DIVORCE: Sababu ambazo zinaweza vunja ndoa yako
Siku hizi kuingia na kuondoka katika ndoa ni kama mchezo wa ‘cha baba na cha mama’. Hakuna wanaoipa ndoa heshima na hadhi yake kama ilivyokuwa hapo awali .Ndoa thabiti ndio msingi wa jamii endelevu na ishara ya ustawi wa kizazi kijacho .Msukosuko katika ndoa ni ishara ya ukosefu wa msingi katika hatua ya kwanza ya kujenga taifa au jamii yenye mtazamo wa kujenga kikubwa cha kudumu .Je,Mbona kuna talaka nyingi siku hizi? Sababu ndio hizi .. na kuna nyingi zaidi ambazo hazimo katika orodha hii 1. Kutojitolea/kukosa kuaminiana Ingawaje nguzo muhimu ya ndoa ni mtu kujitolea kuwa na mwenzake kwa mbivu na mbichi idadi kubwa ya watu hawajajituma katika ndoa zao na baada ya miaka miwili utepetevu unaanza kuingia katika uhusiano wenu na kila mtu anakosa kumjali mwenzake . Hatua hii hufanya ndoa kukosa mvuto na baadaye kusababisha watu kutaka kutalakiana 2. Usinzi /mahusiano ya nje ya ndoa ‘Mipango ya kando’ ni mojawapo ya sababu kuu ambazo huwafanya watu kutala...