RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA THELATHINI NA TATU 33



ENDELEA....... 
Baada ya kumalizana na yule mganga alituruhusu huku akitupatia masharti ya kawaida sana ambayo kwa yeyote kati yetu angeweza kulitatua. 
Mshana pamoja na mimi tulimhofia yule kiumbe ambae kwa mujibu wa mganga kuwa tayari kamkamata na hawezi kutoka tena mpaka pale atakapommaliza kabisa na apotelee mbali. Safari yetu ilikuwa yenye wasiwasi mkubwa sana lakini tulijitahidi kufika nyumbani salama bila hata kuwa na kipingamizi chochote. Mshana alizidi kunitia moyo kuwa nisijali kutokana na yale ambayo yanajitokeza. 
Akili yangu ilibaki kuwaza familia yangu inaendeleaje huko iliko, ghafla gari linaingia pale tulipo na wanashuka Vijana wawili Manyota na Musa ambao moja kwa moja walikuja kunikamata bila hata kujua sababu ni nini zaidi. Walinilazimisha kufika hadi kwenye lile gari ambalo alikuwemo Mzee Paul pamoja na Salha. 
Nilijua kuwa leo hii kazi ipo na lazima wanifanyie kitu mbaya watu hawa. Walinibeba hadi kufika kwenye nyumba ya moja ambayo sikuweza kuitambua vyema. Walinisukumia ndani humo kisha wakanza na kunihoji maswali ambayo kwangu yalikuwa kama kitendawili. 
"Mnali tumesikia kuwa wewe unamiliki kisiwa cha majini kwenye ile bahari kweli ama si kweli". 
Swali aliuliza Manyota. Nilimuangalia ila swali pia nilimuuliza yeye tangu aanze pale kuvua samaki alishamsiki nani kama kuna kisiwa cha majini pale?. Swali hilo pia Manyota hakujibu ndipo walipoona kuwa mimi ni kiburi wakaanza kunipiga kwa nguvu sana sehemu za tumboni na kunipatia maumivu makali. 
"Unakataa unatakiwa kutueleza Sanduku lile wapi umelipeleka, na pia vijana wawili ambao tunafanya nao biashara umewapeleka wapi?". Kwa hakika hakuna kati yao ambae anafahamu swala zima la mimi kuwapeleka wale kule kisiwani japo wenyewe ndio walitaka. 
"Mimi siwajui na sijui hiko mnachozungumza". 
"Mnali utakufa hapa tunahitaji kujua kuhusiana na lile boksi pamoja na wale vijana waliopotea laa sivyo hutatoka mzima". 
"Nakuapia kuwa hiko kisiwa sikijui na wala hao vijana siwajui kadhalika boksi sina na silitambui". 
"Huyu jeuriii...." 
Walimuita Salha alikuja mbele yangu na kunitizama lakini mimi nilimkazia kama simjui kabisa. 
"Unanijua mimi?" 
"Hapana sikutambui kabisa" 
"Mshenziiii! Umekaaa kwangu mwezi tena unanifahamu nyuma na mbele shenzi wewe leo utasema wale watu wako wapi na boksi mmepelwka wapi". 
Aliongea kwa msisitizo mkubwa sana kiasi kwamba ana uhakika na kile anachokisema. "Sikieni nyinyi wajinga...." 
"Khaaaa! Anatukana huyu mpuuzi..." 
"Ndio nyinyi ni wajinga kwanza mnalazimisha vitu ambavyo haviwezekani, mmekamata familia yangu alafu leo mnajifanya kunidhihaki kwa lipi...hamtoweza kupata chochote kwangu kama hamtoweza kuonyesha au kunipatia familia yangu". 
Niliongea nao kwa jazba huku nikiwa na imani tosha kuwa Mshana atafanya juhudi zozote zile ili kunisaidia. Lakini mpaka masaa matatu yanafika bado sioni dalili ya kuja mtu kunisaidia. 
Kwa kweli walinipiga sana mpaka nikakosa nguvu za kufanya mengine. Majira ya usiku wa saa tano alifika Salha kwenye kile chumba, alipofika aalinikaribia na kuanza kunishikashika bila mpangilio alionekana ni mwanamke malaya sana ambae anautumia mwili wake kupata anavyovitaka. 
"Wewee mwanamke shetani unataka nini kwangu....". 
"Niko radhi nikupe mwili kwa mara nyingine ili nifurahi kupata mambo mazuri". 
"Nakuambiajeee hutofanikiwa na sina hisia yeyote ya kimapenzi na wewe ila kama utaniahidi kunirejeshea familia yangu nitawaonyesha wapi ambapo watu wenu wanapatikana na hiko kisiwa kipo wapi". 
"Kwa hiyo shida ni familia yako tu" 
"Ndio" 
"Unajua sisi tunashindwa kukuachia kwa sababu ni kama kinga yetu ila ipo sehemu salama kabisa kwa sasa usiwe na shaka. Kesho utatupeleka huko moja kwa moja tukashuhudie." 
Nikiwa bado nimetulia pale hali yangu haikuwa nzuri sana kutokana a kipigo kutoka kwa Manyota. Ghafla usiku huo baada ya Salha kutoka mule chumbani ndipo sauti za ajabu ajabu zasikika zikisumbua masikio yangu. Haraka sana nashtuka mlango unafunguliwa na sauti ya mngurumo nausikia lakini baada ya sauti ile kuingia nje pia nilipata kusikia sauti za watu wakilalama. 
Nilijua moja kwa moja yule kiumbe kafika pale nilimuona Manyota anaingia akiwa na jazba kubwa lakini hakuweza kunigusa hata kidogo maana alipigwa na kuanguka mbali kwenye ukuta. Niliona nafunguliwa na sauti ya mihemo nikiisikia karibu yangu. 
Bado nilizidi kuwaza kuwa ni kiumbe gani huyu ambae ananisaidia na hali mganga alisema kuwa kamfunga?. Niliondoka bila kikwazo chochote hadi kwa rafiki yangu Mshana. Aliponiona alinikimbilia lakini alishindwa kunikaribia baada ya kusukumwa na yule kiumbeee. 
"Duuuu! Karudiiiiii" 
Nilipoingia ndani ndipo Mshana akafanikiwa kunishika hakika niliumia sana kutokana na vipigo vile. 
"Mnali mbona wanakuandama sana hawa watu jamani eeeeh! Umewafanyia nini..." 
"Aaaah! Wanataka niwapeleke kule kisiwani sasa mimi naogopa kuleta majanga mengine kama yaliyonikuta". 
"Nilienda kwa yule mtaalamu muda uleule nikamueleza kuwa walikuja na wakakuteka akasema msaada uliobaki ni kumuachia yule kiumbe aje kukusaidia lakini anataka leoleo alfajiri tuelekee kwa yule mganga kwa ajili ya ile kazi". 
Nilimueleza nitashindwa kwa kuwa hata nguvu ya kutembea sina kabisa, unaona nilivyopigwa?. Sawa mnali ila unajua kuwa matatizo yatazidi kuwa makubwa sana. Twendeeee. 
Alinilazimisha huku akinibeba, akichoka ananishusha natembea hivyohivyo, ilikuwa majira ya usiku sana kama saa nane tunaingia kwa Mtaalamu yule ambae alikuwa bado kulala akitusubiri. 
Tulimsalimu kisha tukatulia tukimsikiliza. 
"Mnaliiiii nimeona kila kitu, inatakiwa sadaka ya damu haraka sana imwagwe baharini majira ya asubuhi lazima ifanyike". 
"Sasa tunapata wapi hiyo kafara?" 
"Ipo tayariiii nenda wale ambao wanataka uwapeleke huko kisiwani pia kumbuka nitakupa dawa ambayo ukifika umbali wa kuiacha nchi kavu itupie ndani ya maji alafu hakikisha unajitosa kwenye maji lakini usafiri wenu uwe wa mtumbwi na sio boti" 
"Mtaalamu vipi nitawezaje kufanya hivyo na hali s..." 
"Ukishindwa amini kuanzia kesho mwezi unaandama baharini na utashindwavkufanya kazi hiyo kwa sababu nguvu ya mwezi itakinzana na dawa yangu na kukufanya ufeli..kinachofuata wale wawili watatoka baharini na kuanza kuuwa mmoja baada ya mwingine wakikutafuta wewe". 
Aiseee tuliishiwa nguvu kabisa. Inatubidi turudi kule kwa Mzee paul nikawakubalie kwa haraka tuanze safari. 
Kweli tulielekea kule majira ya saa kumi tunafika kwa mzee paul ambae alifurahi sana baada ya kumueleza kuwa nipo tayari kuwapeleka ili wanipe mwanangu. Mzee paul alifurahi sana akamuita yule kijana wake Manyota pamoja na Salha wakajiandaa kwa safari. "Tunasafiri kwa lile boti ili tuwahi kufika". Nilimkumbuka mzee alisema kuwa usafiri uwe wa mtumbwi na si boti. 
"Hapana mzee ile sehemu haihitaji makelele tutakwenda kwa mtumbwi tu". 
Walishangaa lakini haikuwa na jinsi tuliongozana kuelekea baharini. Bahari ilikuwa shwari kutokana na matatizo kadhaa yaliyojitokeza siku chache zilizopita. 
Walimchukua kijana mmoja ambae namfahamu hata mara ya kwanza tulipoelekea na wale wawili alitupeleka. Kijana huyo aliponiona alishtuka kisha akawashangaza kwa kusema. 
"Haaaa wewe unawapeleka watu kule sehemu mbaya aaaah! Sitaki kabisaaa siwapeleki niliyojionea ile siku wakati narudi nayajua mwenyewe..." 
Manyota alinijia na kunieleza. Unataka kutumaliza kwa njia zako za ajabu? Bosi hii safari haifai kabisa inabidi tughailishe hii ni triki ya kutumaliza sisi mkuu. 
Niliumia sana maana muda unawadia sijui sasa nifanyaje?. 

Hery ya mwaka mpya 

TUKUTANE TOLEO LIJALO 

Comments

Popular posts from this blog

SMS 47 ZA MAPENZI ZITAKAZO MNYEGEZA** MPENZI WAKO

KWANINI WADADA WENGI WAREMBO NA WANAOJIONA WAREMBO HUCHELEWA KUOLEWA,HUKOSEA KUOLEWA AU KUTOOLEWA KABISA?SOMA HAPA

HATUA ZA KUCHEZEA KIHARAGE NA KISIMI