Posts

Showing posts from May, 2020

Shemeji hiyo mitego yako dawa Yako iko Jikoni

Image
sana amani ndio maana huwa najisikia vibaya sana ikitokea nimemkwaza mtu wangu yoyote wa karibu kwani najiuliza atanisamehe kweli kwa hili kosa nililomfanyia? Historia ya maisha yangu imenifanya niwe na moyo huu wakutopenda kumkwaza mtu kwani nimefadhiliwa sana na kaka yangu,nimepewa kila kitu muhimu ambacho kijana anastahili awe nacho kama vile simu nzuri,pesa ya matumizi achilia mbali ada ya masomo ya shule za private nilizosoma kuanzia kindergarten mpaka nimefika chuo kikuu,Kwa kweli kaka yangu ni mtu wa pekee sana maishani mwangu na hakika siwezi kulipa fadhila zake. Ameniamini sana kiasi cha kuwaananiachia gari lake anaposafiri niwehuru kulitumia muda wowote nitakao lakini kwa bahati mbaya moyoni nimekuwa mwenye huzuni sana kwani mke wa kaka yangu yaani shemeji amekuwa tatizo kila kaka akisafiri maana vituko anavyonifanyia sio siri nahisi kutamani kuhama kwake pasipohata kujua nitaenda wapi.  Shemeji anathubutuje kunitolea chozi akinililia eti anataka niwe namimi kimapenzi wakati

Sad Story:Siwezi Wachukia Wanawake wote..Ila Wamenitenda Sana

Image
Mimi ni kijana wa kiume nina miaka 24, makazi yangu ni jijini mwanza,nimeamua kushea story yangu ili niweze kupata ushauri kwa watu mbali mbali juu ya nini nifanye baada ya kutendwa katika kila uhusiano ninao anzisha naweza nikasema nilichelewa kidogo kujihusisha na mapenzi kwa mujibu wa Dunia ya sasa,na hii ni kwa sababu nimelelewa na kukua katika familia yenye maadili.  Siwez nikasema nina mvuto mkubwa saana , niko simpo tu kama profile pictures zangu zinavyojieleza lakini siku zote nimejikuta nikiwa kipenzi cha kinadada wengi kulingana na mazingira husika ntakayokua nikiishi, na binafsi me ni mwanamume mtanashati naejpenda sana, mpole na zaid ni mcheshi haswa pengine hizo ndiyo sababu..na story yangu ya mahusiano inaanza nikiwa na miaka 20,kipindi nilipojiunga katika chuo kimoja hapa mwanza.  Baada ya kufika pale chuoni nilijijengea idadi kubwa tu ya marafi na kama unavyojua mtu mcheshi hua ana malafiki wengi ,pamoja na hayo, ckua na mawazo kabisa ya kuwa na msichana k

Nani ni Muhimu Katika Maisha yako? Soma Hichi Kistori Kifupi cha Kufundisha

Image
Siku moja katika darasa la jioni la watu wazima, mwalimu wa saikolojia aliingia darasani na kuwaambia wanafunzi;  "Nataka tucheze mchezo, mtu yeyote yule naomba ajitolee aje hapa mbele" Mwanamke aitwae Cathy akatoka mbele. Mwalimu akamwambia aandike majina 30 ubaoni ya watu ambao anadhani ni wa muhimu katika maisha yake.  Cathy akaandika majina ya wanafamilia yake yaani mumewe na mwanae, ndugu, majirani na marafiki zake.  Mwalimu akamwambia Cathy afute majina matatu ambayo anadhani kwake sio ya muhimu sana kuzidi mengine. Cathy akafuta majina ya marafiki zake watatu.  Mwalimu akamwambia Cathy afute tena majina matano zaidi, Cathy akafuta majina ya majirani zake watano.  Hii iliendelea mpaka alipobakiwa na idadi ya watu wanne tu katika ubao. Haya yalikuwa majina ya wazazi wake, mumewe na mtoto wake wa pekee.  Darasa zima wakabaki kimya, baada ya kugundua kuwa huu sio mchezo wa Cathy peke yake sasa.  Mwalimu akamwambia Cathy afute majina mengine m

Fahamu Historia ya Condom..Ilipoanzia na Jinsi Ilivyogundulika na Kuanza Kutumika kwa Mara ya Kwanza..!!!

Image
KONDOMU ni kifaa/ zana iliyotengenezwa mahususi kuvalisha uume au kuwekwa ukeni wakati wa kujamiiana.Nazo hubana kutokana na umbile la uume au uke.  Kondomu hizi zipo za aina tofauti kutokana na muda na vipindi zilipotengenezwa, nazo ni kama ifuatavyo:-  Awamu ya I – zilizotengenezwa kwa mimea.  Hizi zilitengenezwa mahususi kama kinga dhidi ya maambukizo ya vimelea vya ugonjwa wa kaswende [ugonjwa wa kifaransa]  Awamu ya II – kutokana na utumbo wa kondoo.  Dr. Condom alifahamika kama mgunduzi wa kondomu hizi, naye alikuwa ni dakatari wa Mfalme Charles II.  Alimshauri Mfalme kutumia kama kinga kutokana na magonjwa ya zinaa kutokana na tabia yake ya kuwa na wanawake wengi nje ya ndoa yake.  Awamu ya III – kutokana na mpira  Hizi zilitengenezwa kwa urahisi na kwa wingi na zikawa ndizo pekee zenye uwezo wa kudhibiti mimba hadi miaka ya 1960 vilipogunduliwa na vidonge vya majira.  JE KONDOMU NI SALAMA?  Tunaelezwa kuwa kondomu hutengenezwa kwa ustadi mkubwa ki

Je, Una Malengo gani Katika Maisha?

Image
Je, leo unapofikiria maisha yako yaliyopita, unafurahi na kuridhika kuwa uliyaendesha vizuri au hauridhiki? Watu wengi husikitika hadi wakasema kama wengebahatika kupata nafasi kurudia maisha, wasingeishi kama walivyo sasa. Wanasema wangekuwa makini zaidi katika kupanga maisha yao ili kuyafanya yawe bora zaidi. Huenda hata wewe unafikiria hivyo. Lakini duniani tunaishi mara moja tu wala hatutarudi tena baada ya kufariki. Hivyo nafasi tulitonaayo ndiyo hii ya kurekebisha maisha yetu. Na wala hatujachelewa. Je tunawezaje kufanya maisha yetu yaliyosalia kuwa bora? Hebu tushirikiane kutaafakari kisa hiki tuone kama kitatusaidia kuboresha maisha: Kijana aliyemaliza chuo kikuu alikwenda kwa mwanafalsafa kumuomba amsaidie kuamua kazi itakayomfaa zaidi. Yule mwanafalsafa akamuuliza “ Kwani wewe unataka kazi gani?” Kijana akajibu, “ Nimekuja kwako kwa sababu sijui cha kufanya” Mwanafalsafa akamwambia Mimi sitaweza kukusaidia kama wewe mwenyewe hujui nini unachotaka. Labda fikiri na uniambie baa

Mwanaume Kama Huna Pesa na Unataka Usife Mapema, Usifanye Hivi

Image
Kama wewe ni Mwanaume na unamalengo ya kuoa ila huna Pesa, hakikisha usioe mwanamke kisura. Kila mwanaume anatamani kumiliki mwanamke kisura kiasi kuwa kila atakapokuwa anapita haoni shobo kumtambulisha mkewe. Tatizo linakuje pale huna pesa lakini unataka uweke mrembo ndani. Ndugu yangu, usijidangaje hata siku moja kuwa wapo wanawake wasiopenda pesa na wanapenda maisha ya shida. Hata kama wewe ni Handsome kiasi gani, hakuna mwanamke aliye tiyar kuishi maisha magumu na wewe kisa uhandsome wako. Labda yeye akuowe wewe. Na ukiolewa zipo gharama zake. Sasa ukitaka kufa kwa presha na ma stress, kaowe mwanamke mrembo na huku unajijua ni kapuku kama mimi apa.

Mjue Mnyama NGEKEWA , Mnyama Anayeongoza Kwa Kupendwa na Wanyama Wengi Duniani

Image
Huyu ndiye mnyama anayeongoza kupendwa na wanyama wengi zaidi duniani, anapokaa huzungukwa na viumbe wengi tofauti kiurafiki. Hupatikana zaidi Marekani Kusini na Kati Analiwa na wanyama wachache sana, haswa aina fulani ya mamba ‘caiman’, chui aina ya ‘Ocelot’, jagwa, puma, tai na nyoka wakubwa kama Anaconda. Adui yake mkubwa zaidi ni binadamu ambaye humla na kutumia ngozi yake kwa sababu za kiimani Huyu ni mnyama jamii ya sungura, anaweza kufikia Kg 75 akiwa mkubwa, na urefu wa mita 1.4. Ana uwezo wa kukaa ndani ya maji kwa dakika 5. Maisha yake ni maeneo yenye majani mengi yaliyo karibu na maji Anaishi kwa kula majani yaliyo nchi kavu, yaliyo ndani ya maji na viumbe wa baharini kama majani yakiadimika. - Ngekewa asubuhi hula kinyesi chake ili kupata ‘virutubisho’. Iliaminika mtu akiwa na kipande cha ngozi ya mnyama huyo anakuwa anapendwa na wengi, ndio sababu wanaopendwa huambiwa 'una ngekewa'

Kila Mwanaume Anaye Lala na Mimi Harudii Tena na wala Simu zangu Hapokei

Image
Mimi  ni  mwanamke.Naomba msaada wa  mawazo  maana  sijui nina nini mimi... Umri unanitupa mkono maana nakaribia miaka 35 lakini sijampata aliyewahi kunitangazia ndoa.Cha ajabu kila anayelala na mimi siku ya pili harudii tena na hata nikimpigia simu hapokei Hapo ndo linapoanzia tatizo na  kunifanya nijisikie vibaya...Saivi  hata mtaani nachagua kwa kupita... Kuna mwanaume mmoja huyo ndo aliwahi kunichana live kuwa nina maji mengi na MAMBO  yangu ni kubwa kiasi kwamba ha piz hadi amfikirie mpenzi wake wa zamani... Jamani naomba msaada nifanyaje mie. Je kuna dawa ya kupunguza haya maji na kuifanya hii MAMBO  iwe  ndogo? Hide My Name.

Ifahamu Tamaduni Hii ya Kupasua Midomo

Image
Jamii moja katika kisiwa cha Phuket  kusini mwa Thailand imeendesha tamasha la kitamaduni na la kidini linalojulikana kwa jina la ‘Taoist’ kwaajili ya kujitakatisha dhidi ya madhambi, ambapo washiriki husheherekea kwa kujichoma mishale, visu  na mapanga katika mashavu yao. Tamasha hilo lenye asili ya China hufanyika mwezi Oktoba kila mwaka, ambapo tamasha la mwaka huu limefanyika kuanzia 9, Oktoba likihudhuriwa na jamii kubwa ya Wachina wanaoishi katika eneo hilo . Moja ya matukio ambayo hufanyika katika tamasha hilo ni pale ambapo mtu mmoja hujichoma visu vingi vikali katika mashavu yake na mwingine hushikilia kichwa chake na kukata ulimi wa mtu huyo kwa kutumia shoka, na kumwacha akibubujikwa na damu kifuani. “ Watu hao waliokatwa vitu vikali ni miungu ambao hutembea ardhini wakionesha miujiza yao pamoja na vipande vya nyama vilivyokatwa, ili madhambi ya watu wao yasafishwe”, amesema Pathompong Reanthong, ambaye ni mmoja ya waandaaji. “ Malengo ya sherehe hii ni kwaajili ya watu kuon

Sababu na athari zitokanazo na kitambi

Image
Utafiti  umegundua  kwamba  kuna  idadi  kubwa  sana  ya wanawake  na  wanaume  wanao  sumbuliwa  na  tatizo  la  kuwa  na matumbo  makubwa  kiasi  ama  vitambi  kwa  lugha  nyingine. Uchunguzi wetu  umetuwezesha  kubaini  kuwa  katika  watu  kumi  wanao  tembea bararani  angalau  watatu  kati yao  wanasumbuliwa na  tatizo la kitambi. Sababu  kuu  za tatizo la  kitambi  ni  pamoja  na; Ulaji  mbovu  wa  vyakula ( Ulaji usio zingatia  mlo  kamili ). Ulaji  mbovu  wa  vyakula  unajumuisha   ulaji  wa  vyakula  vya  aina moja  kwa  wingi  kupita  kiasi  bila  kuzingatia  aina  nyinginezo, mfano  ulaji  wa  vyakula  vya  mafuta  mafuta  kwa  wingi kupita kiasi. Unywaji  wa  pombe  kupita  kiasi Kutofanya  mazoezi  ya  mwili  na  viungo pamoja  na  sababu  nyinginezo. Athari  za  tatizo  la  kitambi  ni  pamoja  na : Kuwa  katika  hatari ya  kushambuliwa  na  magonjwa  ya  hatari kama  vile  kisukari, moyo  na  presha. Kutokuwa  na  uwezo  wa  kumudu  tendo  la  ndoa (  kwa  wanaume ) Kupun

Mrembo Afunguka "Nimejaliwa Umbo Zuri na Mungu Hivyo sio Dhambi Kuwaonyesha Watu'

Image
Pichani mrembo huyo kwa jina la Anita amesema kamwe hawezi kuomba radhi sababu ya kujaaliwa umbo lenye mvuto . Ameyasema hayo Kwa hasira akimtuhumu mmoja wa mashoga zake wa karibu kumsengenya kwa watu kuwa muda mwingi anatupia videos mtandaoni Ili kuwaonesha watu umbo lake . . Anita amesema kinachomsumbua rafiki yake huyo ni Wivu wa kutamani umbo lake angepewa yeye kwani Kama Ni videos hata mrembo huyo Pia anatupia Kwa kujifichaficha mtandaoni. Amemalizia Kwa kumwambia ashukuru hapost videos chafu Ila ataendelea kujitukuza alivyoumbika

Nawaza Mateso Waliopata Watu kwa Kutongozana Kabla Simu Hazijaja

Image
Kipindi cha nyuma 1985-2000 simu zilikuwa nadra sana, Lakin pamoja na uchache wa simu, watu walitia maneno mpaka wenza wao wakawaelewa, Kwa wale wa juzi juzi mmerahisishiwa kazi sana, Mtu kipindi hicho anakaa Tabata anamfuatilia msichana wa makumbusho bila hata simu, inabidi apande gari akashuke mwenge atembee mpaka bamaga kwakuwa anahisi msichana yule atapita maeneo yale kama siku alivyomuona akipita nyuma, Na anamkosa, anaamua kurudi home, kesho yake anatia kambi tena lakin hafanikiwi, hii ilileta hamasa kwamba hata akimpata maneno ni hapo hapo, Watu wameng'atwa sana na Mbu wakiwasubiri kina Mwajuma wapite njia fulani kisa wameona anapita asubuhi, Watu wameshinda mtoni wakiwasubiri akina hilda ili wapate nafasi ya kutema yao Watu wameteseka mno, Siku hizi wanaume hata kutongoza imekuwa shida neno linalotangulia ni Naomba namba yake hiyo dada , Hawana uwezo tena wa kumface mwana mke kumtemea cheche live, Siku hizi wamerahisishiwa sana , mwanamke akikunyima namba ya simu unamuomba

Je, Wivu ni Dalili ya Mapenzi ya Dhati au Roho Mbaya?

Image
Leo nimekutana na huu mjadala mahali ulionifanya nilete hilo swali hapo juu. Ni hivii, nimekutana na mtu siku za karibuni na kuanzisha urafiki wa kawaida tu. Sasa katika mazungumzo likaja swala la mapenzi na wivu. Mwenzangu anaamini kuwa na wivu sio mapenzi kwa kuwa, wivu ni dalili ya kumnyima mwenzio kupata kile roho inapenda. Kwamba, kwake yeye hata kama ikitokea akaoa, hatomnyima mke wake kutembea na mwanaume mwingine yeyote atayependa. Tena ikibidi atume na video kabisaa ili impe stimu wakati manzi ake analiwa. Wakuu, je ni kweli wivu ni dalili ya uchoyo? Na kwamba kama unampenda mtu kwa dhati huwezi kuwa mchoyo kwake. Kule uzunguni mume/mke huwa wanapeana nafasi ikitokea mmoja wapo kamtamani mtu mwingine wanakubaliana kuonja. Tuwaeleweje hawa watu? Maana ni binadamu wenzetu. Nawasilisha hoja kwa majadiliano. Karibuni