Mwakinyo Aapa Kuua Leo, Mfilipino Aanza Visingizio
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo ameapa kuwa atahakikisha mpinzani wake, Arnel Tinampay raia wa Ufilipino ‘anafia’ ulingoni huku Mfilipino huyo akiomba waamuzi wasifanye upendeleo. Leo Ijumaa mbele ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Majaliwa Kassim ambaye atakuwa mgeni rasmi katika pambano hilo la kimataifa litakalokuwa la raundi 10 litapigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar. Mwakinyo alitoa kauli hiyo ya kibabe wakati wa kupima uzito jana kwenye kituo cha Azam Media, ambapo alisema kuwa atahakikisha mpinzani huyo hamalizi raundi tano na ikiwezekana kummalizia ulingoni kwenye pambano hilo kutokana na maandalizi makali aliyoyafanya. “Binafsi nimejiandaa vizuri kwa kuhakikisha nashinda kwa ushindi mkubwa hapo kesho (leo Ijumaa) kwa kuwa naamini nimefanya maandalizi ya kutosha,” alisema Mwakinyo. Upande wa Tinampay ambaye anatoka kwenye kambi ya bondia maarufu, Manny Pacquao, alisema amekuja nchini kwa kazi moja ya kuhakikisha anamshinda Mwakiny...