SEX MACHINE - SEHEMU YA 09
"Nimechanganyikiwa Maida na ndiyo maana nipo hapa kwa ajili moja tu ya kukuuwa." Alisema Salome na kumfanya Maida ashangae na kuangua kicheko kabisa. "Hee! Hivi umechanganyikiwa wewe yaani huoni hata haya eti, niko hapa kwa ajili ya kukuuwa (akabana pua yake kwa vidole viwili na kuifanya sauti itokekee nyembamba ya dhihaka), yaani wewe uniuwe mimi?" "Kwaiyo unashangaa kuwa mimi siwezi kukuuwa au kinachokushangaza ni nini, ngoja uone vile nitakufanyia sasa!" Alisema Salome wakati huo akiwa tayari ameshamsogelea Maida karibu. "Siwezi kukuacha Maida, mimi moyo wangu kwa sasa hauna amani sababu yako. Umeninyang'anya furaha yangu, siwezi kuishi kwa namna hiyo. Chriss hataki hata kuniona mimi sababu yako?" Aliongea kwa uchungu mkubwa sana Salome. Maida alimtazama binti huyo kwa dharau kubwa kisha akatazama pembeni akasema; "Nilidhani labda leo umewekwa style ya mbuzi kagoma kwenda ndiyo umekuja kunihadithia kama kawaida yako kumbe limekush...