabisa..." 
"Sasa kama unakataa jamani mbona umelala na mimi na mbona umeshika simu yangu unayo basi lete...." 
"Kulala na wewe ni kama kuingia kwenye dimbwi la maji kwenye kiza...hunipati tena kumbe wewe unashirikiana na shetani Paul kutaka kuniua mimi ndio maana mmeniwekea sumu ile asubuhi eti unaloweka na nguo zangu kwenye maji.." 
Baada ya hapo salha aliona hawezi kunipata kabisa. 
"Ahaaa...umejifanya mjanja zaidi ya sungura kula mmea ambao mwanadamu akila anakufa.. sasa nakuambiaje chagua moja kati ya haya..kupoteza familia yako ambayo iko chini yangu sasa au wewe kujisalimisha hapa mwenyewe." 
Hapo akakata simu kabisa. Nilishtushwa na ile habari maana kama hawa wanaenda kuchukua familia yangu na wakati Salha anasema iko kwenye himaya yake?. Mh nini hatma ya familia yangu au nini hatma ya maisha yangu kule kisiwani?. Nilibaki kusubiri nikiwa na maamuzi mawilimawili ya kubaki kuwaamini wale waliokwenda au kwenda kujipeleka, nilipatwa na hasira nikaitupia simu kwenye maji. 

JE MNALI ATAFANIKIWA JANJA YAKE KWA WALE JAMAA WALIOKWENDA KUCHUKUA SANDUKU NA FAMILIA YAKE. 
JE SALHA ATAFANYA NINI ILI AMKAMATE MNALI.

TUKUTANE TOLEO LIJALO 

Comments

Popular posts from this blog

SMS 47 ZA MAPENZI ZITAKAZO MNYEGEZA** MPENZI WAKO

KWANINI WADADA WENGI WAREMBO NA WANAOJIONA WAREMBO HUCHELEWA KUOLEWA,HUKOSEA KUOLEWA AU KUTOOLEWA KABISA?SOMA HAPA

HATUA ZA KUCHEZEA KIHARAGE NA KISIMI