Chagua Kufanya Mambo Haya, Ili Yakupe Mafanikio Makubwa
![Image](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhAZmxBbBi_uvNXek2piksuq1aIPUggWjouz8A6llF6cZOiAgiCGOhvX5Ar8u7GjcAmB6dnoSLmllsz_7n_xl5pxCDXxhIiDD5rrTglgFWg4UreLOt2CBqjV9PbOt1js2tZ95LIqnNDdrsc/s1600/chagua.jpg)
Siku zote maisha ya binadamu yanaongozwa na uchaguzi tunaoufanya kila siku. Uchaguzi huo ndio unatufanya tuwe na maisha haya au yale. Kama uchaguzi unaoufanya ni mbovu kila siku, basi ni wazi na maisha yatakuwa mabovu vilevile. Na kama uchaguzi wako ni mzuri, halikadharika na maisha yako yatakuwa mazuri vivyo hivyo. Kitu cha kuwa makini nacho hapa, angalia uchaguzi unaoufanya kila siku na kila wakati. Uchaguzi huo ndio unaoamua maisha yako ya kesho yaweje. Kama ni hivyo, ni lazima kwetu kufanya uchaguzi utakaotupa maisha bora. Jaribu kujiuliza, ni uchaguzi wa mambo gani unaotakiwa kuufanya ili kukupa mafanikio makubwa? 1. Chagua kutumia fursa vizuri. Kwa fursa yoyote inayojitokeza mbele yako, jifunze kuitumia vizuri. Kama ni fursa ya kibiashara au elimu itumie vizuri mpaka uone mafanikio yake. Acha kucheza na fursa yoyote ya kimafanikio inayojitokeza mbele yako. Ikiwa utafanya hivyo elewa ni lazima ipo siku utakuja kujuta kwa uamuzi ulioufanya leo. Kuna watu ambao wameshindwa kufa...