Posts

Virusi Vingine Vipya vyaua Mmoja China, 32 Wapimwa

Image
Mtu mmoja ambaye alithibitishwa kuwa na maambukizi ya Hanta Virus amefariki dunia akiwa kwenye basi katika Jimbo ya Yunnan. Abiria wengine 32 waliokuwa kwenye basi hilo wamefanyiwa vipimo kuona kama wameathirika.  Kifo hicho kimekuwa gumzo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kutokana na wengi kukifananisha na Corona Virus, ambayo pia ilianzia China.  Imeelezwa kuwa, Hanta Virus husambazwa na Panya wenye Virusi hivyo na ni vigumu kwa watu kuambukizana.  Kwa mujibu wa Kituo cha kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Marekani (CDC), mtu anaweza kuambukizwa pale anaposhika macho, pua au mdomo wake baada ya kushika haja, mkojo au mate ya Panya.

Did Mwana FA Lie About his Coronavirus Positive Status? He Speaks!

Image
Mwana FA recently announced that his coronavirus tests came in positive after jetting in to Tz from South Africa; where he had travelled for business.  In his video, the father of two revealed that he was not feeling all well while leaving South Africa; and immediately after arriving in Tz, he went straight to run the coronavirus test just to be sure about his status.  Fortunately his results came in as soon as possible, a move that helped him protect his loved ones as he did not come into contact with any of children or family members.  Faking sickness However word on most Tanzanian gossip tabloids is that the rapper lied about his status – just to catch everybody’s attention and of course a pity party of him!  Fans went on to criticize him for acting like the sickness was not dangerous yet they were aware of the cases of deaths back in Europe.  According to most, Mwana FA’s don’t care attitude might have just confirmed that he either lied about his status; or ...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke...Wengi Hudhani ni PESA...Kumbe Wanakosea

Image
   WANAUME wengi wanaamini wanawake, kwa kawaida, ‘wanapenda hela.’ Kwamba ukiweza kumhakikishia mwanamke 'uhakika wa kiuchumi' unakuwa umemaliza. Ingawa hatuwezi kupuuza ukweli kuwa uhakika wa 'kiuchumi' ni moja wapo ya mahitaji ya mwanamke, lakini si sahihi kuamini kuwa moyo wa mwanamke unaweza kuthamanishwa kwa fedha.  Fikra hizi walizonazo wanaume [kuwa anachokihitaji mwanamke ni fedha] zimeleta matatizo mengi katika mahusiano na ndoa. Kwa mfano, wapo wanaume ambao baada ya kuhakikisha wenzi wao wamepata mahitaji ya msingi, basi wanawatelekeza kihisia. Hali hii husababisha upweke mkubwa kwa wanawake hawa wanaojikuta hawana mtu wa karibu kuwasikiliza isipokuwa vitu.  Upweke, kwa hakika, huzaa migogoro isiyokwisha inayowafanya wanaume [ambao kimsingi ndio wasababishi wa upweke huo] washindwe kuwaelewa wanawake. Kwa mtazamo wao, ni vigumu kumridhisha mwanamke. Wengine wanaenda mbali na kufikiri , 'mwanamke ni kiumbe mgumu kueleweka' kwa sababu, ‘hata ufanye nin...

WHO: Marekani huenda ikawa kitovu kipya cha COVID-19

Image
Shirika la Afya Ulimwenguni – WHO limesema kuwa Marekani huenda ikawa kitovu kipya cha ulimwengu cha mlipuko wa virusi vya corona baada ya idadi ya visa vya ugonjwa huo kupanda kwa kasi nchini humo. Image result for WHO Margaret Harris us may be became Msemaji wa WHO Margaret Harris amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kuwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita, asilimia 85 ya visa vipya vimetokea Ulaya na Marekani. Kati ya visa hivyo, asilimia 40 ni vya kutokea Marekani. Kimataifa, idadi ya visa vilivyothibitishwa vya virusi vya corona imepindukia 337,000 kote katika nchi 194 kufikia leo asubuhi, kwa mujibu wa takwimu za shirika la habari la Reuters, huku kukiwa na zaidi ya vifo 16,500 vinavyo husishwa na virusi hivyo. Kwa mujibu wa chombo cha habari cha DW, Nchi ya China imetangaza leo kuondoa vikwazo vya usafiri katika eneo ambalo lilikuwa kitovu cha janga la virusi hivyo, wakati serikali kote duniani zikiimarisha hatua za kuwazuia watu kusafiri.

Diamond Platnumz Awa Msanii wa Kwanza Afrika Kufikisha Views Milioni 900 YouTube

Image
Habari njema kwa wapenda maendeleo. Maendeleo hayana Team kwa sauti ya Magufuli. Habari njema ni kwamba kijana anae liwakilisha Taifa letu katika Tasnia ya muziki kajiandikia historia ya kuwa msanii wa kwanza Afrika kufikisha views 900m You tube.  Nafikiri kuna haja ya watanzania wote kuheshimu mchango wa ndugu yetu huyu bila kujali team za mitandaoni. Nasikitika sana kuona wasanii chipukizi wakilewa sifa wanapo linganishwa na Diamond bila ya kutafakari mafanikio aliyoyafikia Chibu katika muziki. Hivi indicators zote hizi hawazioni na kutambua kuwa katika nchi yetu huyu yupo level ya pekee?

Mtoto Kaiva Sana..Tazama Picha za Tanasha Donna Baada ya Kuachana na Diamond Platnumz

Image
Mwezi mmoja baada ya Tanasha Donna kuachana na staa kutoka Tanzania Diamond, kichuna huyu sasa amerejea mitandaoni na picha na kuacha wengi wakidondokwa mate akidhihirisha urembo aliobarikiwa nao kutoka kwa Mola.  Tanasha ambaye anafahamika sana kutokana na Wimbo wake ‘GERE’ alioufanya na Diamond amekuwa mitandaoni akisemwa kufuatia mishe mishe zilizokuwa  zinakumba uhusiano wake na msanii huyo.  Hizi hapa ni baadhi ya picha ambazo kichuna huyu ametundika katika mitandao ya kijamii.  Kutokana na mkurupuko wa virusi vya Corona, Tanasha kama wasanii wengine ametuma ujumbe katika mitandao ya kijamii akiwataka wananchi kuzingatia usafi kama njia ya kujiepusha na virusi hivyo

Jack Wolper Atamani Kuzaa Mtoto, Ataja SIFA za Mwanaume Anayetaka Kuzaa Naye

Image
Msanii wa filamu na mfanyabiashara Jacqueline Wolper, amekiri kusema anatamani kuwa na mtoto kwa sababu umri unaenda ila bado hajajua nani atakuwa Baba wa kuanzisha naye familia.  Msanii huyo ameyasema hayo kupitia video fupi aliyopost katika akaunti yake ya mtandao wa Instgram, ambapo amevitaja vigezo vya mwanaume anayemtaka.  "Nataka niwe na mtoto, unajua umri unakwenda lakini nani atakuwa ndiyo baba, vigezo namba 1 mpaka 4"  1. Asiwe tajiri  2. Awe mchapakazi ajue kazi na asichague kazi, hata nikimwambia leo tunaenda Kariakoo shimoni kuna deal ya nyanya zimetoka tukanunue, tuuze tupate pesa awe tayari kwa kifupi asiwe bishoo.  3. Awe ana hofu ya Mungu, asiwe anavuta sigara wala unga kilevi chochote ruksa, asiwe staa wa kabila lolote wala dini yoyote.  4. Awe msafi muda wote asiwe na mtoto umri miaka 30 na kuendelea, urefu ufupi uzuri siyo tatizo, muhimu vigezo uwe navyo haijalishi uwe mbaya au la, maana sipendi wanaume wazuri haijalishi una kazi au hauna...