KOVU LA MOYO 33






Poshie alistuka na kumtazama na kumsukuma yule kijana kwa nguvu, kisha akachukua shuka na kujifunika huku akihema kwa nguvu 
"Unataka nini?" .... Poshie alimuuliza kwa sauti huku akihema kwa nguvu ... "Swali gani ilo unaloniuliza? inamana mimi mpaka nimekuvua nguo haujui nataka nini kwako?" ... Yule kijana alimjibu Poshie huku akizidi kumsogelea ... "Inamana unataka kuniambia ulikuwa ukitaka kufanya mapenzi na Mimi?" ... "Ndio maana yake, mbona maswali mengi kama tupo mahakamani?" ... Yule kijana aliongea na kuzidi kuvua nguo zake na kubaki kama alivyo. 
Poshie alilia sana na kumuomba hasimfanyie anachotaka kumfanyia .... "Tafadhali nakuomba sana Kaka, Mimi ni mtoto wa kike naamini hata wewe kwenu utakuwa na ndugu kama mimi sasa unavyoamua kunifanyia ukatiri ni sawa kama umemfanyia Dada yako au Mama yako Mzazi" ... Yule jamaa lilimtoka kofi la nguvu lililomsukuma poshie mpaka ukutani .... "Maneno gani unayoniambia wewe? Yani mimi nikafanye mapenzi na Mama yangu mzazi? Sasa kama ulikuwa hautaki si bora ungeniambia tokea mwanzo. We unafikiri katika Dunia hii kuna msaada wa bure? .. Tafadhali naomba uvue nguo kabla sijatumia nguvu zangu" ... Yule jamaa aliongea kwa hasira huku jasho likimmwagika kama amemwagiwa maji 
Katika maisha yake Poshie aliwahi kufanya kosa moja tu nalo ni kukubali kulala na Omega na kwa sababu alitumia nguvu na yeye aliona bora amuachie tu, mpaka hapo alipo alikuwa hajui kama mzima au la? Ivyo hakupenda mwili wake amuachie mwanaume mwengine wa ovyo aliyetokea kumtamani tu na siyo kumpenda ... Wakati yule kijana akiwa amesimama huku akimsubilia poshie avue nguo, Poshie alikuwa akitafakari jambo moja tu ni jinsi gani anaweza kumuepuka huyo kijana 
Siku zote Henry alikuwa kama mtoto fulani ambaye alikuwa akipenda kumuokoa mama yake pindi kunapotokea matatizo ila ndio ivyo tu alikuwa mdogo sana ... Wakati Poshie akitaka kufanyiwa ukatiri Henry aliamka na kuanza kulia kwa sauti .... "Samahani naomba basi nimnyonyeshe mwanangu kwanza" ... Poshie aliongea kwa uoga huku akitaka kumchukua Henry ... "Unajua wewe una mambo ya ajabu sana. Tafadhali naomba usinitoe mudi nipe walau mara moja kisha utaendelea na huyo mwanao" .... Maneno ya yule kijana yalizidi kumuuzi Poshie na aliona lolote na liwe lakini ni bora apambane kutoka katika hicho chumba japo ilikuwa ni usiku sana 
****** 
Baada ya kupigiwa simu na kulazimishwa aende kwa Dr Ally, Aisha aliona isiwe tabu alitoka usiku huo na kwenda nyumbani kwa Dr Ally 
Kitu pekee kilichokuwa kikimuumiza kichwa Aisha ni kwamba Alifika kwa Dr Ally lakini hakumkuta aliamua kumpigia simu yake Dr Ally alikuwa akipokea kwa hasira na kumwambia amsubiri yeye anakuja hapo ... Aisha alisubiri sana bila ya kumuona Dr Ally akija, alikaa sebuleni mwishowe usingizi ukampitia ... "Amka wewe Shetani" .... Dr Ally alifika na kumuamsha Aisha ... "Umeniitaje wewe Ally" .... "Nimekuita Shetani na ukiendelea kuleta upuuzi wako nitakutwanga makofi muda si mrefu" ... Dr Ally alikuwa amechukia kupita maelezo na siku hiyo alikuwa amejitolea lolote na liwe .... "Naomba uniambie kwanini ulimteka Poshie na kumfukuza nyumbani kwangu?" ... "Ina Mana kunikurupusha kote huko ni kwa sababu ya yule ombaomba wako? Nimemtimua kwa sababu siwezi kukubali kuona mume wangu akiibiwa na mimi nikiona" ... "Mimi mume wako tokea lini? Wapi tulipofunga hiyo ndoa mimi na wewe?" ... "Hata kama bado hatujafunga ndoa lakini wewe si mchumba wangu na kila mtu anatambulika kwa mwenzake? ... "Sawa, umemfukuza yule msichana wewe nyumbani kwako hapa?"... 
Hapakuwa na maelewano baina ya Dr Ally na Mpenzi wake kisa Aisha kumfukuza Poshie ... Dr Ally aliyajua fika maisha ya Poshie, na kwa kitendo cha Poshie kumuadisia kila kitu kinachohusu maisha yake, Dr Ally aliona ni jinsi gani Poshie alivyotokea kumuamini na kuona yeye ndiyo kimbilio lake na ana uwezo mkubwa wa kumsaidia
"Mimi ninachotaka ni kumuona Poshie hapa nyumbani kwangu , akiwa na mwananwe na kama likishindikana ilo basi naomba mimi na wewe mapenzi yetu yaishie hapa" ... "Unanichekesha Ally, yani mimi na wewe tuachane kisa yule Mwanamke? Sasa ndio nimeamini kama wewe yule ni mwanamke wako na nakwambia mimi sitokubali hata kidogo niachane na wewe kisa yule changudoa wako" ... Aisha alimjibu Dr Ally na kuondoka zake usiku huo huo 
****** 
Baada ya kusuka mipango na ikasukika siku hiyo ndio ilikuwa siku ambayo wazee wa kazi wamekuja kuchukua chao nyumbani kwa Prince Wanasema watu wakitaka lao chini ya jua hakuna kinachoshindikana. 
Walijua fika udhaifu wa Prince ni Wanawake na watu wakamletea kile akipendacho ... Mara nyingi kifo kinaweza kukuta katika kazi yako uipendayo na hayo ndio yalikuwa yametokea kwa Prince 
Kulikuwa na mawakala maalumu wa kumtafutia Wanawake bwana mkubwa kisha yeye anawatumia atakavyo kisha anawalipa ujira wao, na kumuacha na maisha yake ... Hakupenda kuwa na mwanamke wa kudumu naye ndiomana aliamua kumtafutia sababu Poshie pomoja na Shakira .... Kama ilivyo ada siku hiyo aliletewa wanawake wazuri watatu na Prince alionekana mwenye furaha akijua fika kuwa siku hiyo atafaidi kupita maelezo 
Aliwachukua na kuwapeleka chumbani kwake kama ilivyokawaida yake huwa anafanya mapenzi nao wote huku akiwafanyia vitu vya ajabu apendavyo yeye ... akiwa amelala kifudifudi huku wale wanawake wakimchua mwili ghafla akapewa mapigo kazaa takatifu ya kumlegeza mwili kisha wote wakatoa bastola na kumuweka chini ya ulinzi .... "ukijaribu kutikisika tunakupasua ubongo wako sasaivi" .... Mmoja wa wale Wanawake alimwambia Prince kana kwamba siyo aliyekuja kama changudoa .... Prince alitaka kujifanya yeye ni Mtoto wa mjini achomoe ya kwake na apambane nao .... Ghafla ulisikika mlio wa risasi paaaaaaaa!!! 
******* 
Unapokutana na Wanaume washenzi na wewe ukajiregeza ili wakuachie Wanaweza wakakufanyia ufilauni na kila siku utakuwa unachezewa na kuambukizwa magonjwa ambayo ukuyategemea katika maisha yako. 
Poshie alifikikiria na kunyanyuka kisha akamtazama mwanawe na machozi yakawa yanamtoka akamfuata yule kijana na kumkumbatia .... "Naitaji unipe penzi adimu sana mpenzi wangu ambalo sijawahi kulipata katika maisha yangu" ... Poshie alimwambia yule kijana na kumpapasa na kumfanya yule kijana naye aanze kumpapasa mwili mzima .... "Usijali Mpenzi wangu nipo kwa ajili yako, nitakupa vitu ambavyo haujawahi kukutana navyo katika maisha yako" ... "Heti hee! Baba Mtoto wangu hajawahi kunifikisha hata siku moja, nitafurahi sana kama utafanikiwa kunifikisha" ... Poshie alimwambia na kumuachia kisha akarudi nyuma na kuanza kuvua nguo .... "Fumba macho bwana baby mi nakuonea haibu" .... Poshie alimwambia na jamaa akafumba macho haraka sana ... Pembeni kulikuwa na rungu kubwa la huyo jamaa Poshie akaliokota haraka na kumtwanga nalo sehemu za siri paaaaa!! ... "Mamaaaaa nakufaaaaaaa" ... "Mshenzi mkubwa wee!! Kumbe unamuheshimu sana Mama yako, kwanini hautaki kuheshimu na wanawake wengine??" 
Nini kitaendelea? Poshie atafanikiwa kuchomoka? Vipi kuhusu Prince je amekufa? .... Tukutane ktk episode ya 34 

Comments

Popular posts from this blog

SMS 47 ZA MAPENZI ZITAKAZO MNYEGEZA** MPENZI WAKO

KWANINI WADADA WENGI WAREMBO NA WANAOJIONA WAREMBO HUCHELEWA KUOLEWA,HUKOSEA KUOLEWA AU KUTOOLEWA KABISA?SOMA HAPA

HATUA ZA KUCHEZEA KIHARAGE NA KISIMI