KOVU LA MOYO 36







Poshie alikuwa akitembea bila ya kujua kama nyuma yake kulikuwa na mtu amempania na alikuwa anataka kumuua 
Aisha alimuona Poshie na alizidi kukanyaga mafuta huku akiwa amemng'atia meno Poshie ili amgonge na kumuua palepale 
Unaweza kuona Binaadamu na Wanyama wote tupo sawa kwa sababu wao pia wanazaa kwa uchungu kama sisi pamoja na kunyonyesha, lakini binaadamu na Wanyama tuna tofauti kubwa sana. Na tofauti yao kubwa na sisi ni kwamba Mnyama amenyimwa uwezo wa kufikiri na kujitambua kwa kile akifanyacho .. Mnyama anaweza kumdhuru mwenzake kwa bahati mbaya au kwa makusudi lakini hasimuombe msamaha zaidi ya kujikung'uta na kuishia zake .. Ndio mana Binadamu ukimfanyia kitendo cha kikatiri binadamu mwenzako basi wewe unaitwa Mnyama maana yake haupo kabisa katika kundi la Binaadamu 
Hivyo basi kwa kitendo ambacho Aisha alikuwa akitaka kwenda kumfanyia Poshie Dhaili alionesha ni jinsi gani alivyokuwa Mnyama. 
Akiwa anakaribia kumfikia Poshie ghafla akaingia Mtoto wa shule barabarani bila kuiona gari ya Aisha iliyokuwa inakuja kwa kasi, na alikuwa akiiwahi daladala iliyokuwa kituoni upande wa pili mwa barabara ..... "Mamaaaaaaaaa!!" .. Yule Mtoto alipiga kelele na kuganda barabarani hasijue nini chakufanya ... Aisha alikanyaga break kwa nguvu zake zote na kusababisha tairi zipige kelele na kuwashtua watu wote waliokuwa maeneo hayo ... Alifanikiwa kumkwepa yule Mtoto na gari ikaenda kuigonga ile Daladala iliyokuwa imepaki pembeni na kuipinda vibaya na kusababisha kioo cha gari yake kivunjike na vioo vikamrukia usoni na kumchana vibaya sana .... Baadhi ya Abiria waliokuwa katika daladala waliumia vibaya sana na watu wazima walikuwa wakilia kama watoto wadogo na yote yamesababishwa na upuuzi wake Aisha 
Kwakitendo chake cha kumkwepa yule mtoto kilimfanya Watu wasimpige na wengi wao walikuwa wakimpongeza kwa ujasiri wake ambao alionesha na kuokoa maisha ya yule mtoto bila ya kujua Dhamila yake ilikuwa nini ... Ama kweli wasiwasi wa mapenzi waua. 
Baada ya kutokea ule mshindo, watu wengi walikimbilia kwenda kutazama ajali hiyo kama unavyowajua wabongo ... Kila anayekimbilia katika tukio husika kila mtu anakuwa na mtazamo wake huku wengine wakienda kwa niaba ya kuwatambua waliopata ajali na kutoa misaada ya haraka lakini wengine wanakuwa kazini na kuja kujarbu kuona kama wanaweza kukwapua chochote cha muhusika aliyepata ajali hata kama ni kukupokonya ... Kati ya watu walio kimbilia ajali ile alikuwa ni Poshie na alipofika pale alistuka kumuona Aisha huku akilia na damu zikiwa zinammwagika kwa wingi usoni na akisema kuwa miguu yake ilikuwa imebanwa. 
Poshie alipomuona alistuka na kutaka kuzuga kama hajamuona ili aondoke zake lakini kwa bahati mbaya Aisha alimuona na kumwita. Poshie alijifanya kama hajamsikia, aligeuza na kuishia zake ... "Dada unaitwa na yule majeruhi nenda kamsikilize anaweza kuwa anakufahamu na ukamsaidia" ... Kijana mmoja alimshika Poshie na kumwambia huku akimuoneshea kwa Aisha ... kwa haibu Poshie alirudi huku akitetemeka na akijifanya hakumjua mwanzo ... "Pole sana Dada kwani imekuaje?" ... Poshie alimuuliza huku akimsaidia kumfuta damu .... "Naomba uniache kwanza wewe unaona nimepata ajali bado unaniuliza maswali kama nipo mahakamani? Chukua simu hii mpigie Dr Ally aje haraka" ... Aisha aliongea kwa hasira huku akimtazama jicho baya Poshie na kama kusingekuwa na watu basi angemfanya kitu chochote pale ... Poshie alichukua simu na kumpigia Dr Ally 
"Hallow" ... Dr Ally alipokea na kusikiliza upande wa pili lakini kutokana na kitete chakuongea na Dr Ally mpaka Poshie alishindwa kuongea lakini baadae alijikaza na kuongea nae ... "Mimi Mama Henry, Mkeo amepata ajali huku na hali yake siyo nzuri unatikiwa uje haraka sana" ... Poshie aliongea huku akiwa anatetemeka kwa kuogopa kuonana na Aisha kwani alihisi anaweza kumfanyia jambo baya 
Kwakitendo cha Dr Ally kupigiwa simu na Poshie kupitia simu ya Aisha kilimstua na kuingiwa na wasiwasi labda Aisha anamfanyia mchezo ama Poshie na mwanae pia ni wahanga wa ajali hiyo ... Aliamua kumpigia tena ili amuelekeze vyema na kumuuliza kama wao walikuwa wazima ... Poshie alimuelekeza na kumtoa hofu kama wao walikuwa wanaendelea vyema 
Baada ya dakika kadhaa Dr Ally alifika pale kwenye tukio na kumpakia Aisha katika gari yake huku akiwa anashirikiana na Poshie na wakamkimbiza hospital .... Poshie alisaidia kumtunzia Aisha vitu vyake zikiwemo simu zake na mkoba ambao ulikuwa na pesa zake. pamoja na kumsaidia Dr Ally kwa jambo lolote ambalo Aisha alitakiwa kufanyiwa ... Nguo za Aisha zilikuwa zimeenea damu na kuchafuka na Poshie alijitaidi kumstiri mwanamke mwenzake Muda wote alipokuwa mule wodini kwa sababu Aisha alikuwa katika tarehe mbaya 
Baadae Ndugu zake Aisha walipofika Poshie aliamua kuwakabidhi kila kitu cha ndugu yao na yeye kuondoka zake. 
Akiwa Ghrofa ya pili ndipo alipokuwa amelazwa Aisha, Dr Ally alimuona Poshie anaishia zake, akafungua dirisha na kujaribu kumwita lakini wapi Poshie alikuwa hasikii hata kidogo .... Dr Ally alibwaga dawa na kuamua kutoka kwenda nje ... "Unaenda wapi?" ... Aisha alimuita na kumuuliza" ... "Namfuata Poshie kwa sababu namuona kama anaondoka" ... "Yani unaacha kuniudumia mimi kwa sababu ya yule mwanamke wako?" ... "Hayo umeongea wewe siyo mimi ila wewe tambua kuwa mimi naenda kumfuata Poshie na siyo Mwanamke wangu" ... Dr Ally alimjibu na kutoka nje kumuwahi Poshie 
Alishusha ngazi haraka na kumkimbilia Poshie na kweli alifanikiwa kumpata alifika na kumshika mkono ... "Unaenda wapi' ... Dr Ally alimvuta na wakakutana macho kwa macho kisha akamuuliza" ... "Kwani vipi Dr? Mimi naenda kujitafutia maisha yangu" ... "Maisha hayo unaenda kuyatafuta wapi" ... "Popote pale ila kwanza naenda kwa Baba Mtoto wangu naenda kumbwagia mwanae kwa sababu hata yule mkeo wakati anapatwa na ajali mimi nilikuwa naelekea huko, hivyo kama Mungu kaniambia nikashangae ndio nikakutana na yeye" ... Dr Ally alisononeka sana baada ya kusikia Poshie anataka kwenda kumbwaga Mtoto kwa mwanaume ambaye alimkana na kumfukuza kama Mbwa ... "Kwanini lakini unataka kwenda kumtupa mwanao katika dimbwi la moto?" ... "Sasa unafikiri nitafanyaje wakati sina Mtu wa kunisaidia? Vyovyote itakavyokuwa lakini yule ni Baba yake mzazi, anaweza kupatwa na huruma" ... "Bado naitaji kukusaidia Pshie Tafadhali naomba nafasi hiyo adimu" ... Mh! Unnishangaza sana Dr Ally, inamana unajifanya haujui kitu alichonifanyia Mkeo?" .. "Najua kila kitu na nimejipanga kukabiliana na yeye" .. Dr ally alimjibu huku akiwa na haibu kwa alichokifanya Aisha kwa Poshie ... "sasa unataka niende pale ili akaniue kabisa? Maana tayari ameshanitishia maisha" 
Dr Ally alijitaidi kumbembeleza Poshie na akamuelewa .. akamwambia amsubiri hapo nje kuna mgahawa kisha akitoka kazini wataondoka na kuongea mengi ... Kisha Dr Ally aliongea na kutoa pochi yake kisha akampa Tsh 50,000 na kumuelekeza kwenye mgahawa na yeye akarudi kazini ... Poshie alizipokea pesa huku akiwa aamini macho yake na akamshukuru mungu wake kisha akaenda kumsubiri hapo kwenye mgahawa na kupata chakula yeye pamoja na mwanae 
******** 
kuna msemo moja unasema "Majuto ni Mjukuu" au laiti ningejua uja mwisho wa safari ... Prince aliokotwa na Wasamalia wema na kukimbizwa Hospital huku akiwa hajitambui ... Alipatiwa matibabu ya mwanzo na kurejesha fahamu zake lakini kilichokua kikimfanya aifikirie hiyo Misemo iliyokuwa hapo juu ni kwamba marafiki zake wote pamoja na wasichana aliokuwa akitanuwa nao walimtenga na kumuacha mwenyewe huku wengine wakiwa wamemsukia mipango ya kuja kumuibia 
Hasikudanganye Mtu kama hauna pesa na hakuna Mtu ambaye anaweza kusimamia matibabu yako, basi kaa ukijua utapata tabu sana ukiwa Hospital na mbaya zaidi Hospital zetu kila siku hazina dawa na Mgonjwa unatakiwa kununuliwa dawa na ndugu zako katika maduka ambayo yanakuwa nje ya Hospital 
Prince aliyakumbuka sana maneno ya Poshie aliyomwambia kipindi kile kuhusu kujenga nyumba na kuanzisha biashara lakini yeye alikataa na kumuona kama alikuwa akimuingilia katika matumizi yake binafsi na kukimbilia kupanga nyumba pembezoni mwa bahari ... Kodi ya nyumba ilikuwa inakaribia kuisha na hakujua kule nyumbani kwake wamembakishia nini? ... Prince alikuwa akilia kama Mtoto Mdogo na kila aliyekuwa akipita alikuwa akimuona kama analia kutokana na maumivu ya mkono na mguu kumbe wapi Prince alikuwa akilia na mengi 
******* 
Baada ya kumaliza shughuli zake Dr Ally alitoka na kuwachukua Poshie pamoja na mtoto wake na kuwapakia katika gari .. wakiwa njiani Dr Ally alimwambia Poshie ... "Nilikuwa nakutafuta sana Poshie, kuna zawadi yako muhimu nilikuwa nataka nikupe na nimeikamilisha tokea siku ambayo wewe umeondoka" .... "Nashukuru sana japokuwa zawadi yenyewe sijaiona" ... Poshie alimjibu huku akiona haibu na kutazama chini ... "Usijali ipo kwa niaba yako na utaiona muda si mrefu" ... Walitembea kama muda wa dakika 40 Dr Ally alisimamisha gari na kumwambia ... "Kwakuwa kitu ninachotakakukupa ni kitu muhimu katika maisha yako, naitaji nikufunge macho yako ili ukifungua macho yako yaone kitu ninachotaka kukupa kwa sababu hiko kitu nilipokiweka si mbali na hapa" .... 
NINI KITAENDELEA 

Comments

Popular posts from this blog

SMS 47 ZA MAPENZI ZITAKAZO MNYEGEZA** MPENZI WAKO

KWANINI WADADA WENGI WAREMBO NA WANAOJIONA WAREMBO HUCHELEWA KUOLEWA,HUKOSEA KUOLEWA AU KUTOOLEWA KABISA?SOMA HAPA

HATUA ZA KUCHEZEA KIHARAGE NA KISIMI