RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA THELATHINI NA TATU 33
![Image](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEisprjUrDElVaqmOCXDCsD8pkKRG1CZtOUGuTCaQE9_xn0mRWDRfmtv-OQBi0ZJB4OLWT5QWj0M_TPE6IFTMSWmWg6o5UtvZu1Q5A-AcViP1x3GBxR_30kDEMuI28rfXQsD6qNp1lQt6-8/s320/IMG-20200126-WA0438.jpg)
ENDELEA....... Baada ya kumalizana na yule mganga alituruhusu huku akitupatia masharti ya kawaida sana ambayo kwa yeyote kati yetu angeweza kulitatua. Mshana pamoja na mimi tulimhofia yule kiumbe ambae kwa mujibu wa mganga kuwa tayari kamkamata na hawezi kutoka tena mpaka pale atakapommaliza kabisa na apotelee mbali. Safari yetu ilikuwa yenye wasiwasi mkubwa sana lakini tulijitahidi kufika nyumbani salama bila hata kuwa na kipingamizi chochote. Mshana alizidi kunitia moyo kuwa nisijali kutokana na yale ambayo yanajitokeza. Akili yangu ilibaki kuwaza familia yangu inaendeleaje huko iliko, ghafla gari linaingia pale tulipo na wanashuka Vijana wawili Manyota na Musa ambao moja kwa moja walikuja kunikamata bila hata kujua sababu ni nini zaidi. Walinilazimisha kufika hadi kwenye lile gari ambalo alikuwemo Mzee Paul pamoja na Salha. Nilijua kuwa leo hii kazi ipo na lazima wanifanyie kitu mbaya watu hawa. Walinibeba hadi kufika kwenye nyumba ya moja ambayo sikuweza kuit...