KOVU LA MOYO 37







Moyo wa Poshie ulimuenda mbio na kuanza kumuogopa Dr Ally. 
Hakuamini kama inaweza kuwa zawadi njema kwake 
Dr Ally alitoa kitambaa na kumwambia Poshie .... "Funga macho yako" .. Poshie huku akiwa anahema kwa wasiwasi akafunga Macho yake ... Dr Ally akamfuata na kutaka kumfunga kile kitambaa lakini Poshie akafungua macho yake... "Mbona unafungua macho wakati nimekuambia ufunge?" ... "Sijui kwanini nimefungua lakini Moyo wangu unaenda mbio na najihisi kama ni mtu mwenye mashaka. Zawadi yako ni njema juu yangu?" .... "Safi sana Poshie Kila siku unanifanya nizidi kujipongeza kwa mimi kukufahamu wewe unajua kwanini?" ... Dr Ally alifurahi na kumuuliza tena swali .... "Sijui kwanini? Lakini mbona unaniuliza swali badala ya kujibu swali?" ... 
Dr Ally alicheka kidogo kisha akamjibu .... "Muda mwingine ni vyema kujibu mtu kwa kumuuliza swali ili umpe uwezo wa yeye kuweza kuchanganua baadhi ya mambo hata mimi nikiwa sipo" .... "Sawa nimekuelewa niambie basi kwanini moyo wangu una mashaka sana na zawadi yako?" ... "Mwanamke mzuri ni yule ambaye anakuwa na mashaka na mtu yeyote yule ambaye anajitolea kumsaidia kitu bure kwa sababu si kila anayetoa msaada basi ana muono wa kukusaidia mwengine huwa na malipo anayetaka kutoka kwako, ila kwangu mimi Usijali we toa hofu na mashaka mimi nimeamua kukusaidia kama Dada yangu au Mama yangu nahisi hata mimi nikifa nawe unaweza kuja kuwasaidia Watoto wangu ama Mtu yeyote bila kujali faida kwa upande wako" 
Maneno ya Dr Ally yaliweza kumuingia ipasavyo Poshie na akakubali na kufungwa kitambaa na wakaelekea eneo la tukio. 
"Shuka taratibu usije ukajigonga bure kipofu wangu" ... Dr Ally alimtania Poshie wakati akiwa anashuka katika gari .. Kwa bahati mbaya Poshie wakati anashuka akajikwaa na Dr Ally akamdaka lakini naye alikuwa hajasimama vizuri na akajikuta wakianguka mpaka chini huku Dr Ally akiwa chini na Poshie akiwa juu yake .... "Pole sana kama umeumia" ... Dr Ally aliongea huku akiwa anacheka ... "Mi sitaki yote umeyataka wewe, kwani mpaka unifunge macho yangu?" ... "Samahani kama nimekuuzi" ... Dr Ally alibadirika na kumwambia Poshie ... "Nimegundua kumbe haupendi kutaniwa" ... Poshie alimwambia Dr Ally huku akicheka na kumfanya naye atabasamu na kumtazama usoni ... "Hapana mimi pia napenda utani ila Samahani ni silaha yangu kubwa pindi ninapogundua kuwa nimemkwaza mtu" .. Wote walicheka na Poshie alikuwa tayari kwa kupewa zawadi ambayo Dr Ally alikuwa akitaka kumpatia 
"Nitahesabu mpaka tatu na nikifika tatu tu we utafungua hicho kitambaa na utakachokiona mbele yako basi ni zawadi yako .... Dr Ally alimwambia na kuanza kumuhesabia na ilipofika tatu tu Poshie akafungua kile kitambaa .... "Surpriiiiiiiise" kumbe kulikuwa na umati wa watu waliolipuka kwa shangwe na vigelegele huku wakipiga makofi ... Poshie aligeuka na kuwatazama na kujisikia haibu kwa jinsi yeye alivyokuwa amevaa na wao walivyokuwa wamependeza lakini kilichokuwa kinamtia haibu zaidi ni jinsi alivyokuwa akicheza na Dr Ally na ukizingatia Dr Ally Alikuwa ni mchumba wa mtu, na alijua wote waliokuwa hapo walikua wakitambua hilo 
Hakutaka kuyaruhusu sana macho yake kuwatizama wao akarudi na kutazama chini kisha akakumbuka kuwa Dr Ally alimwambia kuwa pindi atakapofungua macho na atakachokiona mbele yake basi ni mali yake. 
Alistuka baada ya kuona mbele kuna nyumba nzuri ya kisasa na gari ndogo yenye rangi za kupendeza .. Hakuamini macho yake na kushindwa kujizuia na kujikuta machozi yakimtoka ... "Kama nilivyokuambia mwanzo Poshie, unachokiona mbele yako namaanisha hiyo nyumba na ako kagari vitakuwa ni mali yako kwa sasa" ... Dr Ally alimwambia na kusababisha watu waliokuwa hapo kupiga makofi na kushangiria .... Poshie alishindwa hamshukuru vipi Dr Ally badala yake almkumbatia kwa nguvu na kujikuta akilia kwa kilio cha kwikwi 
****** 
Baada ya kufunga chuo Robby alirudi Tanzania na alipofika tu akakutana na matusi ambayo Rafiki yake Angelo ameyafanya Mtaani kwa kuja kumonga Mwanamke gari mbele ya umati wa watu ... "Najuta kwanini nilishindwa kumsaidia yule kijana mwanangu, leo wamekuja kupewa pesa wengine na mimi nimeonekana kama Kinyesi"..... Mama Robby alimwambia mwanawe huku akiwa kitandani kwa sababu pia alikuwa akiumwa ... "Tunaambiwa tenda wema nenda zako, lakini wewe Mama ulikuwa unataka kuwasaidia ili uje upate kitu. Kama ndiyo hivyo hata ungewasaidia basi wasingefanikiwa. Muda mwingine tunafunzwa kuwasaidia watu kama tuna uwezo wa kufanya hivyo sasa wewe mama yangu haukuwa na sababu ya kutowasaidia Poshie na Angelo ndio maana Mungu anakufunza hapa Duniani kama utakuwa na uwezo wa kubadilika basi ufanye hivyo" ... "Nikweli ilo usemalo mwanangu, Sasa wewe Mimi sina pesa za kuendelea kukusomesha tena. Sasa unaonaje ukiwatufuta ili wakusaidie kwa hapa nilipoishia mimi kwa sababu wewe si umewasaidia sana mwanangu?" .... Mama Robby alimwambia mwanae kwa tabu na kuashiria kweli alikuwa ameshikwa ... "Sawa Mama nimekuelewa lakini bado mimi nitakuwa naomba malipo kutokana na msaada niliokuwa nikiwapa. Mimi nitawatafuta kwa sababu ni watu wangu wa karibu na nina hamu sana ya kukutana nao na si kwenda kulia shida, watanisaidia kama watapenda wenyewe. Lakini umenistua baada ya kuniambia kaja kumuonga gari mpenzi wake na si Poshie! Inamana Angelo ameachana na Poshie na tabu zote zile ambazo walizokuwa wakizipata?".... 
Robby alikuwa haamini hata kidogo kama kweli Angelo anaweza kuachana na Poshie na kuja kuwa na mwanamke mwengine na ukizingatia yeye aliwashuudia kutokana na tabu walizokuwa wakizipata .... Mama yake alizidi kusisitiza kuwa Aliyekuja hapo ni Angelo na mwanamke aliyekuja kumpa Gari ni mwanamke mwengine lakini si Poshie 
Robby alijisikia vibaya sana baada ya kusikia Poshie na Angelo wametengana kwa sababu aliamini kuwa mapenzi yao ni ya dhati na kamwe hakuna anayeweza kuja kuwatenganisha ... Alishindwa kutoa hukumu kwa yoyote kwakuwa hakujua nani alikuwa chanzo cha ugomvi wao mpaka wakaamua kuachana ila alitokea kumlaumu sana Angelo kwa kitendo chake alichokuja kukifanya mtahani kwa sababu haikuwa ni picha nzuri kwake yeye kama Rafiki yake kwa sababu hakuna mtu hasiye jua yeye na Poshie walikuwa wametokea wapi .. 
Robby aliapa kuwatafuta wote wawili mpaka awapate na ikiwezekana awapatanishe tena ikiwezekana waje kufanya tena sherehe pale mtaani kwao kama njia ya kumsafisha Angelo kwa kitendo chake alichofanya cha kuchezea pesa na kumpa mwanamke gari 
***** 
Baada ya kufanya kajisherehe kafupi na baadhi ya marafiki zake aliokuwa amewaaalika katika sherehe hiyo fupi ya kumkabidhi nyumba Poshie pamoja na gari ya kutembelea, Dr Ally aliondoka na kumuhaidi Poshie kuwa angerudi kesho yake. 
Kwa mara ya kwanza katika maisha yake Poshie anaishi katika nyumba yake binafsi japokuwa ilikuwa ni ya kupewa likini alikuwa na mamlaka nayo .... "Dada chakula tayari nimeshaandaa" .. Alikuwa ni Mfanyakazi wake aliyekuwa pia ameajiliwa na Dr Ally na kukabidhiwa kwake alimfuata chumbani na kumwambia ... Poshie alitoka na kwenda katika meza ya chakua ... "Wewe je mbona unaondoka?" ... "Mimi nimebakisha chakula changu jikoni nitakula kule lakini kwa saa niliuwa nataka kwenda kukutandikia chumbani na kufua nguo za Henry" ... Yule Mfanyakazi aliongea huku akiwa anamuogopa ... "Mimi ni nani kwako?" ... Poshie alimwita na kumuuliaza ... "Dada" .. "sasa kama Dada, kwanini mimi na wewe kila mtu ale kivyake? Alafu kuhusu kunitandikia kitanda, Mimi pia ni mtoto wa kike kuna vitu vingine natakiwa kufanya mwenyewe umesikia mdogo wangu? ... Mimi sijabweteka bwana we subiri kesho nikae jikoni ndo utaona mambo yangu, kwanza Henry mwenyewe hana hata nguo mdogo wangu we kaa tule kisha nenda ukalale umesikia heeee?" .... Poshie alimwambia yule Msichana wake wa kazi kwa upendo mpaka yule binti akajisikia raha kama yupo nyumbani (Siyo wewe Ndugu yangu umekiajili kitoto cha watu unakilipa Tsh Elfu 50 unakifanyisha kazi kama Mtumwa mpaka nguo zako za ndani akufulie na makofi juu loh) ... 
Alikaa na wakala pamoja kisha wakaagana na akaenda kulala 
Usiku huo Poshie hakupata Usingizi hata kidogo akijaribu kumtathimini Dr Ally alivyoamua kujitoa kwa niaba yake .... "Ni sawa amenipa Nyumba, nashukuru kwa sababu hiki ndicho kilio changu cha siku nyingi sana, lakini angejua hii gari hata hasingenipa kwa sababu, mimi siwezi kuwa tegemezi naitaji kuendesha maisha yangu .. Kama angejua basi pesa ya hii gari bora angenipa mtaji na niwe nimeanzisha biashara yangu" ... Poshie Aiongea mwenyewe na kujaribu kupima mawazo yake lakini aliona imekaa vibaya kwenda kumwabia Dr Ally kuwa kwanini alimua kufanya vile 
****** 
Asubuhi na mapema Dr Ally alitoka na kuwahi Hospital ili kwenda kumtazama Mchumba wake na kumpa baadhi ya maitaji kwa sababu siku hiyo yeye hakuwa kazini ... kisha akaondoka zake na kuja nyumbani kwa Poshie ... Alifika na kuwasalimia kisha akamchukua Henry na kuanza kucheza nae na kumchekesha mpaka Henry akawa anacheka kupita kiasi .... "Chai tayari Ally njoo kwanza unywe chai kisha utacheza baadae na Anko wako" ... Poshie alimfutata Dr Ally na kumwambia ... "Chai hiyo umepika wewe, mbona Dada simuoni?" ... "Chai nimepika mimi na Dada anaendelea na usafi" ... Poshie alimjibu na kumfanya Dr Ally ampongeze kisha akatoka na kwenda kunywa chai 
Baada ya kunywa Chai Dr Ally alimchukua Poshie na kwenda naye Mjini na wakaenda kufanya shoping ya Poshie pamoja na ya Henry kisha wakaondoka na kutafuta sehemu na wakapumzika na Dr Ally akamwambia .... "Kuna kitu naitaji kukumbia Poshie ambacho kitakuwa muhimu katika maisha yako na yangu pia" ... 
Poshie alistuka na kukaa sawa ili ajue ni kitu gani ambacho Dr Ally alikuwa akitaka kumwambia ... "Mimi nakujua wewe kiundani hivi mimi unanijua kiundani?" ... Poshie alistuka na kutazama chini kisha akamjibu ... "Hapana sikujui" .. "Nashukuru kama haunijui japokuwa ulikuwa hautaki kujua ngojea mimi nikwambie mwenyewe" ... "Hapana Dr Mimi nilikuwa nataka sana kujua ila sjawahi kupata nafasi ya kukaa zaidi na wewe" .... Poshie alimjibu Dr Ally na Dr Ally akamuelewa na kuanza kumuelezea 
Kwanza alimwambia kuwa yeye ni Mtoto pekeee katika familia yao ... Baba yake ni Rubani mstaafu wa ndege katika shirika kubwa la ndege ambalo lipo uarabuni na Baba yake anaishi huko kwa miaka mingi sana huku Mama Yake akiwa ni Mfanya biashara wa madini huko huko Uarabuni .... Kwa mila na desturi zao wao huwa wanachaguliwa wapenzi tokea wakiwa wadogo na ndipo familia yake ilimpomchagulia Mpenzi yule anayeitwa Aisha ambaye anatarajia kufunga naye pingu za maisha katika siku za hivi karibuni ... "Wewe upo tofauti sana na Aisha, unajua mimi nimezaliwa katika familia ya wafanya biashara hivyo muda wote akili yangu inawaza biashara ... Muda mrefu nimekuwa nikianzisha biashara na Aisha lakini zinakufa na yeye anaishia kugombana na wafanyakazi na pesa kutumia katika maswala tofauti na malengo yetu. Kama utakuwa muaminifu Mimi nataka kufanya biashara na wewe, na wewe ndio nataka nikuweke msimamizi wa biashara hizo" .... Maneno ya Dr Ally yalimuingia sana Poshie na kuona amegusa kitu kilichopo moyoni mwake ... Poshie alimuhaidi kuwa muaminifu kwake na atajitaidi kadri ya uwezo wake kuakikisha anaziboresha biashara zake 
**** 
BAADA YA MWEZI MMOJA 
Poshie na Dr Ally walifanikiwa kuanzisha biashara n ndani ya mwezi mmoja tu, biashara zao zilizidi kushamili na Poshie alikuwa na mausiano mazuri na wafanya kazi huku akiwa anashirikiana nao kwa kila jambo... mbali ya hayo Poshie alikuwa na sura ya biashara na kwa kitendo cha Dr Ally kumkabidhi kila kitu Poshie alijitaidi kuziboresha biashara na kuzidi kuwavutia wateja wengi waliokuwa wakimiminika kila kukicha 
Habari ya kupewa nyumba kwa Poshie na kukabidhiwa kila kitu zilimfikia Bibie Aisha na sasa aliamua kufanya tukio kubwa zaidi kwa bibie Poshie 
Mnamo Majira ya saa 7 usiku Kuna mdada alikuja na kugonga Nyumbani kwa Poshie na kuja kuomba msaada wa kuifadhiwa kwa sababu alikuwa anakimbizwa na kutaka kubakwa, kutokana na Maisha aliyopitia Poshie hakuitaji hata kujishauri alimkaribisha mpaka ndani ili amsaidie 
Masikini Poshie kumbe aliuwa ameingiza nyoka nyumbani kwake ... Yule Dada alitoa Bastola na kumteka poshie kisha akapiga simu na ikaja gari na watu wasiojulikana wakamchukua kisha wakampeleka porini 
Asubuhi na mapema alimwagiwa maji ya baridi pale alipokuwa amefungwa kamba na kumfanya afungue macho yake .... Akasikia kuna mtu anakuja huku akimpigia makofi ..... "Mwizi wa waume za watu naona umeptikana" ... Poshie akageuka na kukutana uso kwa uso na Aisha .... "Nafikiri nilikuambia ukae mbali na mume wangu lakini ulikuwa hautaki, kama ulikuwa haujui siku zile nilivyopata ajali kwa taharifa yako nilitaka nikuue wewe ila una bahati sana malaya mkubwa wewe" .... Aisha alimwabia Poshie na kumfanya Poshie astuke na kuzidi kumuogopa .... "leo nakupa kilema cha maisha ili ukikaa katika maisha yako ukumbuke kuwa nimepeta kilema hiki kwa sababu ya Mume wa mtu' ... Aisha alimwambia Poshie na kuchukua plaizi na kuwaambia vijana wake wamshike na wakafanya hivyo .... Walimkaba shingoni na Poshie akaachama Mdomo na Aisha akamng'oa jino Poshie na ile plaizi bila ya ganzi .... "Mamaaaaa!! Nakufaaaaa 
Poshie alipiga yowe moja na kuanguka chini na kupoteza fahamu huku damu zikimmwagika kwa wingi ....... 
NINI KITAENDELEA? NINI HATMA YA POSHIE? VIPI ROBBY ATAMUONA ANGELO? 

Comments

Popular posts from this blog

SMS 47 ZA MAPENZI ZITAKAZO MNYEGEZA** MPENZI WAKO

KWANINI WADADA WENGI WAREMBO NA WANAOJIONA WAREMBO HUCHELEWA KUOLEWA,HUKOSEA KUOLEWA AU KUTOOLEWA KABISA?SOMA HAPA

HATUA ZA KUCHEZEA KIHARAGE NA KISIMI