Posts

Showing posts from February, 2020

Wakati ambapo unapitia magumu kwenye maisha ni wakati muhimu Sana Kwako…

Image
Wakati ambapo unapitia Magumu kwenye maisha ni wakati Muhimu sana,sio kwa sababu ya Ushindi utakaoupata bali kwa sababu ya stamina unayojenga itakayokusaidia mbele ya safari. Arnold Schwarzenegger aliwahi kusema “Nguvu haiji pale unaposhinda.Changamoto zinazokukabili zinakuimarisha.Unapopitia magumu na kuamua kutokata tamaa,hapo hasa ndio unajenga nguvu za kufanikiwa.(Strength doesn’t come from winning.Your struggles develop your strengths.When you go through hardships and decide not to surrender,that is strength).

SMS Ambayo Itamfanya Mwanamke Akutamani

Image
Unaweza dhania kuwa kutuma ujumbe mfupi kwa mwanamke ili umsisimue haifai. Lakini kusema kwa hakika, inawezekana kumtumia mwanamke SMS ambayo inaweza kumsisimua na pia kupata atenshen kutoka kwake. Hii inaweza kufanya kazi vizuri iwapo umeingiwa na kibaridi cha kuongea na mwanamke moja kwa moja. Kabla ujumbe ufupi kuvumbuliwa, wanaume walikuwa wakifuata mbinu nyingine kuonyesha kuwa wamevutiwa na wanawake waliowapenda. Walikuwa wakituma barua, kuambia rafiki wa rafiki zao ama kuwafuata na kuwapigia mbinja majumbani mwao. Lakini kwa bahati nzuri, hivi sasa kuna SMS, ambazo zina uwezo wa kutuma ujumbe mfupi hapo kwa hapo kwa mwanamke ili kurahisisha kazi yako ya kutongoza. Kabla hujaanza kumvutia mwanamke, ni lazima kwanza umfanye akutambue kwa njia chanya kwanza. Mwanzo haupaswi kutumia SMS kumsisimua mwanamke mpaka ile siku ambayo utapata kumsoma na kumjua zaidi. Lazima ujipatie muda ili ujenge connection kati ya nyinyi wawili ili iweze kufanya kazi. Kufanya hivi kutatoa picha ambayo i

Dah Unaambiwa Gaddafi Alipangwa Kuuawa..Barua Pepe za Siri Kuhusu Mipango ya Kifo Chake Zafichuka

Image
Barua pepe zafichua siri Ufaransa ilivyohusika mauaji ya Gaddafi Baruapepe 3,000 zilizotumwa kwa siri kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani zimefichua namna Ufaransa ilivyohusika katika mauaji ya kiongozi wa zamani wa Libya, Muammar Gaddafi. Toleo la Jumapili la gazeti la Ra’yul-Yaum limeandika kuwa, kufichuliwa yaliyomo kwenye baruapepe hizo 3,000 za siri kumeonyesha kuwa, hamu ambayo Ufaransa ilikuwa nayo ya kulinda na kuendeleza ubeberu wake wa kifedha barani Afrika na kupata hisa kubwa zaidi katika uzalishaji wa mafuta ya Libya, iliifanya nchi hiyo ilitumie shirika la kijeshi la NATO kama nyenzo ya kumpindua Gaddafi. Baruapepe hizo zilitumwa mwezi Aprili mwaka 2011 kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani wakati huo Hillary Clinton. Ndani ya baruapepe hizo yalitajwa malengo matano ya aliyekuwa Rais wa Ufaransa wakati huo Nicolas Sarkozy, ya kuishambulia kijeshi Libya ambayo ni kupata mafuta ya Libya, kuhakikisha Ufaransa inaendelea kuwa na satua na ushawishi katika eneo, k

Dangote achangia mamilioni ili kukabiliana na nzige

Image
Taasisi ya Bill & Melinda Gates imechangia dola za kimarekani milioni 10 (Tsh 23.1 bilioni) kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na nzige wavamizi katika ukanda wa Afrika Mashariki. Mchango huo utakabidhiwa kwa Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) la Umoja wa Mataifa (UN) ambalo limekuwa likiwasihi watu na taasisi mbalimbali kuchangia fedha kukabiliana na nzige wanaohofiwa kusababisha njaa kutokana na kuvamia mazao. Katika salamu zake za shukrani, Mkurugenzi Mtendaji wa FAO, QU Dongyu amesema hadi sasa UN imekusanya shilingi bilioni 76 za kitanzania, huku lengo likiwa ni kukusanya bilioni 318. Nzige hao wamevamia nchi sita za Afrika Mashariki na wana uwezo wa kula chakula sawa na watakachokula watu 35,000 kwa siku moja wakiwa kwenye eneo la kilomita 1 ya mraba, FAO imeeleza. Nzige hao wanazaliana kwa kasi kubwa sana katika mazingira rafiki ambapo ndani ya kipindi cha miezi sita wanauwezo wa kuongezeka kwa zaidi ya mara 500.

Je Mpenzi wako anakupenda kweli au anakudanya?

Image
Moja ya dalili kubwa ya mtu uliyenae kuwa anakupenda, ni heshima anayokupa. Heshima ni nguzo ya upendo katika mapenzi yoyote yale, maana huzalisha neno linaloitwa kipaumbele. Wapenzi wanaoheshimiana, daima hakuna neno ubinafsi bali jambo lao ni lao na si la mtu mmoja mmoja. Maana kila mmoja ulipa kipaumbele jambo la mwenzake. Upendo huonyeshwa kwa vitendo, na moja ya matendo makubwa ya upendo ni ile heshima unayoipata kutoka kwa mpenzi wako, na ile unayoitoa wewe. Mpenzi wako anapokuambia ninakuheshimu, ni vinzuri akaonyesha kwa vitendo. Na hiyo ndiyo dalili ya kuwa, mpenzi wako anakupenda kweli na si kwa maneno tu. Siku zote heshima inapoanza kupungua katika upendo wenu, ni moja ya dalili kubwa ya kuanza kuchokana. Kumbuka yeyote anayekupenda, basi atakuheshimu. Na mwenye kukuheshimu kila wakati, huyo ndiyo mwenye mapenzi ya dhati kwako. Maana atakujali na kukuthamini kwa jinsi ulivyo.

Kisa Corona: Juventus v Inter Milan kuchezwa bila ya mashabiki

Image
Kusambaa kwa virusi vya Corona imekuwa ni janga kwa soka Italia baada ya mechi tano za Serie A ikiwamo ya Juventus dhidi ya Inter Milan zitachezwa bila ya mashabiki. Mechi nyingine ni zile za Udinese, AC Milan, Parma na Sassuolo zote zitachezwa bila ya mashabiki. Michezo ya Lazio, Napoli, Lecce na Cagliari yenyewe mashabiki wataingia kama kawaida, lakini mechi ya Jumatatu ya Sampdoria bado hawajatoa uamuzi. Serikali ya Italia imewazuia wakazi wa miji ya kaskazini kutembea baada ya watu 229 kupatikana na virusi hivyo huku watu saba wakiwa wamekufa. Mechi ya Inter Milan ya Europa Ligi hatua 32 bora dhidi ya Ludogorets kesho Alhamisi itachezwa bila ya mashabiki kutokana na kuhofia kusambaa kwa ugonjwa huo. Inter ni moja ya timu nne za Serie A ambazo wiki iliyopita walihairisha mechi zao kutokana na hofu ya ugonjwa huo. Vinara wa ligi Juventus wapo mbele kwa pointi moja kwa Lazio inayoshika nafasi ya pili kabla ya mchezo wake wa Jumapili dhidi ya Inter inayoshika nafasi ya tatu. Ratiba ya

Siku hatari za kushika mimba ni zipi?

Image
Habari za asubuhi wapendwa wafuatiliaji wa blog hii! kabla ya kuanza mada hii ya leo napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu kuweza kuniamsha salama nikiwa na afya njema. Mada yangu leo inahusu siku za hatari ambazo mwanamke akifanya ngono bila kinga basi anakuwa katika hatari ya kushika mimba. Nimeamua kutoa mada hii baada ya kugundua kuwa ongezeko la matukio ya utoaji mimba, utupaji wa watoto na hata kuwa na watoto wa mitaani yanasababishwa zaidi na mimba ambazo hazikutarajiwa ambazo zingine zinatokana na mzazi kutokujua siku yake ya hatari ili kujikinga. Ni muhimu sana kwa mwanamke kujua mzunguko wake wa hedhi, mizunguko hiyo iko katika makundi makuu matatu3 ambayo ni : mzunguko mfupi(siku25 kurudi nyuma), mzunguko wa kawaida(siku28) na mzunguko mrefu(siku30-35) Wanawake wengi mzunguko wao huwa ni wa kawaida yaani siku 28 hawa ndio leo nitawaongelea zaidi. #Namna ya kuutambua mzunguko wako Ili kutambua mzunguko wako ni wa siku ngapi unatakiwa kuhesabu kuanzia siku y

Mgonjwa wa Corona Ujerumani yuko mahututi

Image
Wizara ya afya ya jimbo la North Rhine Wesphalia nchini Ujerumani imesema hii leo kwamba mtu alliyeambukizwa virusi vya Corona yuko katika hali mbaya na amepelekwa kwenye hospitali ya madaktari bingwa iliyoko kwenye mji wa Duesseldorf.  Kulingana na wizara hiyo, mtu huyo anayetokea mji wa Erkelenz karibu na mpaka wa Uholanzi kwa mara ya kwanza alilazwa siku ya Jumatatu akiwa na homa kali ya mapafu. Lakini baadae aligundulika kuambukizwa virusi hivyo na kutengwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kabla ya kupelekwa Duesseldorf. Mke wake pia ametengwa kufuatia wasiwasi kwamba ameambukizwa virusi hivyo baada ya kuanza kuonyesha dalili. Tayari watu 80,000 wameambukizwa virusi hivyo kote duniani, huku Ujerumani ikiwa ni wagonjwa 17, idadi hii ikiwa ni kulingana na shirika la afya ulimwenguni, WHO.

Lunch Time inavyotumiwa na Wafanyakazi Wanandoa Kuchepuka

Image
Usije ukajidanganya kumuona mumeo au mkeo eti anarudi nyumbani mapema na weekend hatoki ukadhani uko salama. Sasa hivi ile lunch time kuanzia saa saba mpaka nane huko maofisini ibilisi anakuwa ameshika usukani, ikizingatiwa sasa kuna mahotel mazuri pande kariakoo, manzese, magomeni zile zinakuwa zimejaa ikifika muda huo, wake za watu na waume za watu wanakuwa wanacheza mechi za kirafiki watch out. Hili halina ubishi

Imevuja! ‘Nandy Ametupiwa Jini’

Image
DUNIA ina mambo mengi sana! Unaweza kusema hivyo kutokana na aliyoyasema Mchungaji wa Kanisa la The World of Reconciliation Ministries (WRM) lililopo Kivule, Matembele ya Pili, Ukonga jijini Dar, Nabii Nicholaus Suguye kwamba mwanamuziki wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ ametupiwa jini. Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Nabii Suguye alisema Nandy alipofika kanisani hapo aligundua alikuwa ametupiwa jini na maadui zake akiwa jukwaani ili safari yake ya maisha ya kimuziki isiwe na mafanikio ambapo alijikuta akiishiwa nguvu. Amejuaje? Nabii Suguye alitoa siri hiyo hivi karibuni ambapo alisema Nandy alifika kanisani kwake na kutaka amuombee, hivyo wakati wa maombi hayo ndipo akagundua kwamba Nandy ametupiwa jini ili limmalize akiwa jukwaani, lakini Mungu akamnusuru. Aliendelea kusema kuwa, Nandy alipatwa na mkasa huo kwenye moja ya shoo zake akiwa jukwaani, hivyo aliamua kufika kanisani hapo kwa maombi. “Kwanza mimi Nandy nilikuwa simjui. Nilikuwa ninaendelea na ratiba zangu,

Iran: Wagonjwa walioambukizwa virusi vya Corona wafariki

Image
Watu wawili walioambukizwa virusi vya Corona nchini Iran wamefariki, na kufikisha idadi ya waliofariki nchini humo kuwa watu 16, maafisa wamesema leo, wakati Wairan wakiwa na hofu kuwa huenda viongozi hawatilii maanani kiwango cha maambukizi. Iran ina idadi kubwa ya vifo kutokana na virusi vya Corona nje ya China, ambako virusi hivyo vilianzia mwishoni mwa mwaka 2019. Miongoni mwa wale walioambukizwa ni pamoja na naibu waziri wa afya, ambaye alipatikana kuwa ameambukizwa virusi hivyo vya Corona. Maambukizi mapya ya virusi vya Corona vimethibitishwa leo nchini Italia pamoja na Austria, Croatia na nchini Uhispania, masaa kadhaa kabla ya mkutano wa mawaziri wa afya wa Umoja wa Ulaya unaofanyika leo. Waziri mkuu wa Croatia Andrej Plenkovic amesema nchi hiyo ina mgonjwa mmoja.Idadi jumla ya wagonjwa nchini Italia imepanda hadi watu 283, ikiwa ni ongezeko la watu 54 kuanzia jana jioni.

Mazoezi 3 ya Haraka ya Kunenepesha na Kurembesha Makalio

Image
Hakuna mwanamke asiyependa kuwa na umbo la kupendeza na umbo bila tako si umbo. Wengi wanawake hufanya kila nia kuhakikisha kuwa wanapata umbo wanalotaka, wengine wakienda kiasi cha kufanyiwa upasuaji na wengine kutumia matembe almuradi wawe na makali mazito. Si hayo tu wapo baadhi ambao huvalia nguo kadhaa ama kutumia makalia bandia ili kuonekana warembo. Hizi hapa njia rahisi za kunenepesha makalio bila kupata taabu yoyote. Kuinama Simama imara na uhakikishe kuwa mgongo wako umelainika kisha uiname sawa na mtu anayetaka kukaa hakikisha kuwa magoti yako hayapiti viganja vya miguu. Rudia hii mara 3 hadi unapokamilisha raundi 20. Kuruka na kuinama Panua miguu huku umesimama kisha uiname na kutia mikono miwili kati kakati ya miguu chini. Rudia hii mara kadhaa huku ukiruka na kurudi katika nafasi hiyo hiyo. Hakikisha kuwa unanyoosha magoti ukiendelea kuridia zoezi hili. Kuinukia kwa mgongo Lala kichalichali  kisha uikunje miguu na mikono yako iuweke kando kando. Kaza mikono kisha uinuke k

Huyu Hapa Mwanamke Aliyetangaza Twitter Anataka Kuolewa Kwa Mahari ya Bilion 2

Image
Mrembo huyo wa Nigeria kwa jina la Gbemi amejitosa twitter kueleza kuwa yeye kuolewa lazima mwanaume atoe mahari ya dola U$1 million sawa na zaidi ya billion 2 za Kibongo. Yani kamwacha Diva mbali kwenye Dau

Unaambiwa Hamisa Mobetto Atamani Kuwa MKE wa Nne wa Dr Mwaka..

Image
Hamisa Mobetto atamani kuwa mke wa nne wa Dkt Mwaka… Aonesha Hisia zake kwa kumpost Picha ya Dr Mwaka katika insta story yake, hii imekuja baada ya Dr Mwaka kuwa Gumzo wiki iliyopita baada ya kutambulisha wake zake wawili ambao wanapika chungu kimoja waswahili tunasema wanaiva mpaka kufikia kulala chumba kimoja na mme wao…. Katika Dini ya Uislamu mwanaume anaruhusiwa kuoa wake mpaka Wanne hivyo kama inampendeza Dr Mwaka anaweza futa jiko la nne

KOVU LA MOYO 40.

Image
Chozi la uchungu lilitoka katika mboni za macho ya Robby ... Hakutegemea kama siku moja angekuja kukutana na binadamu aliotokea kuwapenda na kuvutiwa na mwenendo wa Maisha yao kama Poshie na Angelo  Nini kimewasibu? ... Ndilo swali ambalo Robby lilikuwa likimchanganya .. wote walikuwa wamepata majeraha makubwa lakini Angelo alikuwa akionekana ni mtu aliyetoka kuumia muda si mrefu ... pingu aliyokuwa amefungwa Angelo ilizidi kumchanganya na kuanza kuhisi labda Angelo na Poshie wote wamefanya tukio la Ujambazi au Angelo atakuwa amemfanyia kitu kibaya mwenzake na Wananchi wamemshambulia yeye.  Yalikuwa ni maswali ambayo Robby alikuwa akijiuliza kichwani mwake bila ya kupata jibu kamili lakini ukweli ulibaki kwa Poshie na Angelo nini kiliwatokea nafikiri msomaji wewe unajua.  Robby hakuwahi kukutana na hali ya udhuni katika maisha yake, kama jinsi alivyokutana nayo siku hiyo. Alibaki ameduwaa na hasijue la kufanya, huku akiwa amepoteza kabisa kumbukumbu ya nini ilichompeleka hapo hospitali

KOVU LA MOYO 39

Image
&t;br />  Chozi la uchungu lilimmwagika Aisha hakuamini kabisa kama Dr Ally anaweza kumgeuka na kumfanyia alichomfanyia....  "Nashukuru sana Ally kwa ulichonifanyia ila naomba utambue kuwa nimefanya yote kwa sababu yako ... Nakupenda na nitaendelea kukupenda" ..... Aisha aliongea kwa uchungu akimwambia Dr Ally lakini ndiyo hivyo tena alikuwa mikononi mwa polisi  Alichukuliwa kwa mahojiano zaidi lakini alikana kuhuusika na kupotea kwa Poshie wala hajui chochote kuhusu hao watu waliomteka japokuwa alimwambia Dr Ally pale kuwa yeye ana watu wa kazi na wanaweza kuifanya kazi ya kumteka Poshie na akarudisha pesa aliyoiiba .... "Sikiliza nikuambie Binti, huu muda unaonipotezea utakuja kuujutia, ni bora ukasema kabla sijaamua kukupeleka wanapopelekwaga watu vibuli na wakaidi kwa sababu nakuona wewe ni Msichana mdogo sana na isitoshe wewe ni Mrembo sana" ... Afande Mmoja mwenye sura ya upole alijaribu kuongea na Aisha baada ya kukana kuwa yeye hausiki na upotevu wa P

KOVU LA MOYO 38

Image
Poshie alianguka kama mzigo na kupoteza fahamu huku damu nyingi zikimmwagika..  "Bila shaka atakuwa amekufa huyu!" ... Kijana mmoja mrefu mweusi mwenye mwili wa mazoezi alimwambia Aisha huku akiwa anamgeuza Poshie ... Aisha alicheka kicheko cha kebehi na kumkanyaga Poshie .. "Samahani sana Poshie kwa nilichokufanyia ila naomba utambue kuwa mimi ni Mwanamke kama wewe na Mume anauma kuliko uchungu wa kuzaa" ... "Siyo bure Aisha, lazima utakuwa umechanganyikiwa!" ... Yule kijana alimuuliza huku akimtazama kwa makini ... "Kwanini unasema hivyo Meja?" ... "Unawezaje kuzungumza na Maiti wakati hakusikii?" ... "Kimwili hatupo naye ila kiroho tupo naye na anasikia kila jambo" ... Aisha alijibu kwa kujiamini na kuwaamuru waondoke eneo lile haraka na kumuacha Poshie pale  ****  Ujinga waliofanya waliotumwa na Aisha ni kutokagua ndani kwa Poshie kulikuwa na nani mwengine anayeishi mule .. Walikuwa wamemuacha Dada wa kazi ambaye alishuudi

KOVU LA MOYO 37

Image
Moyo wa Poshie ulimuenda mbio na kuanza kumuogopa Dr Ally.  Hakuamini kama inaweza kuwa zawadi njema kwake  Dr Ally alitoa kitambaa na kumwambia Poshie .... "Funga macho yako" .. Poshie huku akiwa anahema kwa wasiwasi akafunga Macho yake ... Dr Ally akamfuata na kutaka kumfunga kile kitambaa lakini Poshie akafungua macho yake... "Mbona unafungua macho wakati nimekuambia ufunge?" ... "Sijui kwanini nimefungua lakini Moyo wangu unaenda mbio na najihisi kama ni mtu mwenye mashaka. Zawadi yako ni njema juu yangu?" .... "Safi sana Poshie Kila siku unanifanya nizidi kujipongeza kwa mimi kukufahamu wewe unajua kwanini?" ... Dr Ally alifurahi na kumuuliza tena swali .... "Sijui kwanini? Lakini mbona unaniuliza swali badala ya kujibu swali?" ...  Dr Ally alicheka kidogo kisha akamjibu .... "Muda mwingine ni vyema kujibu mtu kwa kumuuliza swali ili umpe uwezo wa yeye kuweza kuchanganua baadhi ya mambo hata mimi nikiwa sipo" .... "S

KOVU LA MOYO 36

Image
Poshie alikuwa akitembea bila ya kujua kama nyuma yake kulikuwa na mtu amempania na alikuwa anataka kumuua  Aisha alimuona Poshie na alizidi kukanyaga mafuta huku akiwa amemng'atia meno Poshie ili amgonge na kumuua palepale  Unaweza kuona Binaadamu na Wanyama wote tupo sawa kwa sababu wao pia wanazaa kwa uchungu kama sisi pamoja na kunyonyesha, lakini binaadamu na Wanyama tuna tofauti kubwa sana. Na tofauti yao kubwa na sisi ni kwamba Mnyama amenyimwa uwezo wa kufikiri na kujitambua kwa kile akifanyacho .. Mnyama anaweza kumdhuru mwenzake kwa bahati mbaya au kwa makusudi lakini hasimuombe msamaha zaidi ya kujikung'uta na kuishia zake .. Ndio mana Binadamu ukimfanyia kitendo cha kikatiri binadamu mwenzako basi wewe unaitwa Mnyama maana yake haupo kabisa katika kundi la Binaadamu  Hivyo basi kwa kitendo ambacho Aisha alikuwa akitaka kwenda kumfanyia Poshie Dhaili alionesha ni jinsi gani alivyokuwa Mnyama.  Akiwa anakaribia kumfikia Poshie ghafla akaingia Mtoto wa shule barabarani

Hemedy “Nataka Kushughulikia vijana wa Taifa Hili”

Image
Hemedy PHD ni mmoja wa wasanii ambao ameajaliwa kuwa na watoto wengi ambao kila mmoja ana mama yake, amefunguka kusema bado ataendelea  na tabia hiyo kwa sababu mbegu yake ni adimu na yupo vizuri kuwashughulikia vijana wa taifa hili. Akiieleza EATV & EA Radio Digital, Hemedy PHD amesema yeye bado hajaoa na hategemi kuoa siku za hivi karibuni, na mbegu yake bado ni mbichi pia anatumia “mkongo” ili kufanya shughuli hiyo. “Bado sijaoa mbegu yangu ni mbichi natumia mkongo kila siku, tegemea watoto wengi sana hii mbegu ni adimu, sijui nitakuwa nao wangapi kwa sababu watoto ni majaliwa ya Mungu ila nina mkongo wa kutosha kuwashughulikia vijana wa taifa hili” amesema Hemedy PHD. Msanii huyo wa filamu na muziki ameendelea kusema  “Haimaanishi ukiona mwenzako ameoa na wewe ufanye hivyo, mwisho wa siku utakuja kuchukuliwa mkeo  utakuwa umeolea watu wengine, bora uchukue muda wa kuchagua mwanamke atakayekufaa na kukuelewa wewe” ameongeza

KOVU LA MOYO 35

Image
Poshie alimtazama kwa uoga huku akitetemeka na hasijue nini chakufanya .. Wakati yule jamaa anavua nguo Poshie haraka akapata wazo..  Poshie Alinyanyuka na kumuweka mwanawe vizuri na kumwita yule kaka .. "Unataka kwenda wapi" ... Yule jamaa almshika mkono na kumzuia ... "nilikuwa nataka twende tukafanyie pale hapa pamekaa vibaya" ... Poshie alimwambia kwa sauti fulani ya kudeka ili kumlegeza yule kijana kisha akamfanyie kama alivyomfanyia yule Mlinzi ... "Sikiliza nikwambie Unapotaka kulalia wewe, Mimi nimeshaamka siku nyingi. Sina muda wa kupoteza na wewe inama unipe mambo" .. Yule kijana alimwambia huku akiwa amechukia ... "Lakini kwanini Kaka umeamua kunifanyia hivi, Mimi ni mtotio wa kike kama alivyo mama yako au Dada yako pale nyumbani kwenu" .. "Sikiliza nikuambie binti, Mimi sina muda wa kuanza kupokea hayo maubiri yako nimekwambia inama usitake kunichelewesha, kama kweli ulikuwa unayajua hayo, pale ulitaka kwenda kufanya nini? kuna k

KOVU LA MOYO 33

Image
Poshie alistuka na kumtazama na kumsukuma yule kijana kwa nguvu, kisha akachukua shuka na kujifunika huku akihema kwa nguvu  "Unataka nini?" .... Poshie alimuuliza kwa sauti huku akihema kwa nguvu ... "Swali gani ilo unaloniuliza? inamana mimi mpaka nimekuvua nguo haujui nataka nini kwako?" ... Yule kijana alimjibu Poshie huku akizidi kumsogelea ... "Inamana unataka kuniambia ulikuwa ukitaka kufanya mapenzi na Mimi?" ... "Ndio maana yake, mbona maswali mengi kama tupo mahakamani?" ... Yule kijana aliongea na kuzidi kuvua nguo zake na kubaki kama alivyo.  Poshie alilia sana na kumuomba hasimfanyie anachotaka kumfanyia .... "Tafadhali nakuomba sana Kaka, Mimi ni mtoto wa kike naamini hata wewe kwenu utakuwa na ndugu kama mimi sasa unavyoamua kunifanyia ukatiri ni sawa kama umemfanyia Dada yako au Mama yako Mzazi" ... Yule jamaa lilimtoka kofi la nguvu lililomsukuma poshie mpaka ukutani .... "Maneno gani unayoniambia wewe? Yani mimi n