Washukiwa 44 wa kundi la Boko Haram wakutwa wamefariki katika jela Chad



Kundi la watuhumiwa 44 wa wapiganaji wa jihadi wa Boko Haram wamepatikana wakiwa wamefariki wakiwa jela katika mji mkuu wa Chad N'Djamena jana, shirika la habari la AFP limeripoti , likinukuu maafisa wa polisi.

Waliofariki ni miongoni mwa washukiwa wa kundi la wapiganaji wa jihadi 58 ambao walikamatwa katika operesheni ya hivi karibuni dhidi ya Boko Haram iliyofanyika karibu na ziwa Chad, mwendesha mashitaka wa nchi hiyo Youssouf Tom alisema katika televisheni ya taifa.

Alisema kuwa kufuatia mapigano katika eneo la ziwa Chad, wanachama 58 wa kundi la Boko Haram walikamatwa na kupelekwa N'Djamena kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi.Tom alisema kuwa asubuhi ya Alhamis , wafanyakazi wa jela waliwaambia kuwa wafungwa 44 wamekutwa wamefariki katika chumba walimofungiwa.

Uchunguzi wa kufahamu vipi watu hao walifariki unaendelea, mwendesha mashitaka alisema. Uchunguzi wa miili minne ya watu waliofariki umekwisha fanyika.

Maafisa wa jela wanashuku kwamba wafungwa hao walijidunga kitu hatari ambacho kinasababisha matatizo ya moyo na kupumua.

Comments

Popular posts from this blog

SMS 47 ZA MAPENZI ZITAKAZO MNYEGEZA** MPENZI WAKO

KWANINI WADADA WENGI WAREMBO NA WANAOJIONA WAREMBO HUCHELEWA KUOLEWA,HUKOSEA KUOLEWA AU KUTOOLEWA KABISA?SOMA HAPA

HATUA ZA KUCHEZEA KIHARAGE NA KISIMI