Serikali ya Jamhuri ya Kenya imeandaa mpango maalum wa kuwapa ruzuku watu wenye mahitaji maalum walio kwenye hatari zaidi, walioathirika zaidi na mlipuko wa virusi vipya vya corona (covid-19).

Wizara ya Kazi imeandaa mpango huo kupitia mfuko maalum na wataanza kutoa fungu hilo katika kaunti nne zilizoathirika zaidi. Taarifa ya wizara hiyo imetaja Nairobi, Kwale, Kilifi na Mombasa ambazo kwa sehemu nyingi watu wamezuiliwa majumbani au kukataza mizunguko.

Rais Uhuru Kenyatta alipiga marufuku mizunguko katika maeneo mbalimbali nchini humo, hususan katika kaunti hizo nne kwa siku 21, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kupambana na kusambaa kwa virusi vya corona.

Wizara hiyo imesema kuwa inaendelea kutambua na kuchambua waliothirika zaidi ambao pia ni watu wenye mahitaji maalum walio kwenye hatari zaidi. Pia, maeneo yaliyoathirika zaidi ili kufanikisha mchakato wa kutoa mafungu hayo.

“Lengo ni kuanza na kaunti ambazo zimeathirika zaidi kabla hatujaingia kwenye kaunti zote 47,” alisema Simon Chelugui, Katibu katika Wizara hiyo, akisimamia Kazi na Ulinzi wa Kijamii.

Pamoja na mpango huo, Serikali ya Rais Kenyatta awali ilitangaza hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kupunguza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na kodi katika mishahara (PAYE).

Hadi jana, Kenya ilithibisha kufikia visa 296 vya corona, 14 wakiwa wamefariki na 74 wamepona, kwa mujibu wa Waziri wa Afya wa Kenya, Dkt. Mercy Mwangangi.

Comments

Popular posts from this blog

SMS 47 ZA MAPENZI ZITAKAZO MNYEGEZA** MPENZI WAKO

KWANINI WADADA WENGI WAREMBO NA WANAOJIONA WAREMBO HUCHELEWA KUOLEWA,HUKOSEA KUOLEWA AU KUTOOLEWA KABISA?SOMA HAPA

HATUA ZA KUCHEZEA KIHARAGE NA KISIMI