KOVU LA MOYO 38






Poshie alianguka kama mzigo na kupoteza fahamu huku damu nyingi zikimmwagika.. 
"Bila shaka atakuwa amekufa huyu!" ... Kijana mmoja mrefu mweusi mwenye mwili wa mazoezi alimwambia Aisha huku akiwa anamgeuza Poshie ... Aisha alicheka kicheko cha kebehi na kumkanyaga Poshie .. "Samahani sana Poshie kwa nilichokufanyia ila naomba utambue kuwa mimi ni Mwanamke kama wewe na Mume anauma kuliko uchungu wa kuzaa" ... "Siyo bure Aisha, lazima utakuwa umechanganyikiwa!" ... Yule kijana alimuuliza huku akimtazama kwa makini ... "Kwanini unasema hivyo Meja?" ... "Unawezaje kuzungumza na Maiti wakati hakusikii?" ... "Kimwili hatupo naye ila kiroho tupo naye na anasikia kila jambo" ... Aisha alijibu kwa kujiamini na kuwaamuru waondoke eneo lile haraka na kumuacha Poshie pale 
**** 
Ujinga waliofanya waliotumwa na Aisha ni kutokagua ndani kwa Poshie kulikuwa na nani mwengine anayeishi mule .. Walikuwa wamemuacha Dada wa kazi ambaye alishuudia mchezo Mzima. Japokuwa hakujua kama Aisha ndiye aliyesuka mchezo wote 
Hakuwahi kusikia mlio wa bunduki katika maisha yake, siku hiyo alijificha uvunguni mwa kitanda huku akiwa amejikojolea na kulia km mtoto mdogo .. Kama ilivyoada Henry huwa anastuka na kulia kwa sauti pindi Mama yake anapofanyiwa jambo baya ... Siku hiyo alilia sana bila msaada wowote, Mama yake Hakuwepo na Dada wa kazi alikuwa amejificha uvunguni huku akilia usiku kucha. 
Kilio cha Henry kilimstua yule binti na kugundua kuwa Henry alikuwa amelala mwenyewe. Alitoka mbio na kumchukua huku akiogopa na kuanza kummbeleza ... Wakati anambeba Henry na kutoka naye nje ghafla akasikia simu ya Poshie inaita. Haraka akarudi na kuipokea. 
Hakuwa mwingine bali alikuwa ni Dr Ally ... "Jana tumevamiwa na Majambazi na wamemteka Dada Poshie sijui wamempeleka wapi" ... Yule Binti alimwambia Dr Ally huku akiwa analia na kumfanya astuke na kuchanganyikiwa. 
Haraka Dr Ally aliinuka na kutoka nje haraka huku akiwa bado anavaa na kuingia katika gari ... Akika alijua kuwa hakuna mwingine zaidi ya Aisha ndiye atakayekuwa muhusika wa kwanza kufanya huo mchezo ... Aliondoka kwa kasi ya hatari kutoka eneo lile mpaka majirani walimshangaa 
**** 
Maisha kama filam kuna Mwanzo kati na mwisho. Sasa inategemea na mtunzi wewe mwenyewe utakavyojiendesha ndivyo utakavyoishia ... Prince alikuwa amechoka vibaya sana maisha ya Anasa yalimponza, alijaribu kuuza kila kitu chake ili kuendelea na aina ya maisha aliyokuwa akiishi huku bado akiwa anajipa moyo kuwa yeye ndiye Mfalme wa starehe. 
Alikumbuka sana kufuru alizokuwa akifanya baada ya kupata utajiri ambao akuutolea jasho ... Kilichokuwa kikimuuma zaidi ni kwamba yeye alishafanya Sherehe ya kuuaga umasikini na jina akabadilisha kutoka Angelo kuja Prince ... Alikumbuka jinsi alivyokuwa akiogeshwa pesa na kubatizwa na mabinti waliokuwa uchi wa mnyama hakuamini kama yeye leo angekatwa mguu na kuwa mtu wa kawaida kama watu wengine. 
Akiwa amekaa sehemu karibu na mgahawa mmoja huku mvua kubwa ikiwa inamnyeshea mara akamuona Mtu aliyemjua akiwa anatoka mule Mgahawa .... "Dada! Dada!" ... Prince alinyanyuka kwa tabu na gongo lake na kumuwahi yule Dada huku akimuita 
Yule Dada akiwa ameshikana na kijana Mmoja wa kiarabu mwenye nywele nyingi za kuvutia, kwa haraka walionesha kuwa wapenzi. Aligeuka na kumtazama Prince ... Hakuwa mwengine bali alikuwa ni Shakira ... "Prince?!" ... Shakira alistuka na kumtazama kwa Mshangao ... "Nimimi Shakira wala usishangae, yote Maisha kuna kupanda na kuanguka" ... Prince aliongea kwa unyonge huku akitia huruma. 
Shakira alimtazama sana na kutoa miwani yake na kumtazama vyema kisha akacheka tena kwa sauti ... "Mbona unanicheka kiasi icho Shakira? Kumbuka kuwa mimi nimeteleza" ... "Masikini Prince unatia huruma" ... "Nimeamua kuachana na ilo jina kwa sababu linanitia mkosi, kwa sasa naitwa Angelo jina ambalo nimepewa na wazazi wangu" ... Shakira baada ya kusikia jina la Angelo alistuka na kumuuliza ... "Inamana wewe unaitwa Angelo? Na vipi kuhuyu yule mwanamke aliyekuja na mtoto siku zile?" ... "Yule anaitwa Poshie na yule Mtoto ni Damu yangu ila nilimsaliti kwa sababu ya tamaa" ... Angelo aliongea na kulia kama mtoto Mdogo 
Shakira hakuamini kabisa alichokuwa akiongea Angelo ... "Pole sana Angelo mwanaume katiri usiye na roho ya huruma. Yani unamuacha mkeo na Mtoto wako wanapata tabu alafu wewe unaponda raha? ... Mimi nataka kuondoka tafadhali sema shida yako" ... Shakira aliongea kwa madaha huku akimpandisha na kumshusha ... "Shida yangu nilikuwa nataka turudiane" ... Angelo aliongea kwa haibu huku machozi yakimtoka ... Shakira alistuka na kumkumbatia Angelo ... "Yani hata siamini km kweli tunarudiana" .. "Amini hivyo Shakira Mimi bado nakupenda" .. "Nimekuelewa Angelo, ila mimi nina Shart 1" .. "sharti gani mpenzi wangu?" .. "Nidogo ila gumu, naitaji utapike kisha ulambe matapishi yako sasaivi" .. Shakira alimwambia Angelo huku akiwa amemkazia macho .. "Yani Shakira!" .. "Sina mjadala we tapika na ulambe" 
Angelo alimtazama kwa uchungu Shakira na hasijue nini cha kumfanya ... "Shakira wewe si wa kunifanyia hivi, kumbe ulinipendea pesa?" ... Angelo alimwambia Shakira huku akiwa analia ... "Ilo utajua mwenyewe, mimi namshukuru mungu kunitoa katika penzi la Shetani na kwa sasa nina mpenzi wangu nafikiri unamuona na lile gari ambalo umenipa ndiyo lile natesea .. Pole kwa kuporomoka wewe haujaanguka Prince ... Aah! Samahani kumbe Angelo" ... Shakira aliongea na kumdhiaki kisha akaondoka na kuingia katika gari na kummwagia maji machafu. 
Angelo alilia sana na kujinyanyua taratibu pale alipokuwa na kumtukana Shakira hasiye muona ... "Nimefanya sana umalaya lakini sijawahi kukutana na Mwanamke mwenye sifa kama za Poshie ... Kwanini nilikupoteza Poshie wangu? Nakupenda sana Poshie wewe ni Mwanamke wa Maisha yangu" ... Angelo aliongea na kujilaumu mwenyewe .. 
Angelo alitambua fika maumivu aliyompatia Poshie kwa kitendo chake cha kumtelekeza na yeye kuingia katika anasa za dunia ... "Nibora nirudiane na Mpenzi wangu ili tulee mtoto wetu hata kama tutakuwa hatuna kitu .. Lakini Poshie anaweza kukubali kuishi na mimi kweli nikiwa katika hali kama hii?" ... 
Angelo aliongea na kujiuliza maswali mwenyewe kisha akatulia na kufikilia baadae akanyanyuka na kuchekelea ... "Mimi ndiyo Mwanaume wa kwanza wa Poshie. Milele atoniacha ata nimfanyie nini, kinachotakiwa ni kumfuata na kuongea nae" ... Angelo alijipa moyo kwakuwa yeye ndiye aliyemtoa bikra Poshie basi Poshie hana sauti juu yake ni lazima atamsikiliza. 
**** 
"Hallow Mpenzi wangu, umeamkaje?" ... Dr Ally alimpigia simu Aisha na kuongea naye kwa mahaba ya hali ya juu ... "Leo umesahau nini kwangu? Yule malaya wako umegombana naye?" .. Aisha alijibu kwa hasira huku akiwa anaendesha gari ... 
Dr Ally alizidi kuongea naye kwa mahaba na kumuomba wakutane katika Hotel moja kuna kazi anaitaji kumpa ... "Haupo na Mama Henry lakini?" ... Aisha alizuga kumuuliza ili kujua km Dr Ally anajua chochote ... "Mama Henry katika mapenzi yetu anausikaje? Tena sitaki kumsikia hata kidogo huyo changudoa" ... "Imekuaje tena? Usimfanyie hivyo jamani mungu hapendi" ... Aisha alijifanya kuongea kwa upole na huruma km mtu kweli ... "Sikiliza nikwambie Aisha nilipanga sana kumsaidia yule mwanamke ila hafai hata kidogo. Ameniibia pesa zangu nyingi sana, na nataka kumtimua leo hii" ... Kauli ya Dr Ally ilimfanya Aisha afurahi na kuzidi kuongeza kasi ... "Nakuja sasaivi mume wangu tena ikiwezekana kazi ya kumtimua niachie mimi" ... "Yani natamani nikwambie pitia huko kabisa, ila we njoo ukitoka hapa utamtimua. Ila usije kumuonea huruma!" ... "Usijali kwa hilo Mume wangu .. Mimi siwezi kuwa na huruma na kunguni km yule ... Yani kwa jinsi ulivyonifuraisha sijui hata nikupe zawadi gani?" ... Aisha aliongea kwa furaha huku akiwa anaendesha gari kwa kasi. 
Ndani ya nusu saa Aisha alikuwa ameshafika alipo Dr Ally alifika na kumkumbatia kwa furaha ... "Nakupenda sana Aisha naitaji unipe cheo ndani ya moyo wako" ... Dr Ally alimwambia Aisha huku akimtazama usoni ... "Nakupenda pia Ally ... Wewe ndyo mmiliki wa moyo wangu".. 
Baada ya kusalimiana walikaa chini na kuongea ... "Nimefurahi sana kusikia unataka kumtimua yule Malaya, kiukweli nilikuwa simpendi na nilitamani hata kumfanyia jambo baya" ... Aisha alimwambia Dr Ally huku akiwa mwenye furaha ... "Samahani kwa yote Mpenzi wangu ila mimi hakuwa mpenzi wangu isipokuwa nilitaka kumsaidia tu" ... "Ok tuachane na hayo vp kuhusu hizo pesa zako mpenzi wangu?" ... "Sasa unafikiri tutafanyaje na tukisema twende polisi, hakuna jambo dogo nao watataka pesa na watatusumbua" ... "Yule Mtoto mdogo tu, polisi tukafanye nini?" ... "Sasa tunafanyaje ili tupate pesa zetu?" ... Dr Ally alimwambia huku akimsogelea na kumsikiliza kwa makini ... "Tumteke na tumpeleke porini tukamtese atasema tu alipozificha" ... Aisha alitazama watu na kuongea kwa sauti ya chini ili waliokuwa pale ktk ule mgahawa wasiwasikie ... 
Dr Ally alistuka na kumtazama kwa makini, kisha akamuuliza ... "Nani atakayefanya kazi hiyo?" ... "Mimi naweza kufanya kazi hiyo na vijana ninao mpenzi wangu. Nafanya yote kwa sababu nakupenda Ally" ... Aisha aliongea kwa sauti ya upole baada ya kuona Dr Ally amemkazia macho. 
Masikini Aisha alikuwa hajui kama ametegewa mtego na kujikuta akilopoka .... "Upo chini ya ulinzi Aisha weka mikono yako juu" ... Kumbe wale waliokuwa wakiendelea na mambo yao wakijifanya wote wapo busy nao walikuwa mapolisi. 
Aisha hakuamini kilichotokea pale, macho yalimtoka na machozi ya uchungu yalimmwagika ... "Ally hata wewe?" ... Aisha aliongea kwa uchungu huku akimtazama Dr Ally ... "Nakupenda sana Aisha ila kwa ili sipo pamoja nawe ... Usalama wako ni pale utakapoweza kusema wapi Poshie alipo ... Unamuonea sana yule binti hana kosa lolote, kama wewe ungekuwa yeye ungejisikia raha kuishi maisha anayoishi Poshie??" 
NINI KITAENDELEA?? ... 
Nini hatma ya Poshie?? Je amekufa? Angelo atamuona Poshie .... 

Comments

Popular posts from this blog

SMS 47 ZA MAPENZI ZITAKAZO MNYEGEZA** MPENZI WAKO

KWANINI WADADA WENGI WAREMBO NA WANAOJIONA WAREMBO HUCHELEWA KUOLEWA,HUKOSEA KUOLEWA AU KUTOOLEWA KABISA?SOMA HAPA

HATUA ZA KUCHEZEA KIHARAGE NA KISIMI