KOVU LA MOYO 39




&t;br /> 
Chozi la uchungu lilimmwagika Aisha hakuamini kabisa kama Dr Ally anaweza kumgeuka na kumfanyia alichomfanyia.... 
"Nashukuru sana Ally kwa ulichonifanyia ila naomba utambue kuwa nimefanya yote kwa sababu yako ... Nakupenda na nitaendelea kukupenda" ..... Aisha aliongea kwa uchungu akimwambia Dr Ally lakini ndiyo hivyo tena alikuwa mikononi mwa polisi 
Alichukuliwa kwa mahojiano zaidi lakini alikana kuhuusika na kupotea kwa Poshie wala hajui chochote kuhusu hao watu waliomteka japokuwa alimwambia Dr Ally pale kuwa yeye ana watu wa kazi na wanaweza kuifanya kazi ya kumteka Poshie na akarudisha pesa aliyoiiba .... "Sikiliza nikuambie Binti, huu muda unaonipotezea utakuja kuujutia, ni bora ukasema kabla sijaamua kukupeleka wanapopelekwaga watu vibuli na wakaidi kwa sababu nakuona wewe ni Msichana mdogo sana na isitoshe wewe ni Mrembo sana" ... Afande Mmoja mwenye sura ya upole alijaribu kuongea na Aisha baada ya kukana kuwa yeye hausiki na upotevu wa Poshie .... "Mimi Sijui chochote Afande kama ningejua kwanini nisingekuambia tokea mwanzo?" ... "Afande hataki kusema naomba umchukue na umpeleke chuo cha mafunzo akakutane na wafunza adabu" ... Baaada ya amri ile kutolewa Aisha alitolewa pale na kupelekwa katika chumba maalum 
"Nasema Afande naomba unifungulie" ... Aisha alipiga kelele baada ya kupata maumivu makali ambayo hakutegemea kuyapata .... Alilia sana baada ya kuona anateseka juu ya Dr Ally na mbaya zaidi aliyemfanya ateseke ndio huyo huyo aliyemchoma na kumfanya akamatwe 
Wivu ni kipimo cha mapenzi kwa umpendaye na akupendaye lakini wivu unapozidi sana matokeo yake yanakuja kuwa mabaya .... Aisha alimchukia Poshie na kutaka kumfanyia ubaya kisa wivu kwa kumuhisi kuwa anatembea na mpenzi wake, kumbe wapi., Dr ally alijitolea kumsaidia Poshie kama Dada yake (Sijui Tunajifunza ndugu zangu?) 
Baada ya kukubali kuwa yeye ndiye aliyemteka Poshie na kumpeleka Porini ili kumfanyia ubaya, Mapolisi walimchukua ili kuwahi kule alipomfanyia ubaya Poshie. 
Wakati anatoka ndani kuja kupanda gari la polisi alikutana macho kwa macho na Dr Ally akiwa anasubiria majibu ya ndani kama kweli Aisha amehusika na kupotea kwa Poshie au lah ... Aisha alimtazama kwa jicho la uchungu Dr Ally huku anapanda katika ile gari ya Polisi ... "Vipi amesemaje?" ... Dr Ally alimfuata rafiki yake wa karibu ambaye naye alikuwa ni mmoja kati ya wapelelezi wa ile kesi na kumuuliza .... "Inabidi ukaze moyo Ally bado tupo katika uchunguzi, ila wamemteka na kwenda kumfanyia kitu kibaya sana" ... Yule mpelelezi aliongea na kuvuta hisia kisha akamwambia ... "Wamemuua" ... Dr Ally alistuka na palepale akaanguka na kupoteza fahamu 
****** 
Kila binadamu anavuna alichopanda, muda mwengine mungu anakulipia kwa yale uliyofanya hapa Duniani ukiwa hapa hapa Duniani. 
Maisha ya Angelo yalibadilika ghafla na hakuwa Angelo yule ambaye ulikuwa unamjua wewe ... Pesa ya kula kwake ilikuwa ni mtihani mkubwa sana na hakuwa na uwezo tena wa kufanya japo kibarua cha kumuingizia ridhiki ... Ndoto zake za kumpata Poshie na waje kupata tabu kama alivyokuwa amepanga hapo hawali zilikuwa zinaingia doa kila kukicha ... hakujua wapi alipo Poshie na vipi atampata ... Mguu aliokatwa hospital ulichangia kumfanya yeye ashindwe kutimiza ndoto zake za kumpata Mpenzi wake. 
Kazi pekee aliyokuwa na uwezo wa kuifanya kwa ufanisi mkubwa ni kuomba katika makutano ya barabara ... Angelo alikuwa mchafu na kidonda kilikuwa akijapona vizuri, kama moyo wako mdogo husingeweza kukaa na Angelo japokuwa hata dakika 10 ... Siku hiyo mvua ilikuwa imenyesha kubwa na mbaya zaidi Angelo ilimnyeshea sana hakubaatika kumpata mtu yoytote yule ambaye anaweza hata kumuomba Tsh 200 ili akapate angalau muogo wa kuchoma .... 
Kidonda chake alikifanya mtaji ili watu wamuonee huruma wamchangie chochote kitu apate pesa ya kula. Muda mwingine alikuwa akilazimika kukichubua ili kiwe kibichi na watu wamuonee huruma .... "Poshie Mpenzi wangu!! wapi ulipo mpenzi wangu? Nimekutafuta kwa muda mrefu mpenzi wangu ili tuje tuishi pamoja, najua unateseka na mtoto lakini mumeo nimejirekebisha ili nije kukusaidia kukilea hicho kiumbe kisicho na makosa" ... Angelo aliongea mwenyewe baada ya kuona maisha yamemshinda. Alijua fika kuwa akirudi kwa Poshie na kwa jinsi Poshie alivyo katika kutafuta maisha anaweza kumsaidia ili na yeye akapumzika na shida za dunia ... 
Muda mwingine maisha aliyoyaishi kwa muda mchache aliona kama alikuwa ndotoni na alikuwa akitamani kurudishiwa kila kitu chake ili akarekebishe makosa yake likiwemo la kumtimua Poshie na kumkana kama hamjui .. 
Hapa tujifunze kuwa Radhi si kwa wazazi pekee muda mwingine hata kwa mpenzi wako ambaye mmepata tabu katika maisha na ukamuhaidi baadhi ya vitu na wewe ukaja kumgeuka na mwenzako akawa na kinyongo na wewe basi tambua kuwa hautokuja kufanikiwa kamwe ... {Kama utakuwa na kumbukumbu nafikiri tuliona Angelo baada ya kutimuliwa kwa kina Robby alienda kulala kiwanjani na Poshie na hapo alinusulika kifo baada ya kuiba mfuko wa mtoto wa maandazi na aliporudi kwa Poshie alimwambia kuwa ikitokea siku mimi nikakuacha wewe basi ardhi ifunguke na inimeze' ... Leo kamsaliti na kapoteza kila kitu katika maisha yake ... Chunga sana kauli zako unazoongea na mpenzi wako mkiwa faragha" 
Baada ya kunyeshewa sana na Mvua Angelo alijisogeza katika duka moja na kujibanisha hapo ili kujikinga na mvua ... akiwa hapo mara akaja mtu dukani na kutoa pochi ili kupata maitaji .... Tamaa ilimshika Angelo na kutaka kumuibia yule jamaa Pochi ... yule kijana aligeuka na kumkamata Angelo na akaanza kumshushia kichapo ... Wananchi wenye hasira kali waliongezeka na kumpiga Angelo na kutaka kumuua kabisa ... akiwa hajitambui kabisa Mapolisi walijitokeza na kumnusuru na kifo hicho ... Haraka walimbeba na kumkimbiza Hospital huku wakihisi kuwa ameshakata roho 
******* 
Aisha aliwachukua na kuwapeleka kule walipomfanyia unyama Poshie ... Lakini cha ajabu baada ya kufika kule hawakuikuta kabisa Maiti ya Poshie ... "alikuwa hapa" ... Aisha alionesha huku akiogopa ... "sasa hapa yupo wapi., Binti tunaomba utuoneshe kabla hatujakufanyia kitu kibaya" .... "Afande mmoja alimwambia Aisha kwa hasira huku akimminya masikio yake .... "Afande kuna Binti ameokotwa maneo haya na kupelekwa Hospital ya Taifa hakiwa hajitambui huku akiwa amepata majeraha na kung'olewa meno" ... Afande mmoja alileta taharifa na haraka wakaondoka eneo hilo kwenda kuthibitisha taharifa hizo kama ni za kweli au la 
******* 
Baada ya kurudi Uganda Robby alikuwa na lengo moja tu, nalo ni kuwatafuta Poshie na Angelo na kuwapatanisha na warudi katika mapenzi yao ... Kila siku alikuwa kiguu na njia na picha yake akiwatafuta mitaani kama anaweza kuwapata .... ilimchukua takribani wiki lakini hakubaatisha hata kumpata mmoja wao. 
Siku hiyo akiwa njiani anawatafuta mara akapigiwa simu na kuambiwa kuwa Mama yake ameanguka na kuzidiwa hivyo hali yake mbaya na anakimbizwa Hospital .... Robby alitoka mbio na kuwahi Hospital ili kwenda kumuona Mama yake 
Alifika Hospital huku akiwa amechanganyikiwa na hajitambui kabisa ... Mipango yake ni hasome na kumsaidia Mama yake kwa sababu yeye hakuwa na Baba katika maisha yake ... Alifanikiwa kuingia Wodini ambapo kulikuwa kumelazwa watu mahututi.... Ile anaingia Tu hakuwezsa Kuamini macho yake baada ya kumuona Poshie akiwa amelazwa hajitambui.. 
Alistuka na chozi la uchungu likamtoka baada ya kumkuta rafiki yake akiwa katika hali ile alitamani kuongea nae lakini Poshie alikuwa ajitambui na ghafla alikuja kuamishwa na kupelekwa katika chumba cha uangalizi maalimu kwa sababu alionekana kupumilia mashine maalum ya hewa na hali yake ilikuwa mbaya zaidi 
Robby alichanganyikiwa kiasi ambacho hata alikuwa amepitiwa Nini kilimpeleka pale .......... "Robby umemuona rafiki yako? Yupo kule katika wodi ya wanaume na sidhani km atapona" ... Dada mmoja ambae alikuwa ni mpangaji wao kumbe alimuona Angelo akiletwa pale ... Haraka Robby alienda na hakuamini macho yake baada ya kumuona Angelo akiwa katika hali ile huku akiwa na pingu mkononi na mwili mzima ukiwa umetapakaa damu .... Alishindwa kujizuia na kujikuta chozi la uchungu likimdondoka ...... 
NINI KITAENDELEA?? ...... TUKUTANE KATIKA EP YA 40 NA YA MWISHO 

Comments

Popular posts from this blog

SMS 47 ZA MAPENZI ZITAKAZO MNYEGEZA** MPENZI WAKO

KWANINI WADADA WENGI WAREMBO NA WANAOJIONA WAREMBO HUCHELEWA KUOLEWA,HUKOSEA KUOLEWA AU KUTOOLEWA KABISA?SOMA HAPA

HATUA ZA KUCHEZEA KIHARAGE NA KISIMI