KOVU LA MOYO 35







Poshie alimtazama kwa uoga huku akitetemeka na hasijue nini chakufanya .. Wakati yule jamaa anavua nguo Poshie haraka akapata wazo.. 
Poshie Alinyanyuka na kumuweka mwanawe vizuri na kumwita yule kaka .. "Unataka kwenda wapi" ... Yule jamaa almshika mkono na kumzuia ... "nilikuwa nataka twende tukafanyie pale hapa pamekaa vibaya" ... Poshie alimwambia kwa sauti fulani ya kudeka ili kumlegeza yule kijana kisha akamfanyie kama alivyomfanyia yule Mlinzi ... "Sikiliza nikwambie Unapotaka kulalia wewe, Mimi nimeshaamka siku nyingi. Sina muda wa kupoteza na wewe inama unipe mambo" .. Yule kijana alimwambia huku akiwa amechukia ... "Lakini kwanini Kaka umeamua kunifanyia hivi, Mimi ni mtotio wa kike kama alivyo mama yako au Dada yako pale nyumbani kwenu" .. "Sikiliza nikuambie binti, Mimi sina muda wa kuanza kupokea hayo maubiri yako nimekwambia inama usitake kunichelewesha, kama kweli ulikuwa unayajua hayo, pale ulitaka kwenda kufanya nini? kuna kitu ulitaka kunifanyia si ndio?" ... Yule kijana alizidi kumfokea na kutoa panga akamchapa nalo kwenye mgongo .... 
Kitendo cha yule jamaa kutoa panga na kumtandika nalo Poshie, kilimfanya Poshie akate tamaa na hakuwa na mbinu mbadala ya kumuepuka huyo kijana ... Roho ilimuuma sana kwa kitendo alichokuwa akifanyiwa na kila mwanaume aliyekuwa akikutana naye ... Lakini kilichokua kikimuuma ziidi ni kubakwa mbele ya mwanae... Poshie alishindwa kujizuia na kujikuta akizidi kulia 
Anampenda sana mwanae anamuheshimu na yupo kwa niaba ya kuokoa maisha yake endapo ikatokea yule kijana akampiga na lile panga tumboni au sehemu yoyote mbayo inaweza kuatarisha maisha yake au kumtia kilema cha maisha basi hakutokuwa na mtu ambye anaweza akmlea mtoto wake na ukizingatia Baba yake ndio kama vile hamtaki hata kumsaidia. Kiukweli alikata tamaa kabisaa 
Wakati Yule kijana akiwa anajiandaa kumfanyia unyama Poshie ghafla akachapwa fimbo na mtu hasiyemuona ... akastuka na kugeuka Mala Poshie naye akachapwa fimbo ... Wote kwa pamoja wakaanza kuogopa na kuulizana nini kilichotoea .. Wakiwa hawajajua nini kilichotokea hapo mara kukawa na mwanga mkubwa ulikuwa ukiwapiga machoni. 
Alikuwa kama mtu ameshika tochi na alikuwa akiwafuata. 
Poshie alikuwa akiogopa na alimkamata yule kijana kwa nguvu zote huku akimuuliza yule kijana mswali kibao yaliyokosa majibu .. Ule mwanga uliwafuata mala ukakata na pakawa kimyaaa ... Kabla hawajatafakari kilichotokea hapo sekunde chache Ghafla ukasikika muungurumo mkubwa na wakutisha kama Simba amemkurupua mnyama aliyetaka kumkamata ... Hakuna aliyeweza kusubiri kumuuliza mwenzake nini kilichotokea hapo na kila mmoja alishika njia yake ili kuokoa maisha yake. 
Nguvu za Ajabu zilimpata Poshie na akakimbia kuliko alivyokuwa akikimbia mwanzo ... Kitu kilichomshangaza zaidi wakati anakimbia ni kwamba Tokea yalipotokea yale mauzauza Henry alikaa kimya na kunyamaza kabisaa 
Poshie alikimbia bila kujua wapi alipokuwa anakimbilia kitu pekee ambacho kilikuwa akilini mwake ni kuokoa maisha yake yeye na mwanae ... Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, Poshie Alikimbia na kujikuta ametokea pale palipokuwa na nyumba ya Marehemu Bi Dua na kuingia katika kile kijumba cha yule kijana aliyetaka kumbaka. 
Aliona kama kuna mtu ambaye alikuwa akimkimbiza alifika na kuusukuama ule mlango na kujifungia ndani ... Alipofika ndani alimkuta yule kijana kidogo amepunguza kuugulia ... "Nilikuambia usiondoke tokea mwanzo lakini ulikuwa mbishi" .. Yule kijana alimwambia Poshie ambaye hakumjibu kitu na badala yake aliendelea kuhema kwa nguvu huku akiwa haamini kama kweli amenusulika kutoka pale alipokuwepo ... Poshie hakuweza kupata usingizi siku hiyo na hakutaka kabisa kulala kwa sababu aliogopa yule kijana anaweza akaamka na kufungua kamba alizomfunga na kumfanyia kitendo cha kifirauni ... Wakati yupo chini amejiegesha huku akiwa amemlaza mwanawe aliona damu zinamtoka mguuni na alijitizama vizuri aligundua kuwa, kucha ilikuwa imeng'oka katika kidole chake gumba ... 
Alichana kitambaa Mtoto wa kike na kukifunga kidole kilichokua kikitoa damu nyingi na kumshukuru Mungu wake kwa kumuepusha na majanga mawili kwa mpigo ... Yani kubakwa na yale mauzauza yaliyojitokeza pale 
****** 
Asubuhi na Mapema kabla yule kijana hajaamka Poshie aliamka na kumuinua mwanae na kumbeba mgongoni ... Kwa bahati mbaya, wakati yale matatizo yanajitokeza alikuwa ameangusha begi lake na alijaribu kudamka ili kuona kama anaweza kulipata begi ilo ... Ilikuwa ngumu kuigundua ile njia ambayo alikuwa ameipita jana usiku, alijitaidi sana kuutafuta mkoba wake lakini wapi hakuweza kuupata. 
Baada ya kuangaika sana huku akiwa hajui nini hatma yake ya kila siku wakati alikuwa hana hata pesa ya kunywa chai kwa siku, na hakujua ni vipi ataendelea kushi kama Mtoto wa kike ... "Nimeteseka vya kutosha, kwanini niangaike peke yangu wakati Henry ana baba yake? Ni lazima niende Kwa Angelo ili nikambwagie Mtoto na yeye atajua nini chakufanya na Mtoto wake .. Najuta kwanini nilikubali kumuachia Angelo auchezee Usichana wangu na leo hajui thamani yangu" ... Poshie aliongea mwenyewe na kulia sana. 
Waliokuwa wakipita kwenda katika miangaiko yao ya kila siku walikuwa wakimuona Poshie kama Mtu ambaye Amechanganyikiwa na hakuna hata aliyethubutu kumfuata na kumuuliza nini kinachomliza asubuhi yote ile. 
Maisha bwana kamwe usimdhalau mtu usiye mjua,. Usimuone mtu anatembea na kuongea mwenyewe na wewe ukamcheka, chunga sana siku moja unaweza kuja kulia kama yeye ... {Poshie ni funzo kubwa sana kwa Dada zangu ambao umekuwa mkiwazawadia wapenzi wenu miili yenu bila kuwachunguza vya kutosha, huku ukijitoa kwa kila kitu juu yake bila kujua kama siku moja nawe anaweza kukumbuka na kuuthamini utu wako .. Maneno yangu siyo sheria ukipenda jifunze} 
Baada ya kukubaliana na Mawazo yake Poshie Aliona bora aende Nyumbani kwa Angelo na akambwagie mtoto .. Alinyanyuka na kutembea kwa haraka kama kuna kitu amekisahau sehemu aendako ... "Leo unaenda kwa Baba mwanagu, nafikiri unaona jinsi gani mimi ninavyopata tabu na wewe? Nakupenda sana mwanagu lakini maji yamefika shingoni nafikiri mwenyewe unajionea! Baba yako ametutupa kama hatuoni sasa ni zamu yake na mimi nipumzike na moyo wangu. Amenifanyia mengi sana Angelo lakini hata wewe anashindwa kukulea?" ... Poshie alitembea na kuongea mwenyewe kama mtu ambaye alikuwa akikaribia kuokota makopo ... {Maisha haya we acha tu jamani. Kuna wakati Binaadamu tunatenda sana dhambi. Kina Kaka kama kuna dhambi kubwa muitendayo nikuwapa wadada Mimba na kuwakataa yani dah!!} 
******* 
Prince alimwaga damu usiku kucha na hapakuwa na mtu ambaye alijitokeza na kumsaidia. Baada ya kuugulia maumivu sana na kumwaga damu nyingi sana Prince alipoteza fahamu kabisa na hapo ndipo Walinzi wake walipoona hiyo ndio sehemu pekee ya kuweza kumfundisha jinsi ya kuishi na watu. 
Kama Wahenga walivyosema hasiyefunzwa na mamaye basi urimwengu utamfunza na siku hiyo waliamua kumfunza maisha Prince 
Walimchukua Prince na kumpakia Katika gari na kwenda kumtupa katika fukwe za bahari ya Indi huku akiwa hajitambui na wao wakarudi zao. 
Baada ya kurudi nyumbani kwa Prince walichukua Fuso mbili na kuja kuhamisha vitu nyumbani kwa Prince kama palikuwa nyumbani kwai, kiukweli hawajabakisha kitu hapo ... Walikomba kila kitu na kuishia zao wanapopajua. 
***** 
Poshie alikuwa akitembea pambezoni mwa barabara huku akiwa anaongea na mwanae kama vile alikuwa akiongea na mtu mzima mwenzake, akika alikuwa amedhamilia kwenda kumpeleka Mtoto kwa Baba yake, laiti angejua mh! 
Aisha alikuwa kwenye gari yake ndogo na yeye akiwa anaenda katika miangaiko yake ya kawaida ghafla akamuona Poshie akiwa anatembea pambezoni mwa barabara ... "Pumbavu kabisa huyu Changudoa! Yani mimi nashindwa kuelewana na Dr Ally Kisa yeye? Yeye kama nani anayenifanya mimi nkose raha kwa mpenzi wangu" ... Aisha alimpita Poshie na gari na kuongea mwenyewe peke yake. 
Ghafla aligeuza gari na kuelekea alipotoka ... "Lazima nikamgonge huyu Malaya ili nimkomoe. Nikiendela kumchekea, hata Ally anaweza hasinioe na akaishia kunichezea" ... Aisha aliongea na kukanyaga mafuta kurudi kwa kasi ili akamgonge Poshie ..... 
NINI KITAENDELEA? . 

Comments

Popular posts from this blog

SMS 47 ZA MAPENZI ZITAKAZO MNYEGEZA** MPENZI WAKO

KWANINI WADADA WENGI WAREMBO NA WANAOJIONA WAREMBO HUCHELEWA KUOLEWA,HUKOSEA KUOLEWA AU KUTOOLEWA KABISA?SOMA HAPA

HATUA ZA KUCHEZEA KIHARAGE NA KISIMI