HIVI..!,,,MWANAMKE KUMKUBALI MWANAUME KWA UHARAKA ZAIDI NI DALILI YA UMALAYA
![Image](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhrvWJJlSJKSBKTTR6_3RRItEYymKTk7C89atAbDA5F2qKn6ASIlRTvftWEKe0WZW9AdyjfjYADHSMNWjkBDKZ7imh3kpzRTLyf18hMBQquJf-aUKBmLOpOV4LXpbZhOgnj9NvMxhc9fu2K/s1600/WhatsApp-Image-2018-03-09-at-16.18.57-4-300x300.jpg)
Namshukuru Mungu kunifanikisha hadi kuona jua la leo, na namshirikisha kila jambo nifanyalo. Karibuni tukumbushane machache juu ya mapenzi ambayo kila siku tumekuwa tukikumbana nayo, iwe asubuhi, mchana, jioni na usiku. Katika sekunde, dakika ama saa yeyote popote pale duniani. Naweza kutafsiri mapenzi kama hisia nzito zimuingiazo mtu pale moyo wake unapozama katika ulimwengu wa huba kwa yule ampendae, akajikuta kwa lazima isiyoweza kuvumilika ama kukwepeka akampenda mwenzake. Nadhani hakuna mtu asiyejua kupenda, ni wazi hata wewe unajua kupenda na ulishawahi kupenda na kupendwa, kama bado ipo siku mungu atakujaalia utampata umpendaye na akupendaye. Usikate tamaa mwombe mungu atakusaidi yeye ndiye anayejua mume gani au mke gani atakupa. Na kama yupo asiyeweza kupenda basi huenda ana matatizo kisaikolojia na namshauri aende kwa wataamu wa mambo ya saikolojia waliopo karibu nae waweze kumshauri cha kufanya juu ya tatizo lake. Kuna Makala iliyopita nilizungum...