MDADA ZINGATIA HAYA KABLA NA BAADA YA KUOLEWA
![Image](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEigqlnWObUjBwzNXZrlIJRVy1cueYTlSWYcWQ1Jn0ZeZ3rdRd0z7KofHRxqhDAS3GeBX9BxUUaO1dmzDVjOxeSHY-B8Fqfbb-GjDJzvRbXTT3A-8zovmhPm4elYrB3QAdgTkKNXyYvvvGc/s320/download-2.webp)
Naomba kuleta kwenu mambo ambayo naamini ni muhimu kuyatafakari na kuyapa uzito wenye kustahili. Yafuatayo ndiyo mambo ambayo unapaswa kuyazingatia kabla na baada ya kuolewa: 1. Kujitambua Kila msichana aweze kutambua nini kinamfanya kuwa mwanamke. Kwa maana kama ni maumbile hiyo ni default settings, kama ni kuzaa mwanaume haendi leba, sasa ni nini kinakufanya kuwa mwanamke? Kujitambua, kujiheshimu na kuwajibika. Nyumba yenye mwanamke anayeheshimika ni Baraka na nyota njema. Nyumba yenye mwanamke asiyejiheshimu na kuheshimika huwa haitamaniki, wewe wataka kuwa yupi kati yao? 2. Kila mwanaume ni tofauti 'wanaume wote ni wale wale tu'' Ni vibaya sana kumchukulia mwanaume sawa tu na wengine (hata kwa rafiki wa kawaida tu). Kuwa unajua au umesikia sifa mbaya za wanaume flani na flani, au umewahi kuwa na mahusiano na ukaona sifa mbaya kadha wa kadha za huyo, ukaja ukampata mwingine harafu unamchukulia ni sawa na hao wengine tu. (kosa kubwa sana) Kila mwanaume ana sifa za...